HATA kama uongozi hausemi kuwa una hasira ya kipigo walichopata dhidi ya Arsenal, ni dhahiri Real Madrid imeamua kuingia soko la usajili ikiwa imekabwa kooni na ndonge la hasira. Matendo yanayoendelea katika maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia ngazi ya klabu na msimu ujao ni dhahiri yanatokana na mabao matano ya Arsenal katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal.
Real Madrid ilichapwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu unaoisha. Kisha katika mchezo wa marudiano kwenye dimba la Snatiago Bernabeu, Real Madrid ilichabangwa mabao 2-1 na kuhitimisha safari yake ya kutetea taji hilo kubwa barani Ulaya. TANZANIASPORTS inachambua sababu za Real Madrid kwenda kwa kasi katika soko la usajili na hatima ya mastaa wa timu hiyo kuelekea msimu ujao.
Safu ya ulinzi
Real Madrid ilifungwa na Arsenal kutokana na makosa ya wachezaji binafsi pamoja na kuzidiwa maarifa na wapinzani wao. Katika mchezo wa kwanza mabao mawili yalitokana na adhabu ndogo na yalifungwa na Declane Rice. Bao la tatu lilitokana na mpango wa Arsenal kulisakama lango la Real Madrid. Kutokana na safu ya ulinzi kuwapoteza wachezaji wake muhimu, Dani Carvajal, Eder Militao, David Alaba, timu hiyo iliwategemea Lucas Vazquez kama beki wa kulia, huku upande wa kushoto ukiwa hauna mwenyewe kwani ulianza na David Alaba na baadaye akamalizia Fran Garcia huku Ferland Mendy akiwa majeruhi.
Alaba alipangwa kwenye mchezo huo akitokea majeruhi, lakini kocha Carlo Ancelotti alifanya hesabu vibaya kumpanga nyota huyo ambaye msimu huu amekumbwa na majeraha. Hata hivyo taarifa za ndani toka klabuni hapo zimebainisha kuwa maombi ya Ancelotti mwanzoni mwa msimu huu hayakufanyiwa kazi, kwani alihitaji beki wa kati, beki wa na kushoto.
Kutokana na kutosajiliwa wapya alitakiwa kutumia wachezaji waliokuwepo. Hata hivyo, kufungwa na kuvuliwa taji la Arsenal huenda ndicho kitu kilichowaamsha usingizini viongozi w aklabu hiyo. Usajili wa sasa ni umeegemea upande wa nafasi ya ulinzi, ambapo Trent Alexandre Anold toka Liverpool, Huidjsen toka Bournemouth na Mastarnouno toka Argentina. Wachezaji hawa ni beki w akati, kulia na kushoto. Pia anawindwa beki mwingine wa kushoto.
Kama kuna ubovu uliowagharimu Real Madrid basi ni eneo hili. Timu hyo ilicheza huku baadhi ya wachezaji wakiwa majeruhi akiwemo Antonio Rudiger. Pia ikalazimika kuwategemea makinda Raul Asencio na Jacobo, lakini kabla hawajabeba majukumu yao, Jacobo akapata maumivu hivyo akaliacha jukumu kwa Asencio.
Kwa upande wa Raul Asencio alikuwa kinda ambaye amebeba majukumu kuliko ilivyotarajiwa, akiwa amecheza chini ya Rudiger katika mechi kadhaa na baadaye chini ya Aulien Tchouameni. Hata hivyo Aulien Tchouameni ni kiungo mkabaji lakini baadhi ya nyakati alitakiwa kucheza kama beki wa kati hususani mechi didi ya Arsenal.
Upande wa kulia Lucas Vaquez alichezeshwa kama beki kutokana na kuumia kwa Carvajal, lakini pia Vazquez ni winga ambaye amebadilishiwa nafasi na kucheza kama beki wa kulia. Na anakuwa beki mzuri pale timu inaposhambulia, kuliko inapozidiwa na wapinzani.
Usajili wa sasa unaofanywa na Florentino Perez unadhihirisha kuwa timu yake ilikuwa na upungufu kwenye eneo la ulinzi. Wakati Juses Vallejo anaondoka, hivyo nafasi ya ujio wa beki w akati ilikuwa muhimu. vijana wengine wawili Raul Asencio na Jacobo wapo tayari kutumikia klabu hiyo. Kilichobakia ni uamuzi wa kocha tu.
Kocha mpya
Ingawaje Carlo Ancelotti amelaumiwa kwa masuala kadhaa, lakini suala la usajili wa mabeki wa kati, kulia na kushoto lilikuwa wazi na hakupewa mahitaji yake. Lakini sasa Ancelotti hayupo kikosini, kaenda zake Brazil. Kocha mpya Xabi Alonso anatarajiwa kuimkarisha safu ya ulinzi akiwa na imani na wachezaji aliowahi kuwaandaa katika kikosi cha chini ya miaka 14, wakiwemo Raul Asencio na Jacobo pamoja na wengine.
Kocha huyu anachukua nafasi ya Ancelotti akiwa anapewa mahitaji yake kwa usajili wa nguvu na bila shaka hasira hizi za Perez zikikutana na umahiri wa kocha basi timu nyingi zitaambulia vipigo. Kazi kubwa ya kocha huyu ni kuhakikisha Real Madrid wana mabeki imara na wanacheza vyema, hivyo kuimarisha ukuta ni mpango unaoonekana dhahiri. Jaribio la kwanza ni katika mashindano ya Kombe la Dunia la klabu ambapo anatakiwa kuonesha cheche zake za ufundi ili kuandika historia yake akiwa kocha kama ilivyokuwa kwa mchezaji.
Ushambuliaji
Ni eneo ambalo linaonekana kumridhisha baada ya kufanya usajili wa Kylian Mbappe msimu uliopita na sasa huenda Real Madrid wasiingie gharama kubwa kusajili mshambuliaji mwingine huku tetesi zikibainisha kuwa Gonzalo aliyeko kwenye kikosi cha pili anatakiwa kucheza nafasi ya Joselu yaani mshambuliaji anayetakiwa kucheza kwenye boksi la adui akiwa na kazi moja tu kutupia magoli.
Mawinga
Tayari nafasi hizo zina wenyewe, Vinicius Junior na Rodrygo Goes na hata Kylian Mbappe anaweza kutumikia eneo hilo pamoja na Lucas Vazquez kama atabakia klabuni hapo. Kwa vile muda wa usajili bado upo, huenda Perez na viongozi wenzake wanaweza kuongeza wachezaji katika maeneo mengine ili kuponya hasira zao za kushindwa vibaya msimu uliopita.
Comments
Loading…