in , ,

SERENGETI BOYS ITUPE FUNZO KWENYE MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA

Serengeti boys

Mechi dhidi ya Cameroon ilikuwa mechi ya tatu (3) kati ya mechi za
kirafiki ilizopangiwa Serengeti boys kabla haijaenda kushiriki
michuano ya Afcon kwa vijana nchini Gabon.

Mechi tatu zilizopita wameshinda mechi zote tatu huku wakifunga goli 5
na kuruhusu magoli 2 na kizuri zaidi ilicheza na timu ambazo
zinashiriki michunao hiyo ya Afcon kwa vijana ikiwemo mwenyeji Gabon.

Matokeo ambayo kwa kiasi kikubwa yamejenga vitu viwili kwao na kwetu
sisi mashabiki na wadau mbalimbali wa soka.

Kitu cha kwanza ambacho wanazidi kukipata Serengeti boys ni kujijengea
hali ya kujiamini kati yao kwani mechi ambazo wamecheza, wamecheza
dhidi ya timu ambayo ni mwenyeji ambayo ni Gabon, na wamecheza dhidi
ya timu yenye jina kubwa barani Afrika na yenye maendeleo makubwa ya
mpira barani Afrika yani Cameroon.

Kucheza na mwenyeji na kuwafunga katika mechi mbili mfululizo kulikuwa
kuna maana kubwa sana katika kujenga morali ya wachezaji.

Kuwafunga pia Cameroon tena kwao kulikuwa kuna maana kubwa sana
kujenga hali ya kujiamini kwa wachezaji kwani walifanikiwa kuifunga
timu yenye jina kubwa katika soka barani Afrika.

Na pia ushindi huu wa mechi tatu mfululizo utakuwa umejenga kwa kiasi
kikubwa tabia ya ushindi ndani ya kikosi cha Serengeti boys, timu
yoyote ikifanikiwa kuwekeza hali ya ushindi ndani ya vichwa vya
wachezaji inakuwa na faida kubwa sana katika kupambania ushindi.

Kila mechi wachezaji huingia uwanjani wakitaka ushindi, kwao bila
ushindi huona siku haijakamilika hivo ili kukamilisha siku hupigana
kadri ya uwezo wao kupata ushindi.

Kwetu sisi mashabiki na wadau wakubwa wa michezo kuna vitu viwili
ambavyo tunatakiwa tujifunze kwa ukaribu katika maendeleo haya ya
Serengeti boys.

Kuhamasika kwetu dhidi ya timu yetu ndicho kitu cha msingi kwetu, na
tusiishie kuhamasika peke yake ila pia tuiunge mkono kwa kuichangia
timu hii ili iweze kupata motisha ya kupambana ifanye vizuri katika
michezo ya Afcon na ifanikiwe kufika katika fainali za vijana za kombe
la dunia zitakazofanyika India.

Kitu cha pili ambacho ni cha msingi sana ni kuhusu maendeleo ya soka
la vijana nchini kwetu.

Ni wakati sahihi kwa wadau wote kuhamasika kwa kiasi kikubwa kushiriki
kwa kila mmoja upande wake katika maendeleo ya soka la vijana.

Ukiangalia asilimia kubwa ya wachezaji wa Serengeti boys waliopo sasa
wanalelewa na kutunzwa na TFF, hii ni tofauti na sehemu zingine.

Nchi zingine chama cha soka huhusika kuandaa mazingira mazuri ya timu
zao za Taifa na siyo kutengeneza wachezaji.

Kikosi cha Ghana cha chini ya umri wa miaka 17 kitakachoshiriki pia
hiyo michuano ya Afcon nchini Gabon, kilichotangazwa wiki iliyopita
asilimia kubwa ya wachezaji wake wametoka katika vituo vya michezo
pamoja na vilabu mbalimbali nchini humo.

Hii inafaida kubwa sana kwani wachezaji hawa hukulia na kukaa katika
mazingira ambayo wanafundishwa soka kwa muda mwingi kutoka kwa
wataalamu wa soka la vijana wa vituo vya soka la vijana au klabu
husika.

Hivo kuipunguzia mzigo chama cha soka katika kuendeleza viwango vya
wachezaji hawa tofauti na sisi ambavyo tumetegemea TFF ndiyo ihusike
kwenye kila kitu katika maendeleo ya vijana hawa.

Mpira siku hizi ni biashara kubwa sana, kuanzisha kituo cha kukuja
vipaji vya watoto katika soka kuna faida kubwa sana kibiashara kwa
sababu unakuwa na mkataba na mchezaji husika kiasi kwamba siku
akitakiwa na timu yoyote unanufaika katika pesa ya mauzo.

Vilabu vingi vimekuwa vikitafuta namna ya kuongeza njia za mapato,
kuwa na timu za vijana ni aina mojawapo kubwa ya kuongeza mapato ya
klabu.

Pamoja na kwamba Taifa litanufaika kupata wachezaji bora katika timu
za taifa kuanzia za vijana mpaka za wakubwa, lakini Klabu itakuwa
inanufaika na mchezaji huyo mpaka pale atakapostaafu kucheza soka.

Mfano kama klabu yenye uwekezaji mzuri katika soka la vijana
ikifanikiwa kuuza wachezaji Zanako ya Zambia itanufaika katika pesa ya
usajili. Haitoishia hapo tu kama Zanako watamuuza mchezaji huyo
Arsenal, klabu iliyohusika kumlea mchezaji huyo itanufaika na asilimia
kadhaa ya pesa hiyo ya usajili wa kutoka Zanako kwenda Arsenal.

Kwa mtiririko huu, klabu ikizalisha wachezaji watatu itanufaika kwa
asilimia kubwa sana kipesa.

Muda huu Serengeti boys itashiriki Afcon na Mungu atajalia itaenda
India kushiriki kombe la dunia, mawakala wa wachezaji watawaona na
kuwatafutia soko, hapo TFF itanufaika kwa kiasi kikubwa sana.

Hivo ni wakati sahihi kwa mtu mmoja mmoja, taasisi, vilabu vya mpira
wa miguu na vituo vya kulea na kukuza vipaji vya soka kuingia moja kwa
moja kwenye maendeleo ya)c soka la vijana kibiashara zaidi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MAENEO AMBAYO YALIWAPA NGUVU YA USHINDI SPURS DHIDI YA ARSENAL JANA

Tanzania Sports

JUVENTUS NA REAL MADRID WANA 60% YA KWENDA CARDIFF