in , , ,

SABABU KWANINI SPURS WATASHINDA DHIDI YA ARSENAL

Miaka 22 imepita bila ya Spurs kumaliza ligi mbele ya Arsenal.

Msimu huu wana nafasi kuɓwa sana ya kumaliza mbele ya Arsenal. Ushindi
wa mechi ya leo unataipa nafasi Spurs ya kumaliza mbele ya Arsenal
hivo kutowapa nafasi Arsenal kuwa St. Totteringham’s Day.

Arsenal huwa wanafanya sherehe kila wakimaliza mbele ya Spurs kwenye
ligi kitu ambacho kimekuwa kinawaudhi Spurs kwa muda mrefu.

Wachezaji wa Arsenal…

Kwa miaka 22 mfululizo, Spurs wamekuwa wakisononeka sana, nafasi hii
waliyonayo ya kuifuta sherehe hii mwaka huu itakuwa chachu kubwa ya
kupigania ushindi siku ya leo ili wazike ndoto za Arsenal kumaliza
mbele ya Spurs kwa miaka 23 na kuifuta rasmi St. Totteringham’s Day

2: Safu kali ya Ushambuliaji ya Spurs vs Safu mbovu ya Ulinzi ya Arsenal.

Kwa misimu mitatu mfululizo Harry Kane amefanikiwa kumaliza kila msimu
akiwa na goli 20+

Delle Alli na Harry Kane kwa pamoja wamefanikiwa kufunga magoli 36
kwenye mechi 69 kwa pamoja msimu huu kwenye ligi kuu ya England

Delle Ali akifunga goli 16 na Harry Kane akifunga goli 20.

Son amefunga goli 12 wakati Christian Ericksen akiwa amefunga goli 8
na kutoa pasi za mwisho za magoli 8. Safu hii ya ushambuliaji inaenda
kukutana na Arsenal ambayo imeruhusu magoli 40 msimu huu.

Ukiangalia uwezo mkubwa wa safu ya ushambuliaji ya spurs na uwezo
hafifu wa safu ya ulinzi ya Arsenal inakupa picha kuwa Spurs
wanauhakika wa kupata goli muda wowote ule ndani ya mchezo.

3: Uwezo wa Pochettino.

Tangia aichukue Spurs amefanikiwa kuifanya kuwa timu ambayo
inashinɗania uɓingwa na siyo kuingia top 4 tena.

Na amewaamini vijana wenye umri mdogo kuwa wapiganaji kwenye vita hii
kitu ambacho kinawapa moyo wachezaji wa Spurs kupigana muda wote ili
wasivunje imani ya kocha wao kwao.

Pochettino ameifanya timu icheze vizuri na ipigane kwa kiasi kikubwa
na hii inawapa nafasi kubwa ya kushinda leo.

4: Safu imara ya Ulinzi.

Mpaka sasa Spurs imefungwa magoli 22 na ina clean sheets 14 kitu
ambacho kinaipa nafasi kwao kuwa ni timu ngumu ambayo haifungiki
virahisi.

5:Matokeo mazuri ya uwanja wao na faida ya uwanja wa nyumbani.

AW

Hali ya hewa ya White hart ƙline itakuwa nguzo imara kwa matokeo
chanya kwa Spurs kwa sababu watakuwa na watu nyuma yao ambao watakuwa
wanawaunga mkono kwa hali kubwa hii itawapa nafasi kubwa Spurs ya
kupigana zaidi kutafuta ushindi.

Pia kwa msimu huu Spurs anamatokeo mazuri kwenye uwanja wake wa
nyumbani kwani amepoteza points 4 pekee na kufungwa goli nane kwenye
uwanja wake wa nyumbani kwa matokeo haya yanaonesha wanayo nafasi
kubwa ya wao kushinda mechi ya leo.

6: Viwango vya timu katika mechi zilizopita.

Spurs wameshinda mechi 8 zilizopita za ligi kuu ya England wakati
Arsenal katika mechi 5 zilizopita wameshinɗa mechi moja tu.

Kitu kinachoonesha Spurs wapo katika hali nzuri ya ushindani kuliko Arsenal.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Hii ya kadi za njano ni fedheha kwa TFF

Tanzania Sports

MAENEO AMBAYO YALIWAPA NGUVU YA USHINDI SPURS DHIDI YA ARSENAL JANA