Mashindano ya COSAFA yanayoendelea nchini Afrika kusini yemeleta mjadala kuhusu uwezo wa wachezaji wa ndani ya Ligi Kuu Afrika kusini. Mjadala umetawala mitandaoni huku wengi wakimzungumzia Feisal Salum ambaye anahusishwa na kujiunga klabu ya Kaizer Chiefs. Habari kutoka Afrika kusini zimeeleza kuwa Kaizer Chiefs wanaofundishwa na Nasredine Nabi huenda wakamsajili nyota huyo wa Azam kwa ajili ya msimu ujao.
Kaizer Chiefs wanashikilia nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi hiyo, huku ikiwa kwenye mikakati ya kurudi kwenye ubora wake kama zamani. Safari ya Kaizer Chiefs kurudi kwenye ubora si rahisi lakini chini ya Nabi huenda wakafanikiwa kuwa wazuri zaidi. Mjadala huo umekolezwa pia juu ya wachezaji wa kigeni kutoka Ligi Kuu Tanzania ambao wanaweza kucheza katika timu mbalimbali. TANZANIASPORTS inawachambua wachezaji kadhaa ambao wanaweza kutumikia klabu za Afrika kusini.
Timu zenyewe zilivyo
Ligi kuu ya Afrika kusini ni maarufu kama Premier Soccer League (PSL) ina vigogo kama vile Mamelodi Sundowns, Orland Pirates, Kaizer Chiefs, Stellenbosch, Sekhukhune, TS Galax, Amazulu, Polokwane, Richards Bay, Kaizer Chiefs na Gallants ambazo zipo kwenye nafasi 10 katika msimamo wa Ligi hzina wachezaji ambao unaweza kusema wanatisha sana.
Baadhi ya wachezaji walionao hawawezi kupata namba katika kikosi cha Yanga, Simba au Azam. Bahati walinayo wachezaji hao ni kuwepo katika Ligi inayowachukua kama njia mbadala ya kuepuka kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa kutoka nje ya Afrika kusini. Licha ya ubora wa Ligi hii bado inao wachezaji wenye uwezo wa kawaida ambao si tishio kwa vilabu vya Ligi Kuu linapofika mashindano ya Kimataifa.
Yusuf Kagaoma-Mamelodi Sundowns

Hii ni timu inayosifika kuwa na bajeti kubwa na imesajili wachezaji wengi kutoka Amerika kusini kwa madai wana vipaji vikubwa. Allende ndiye mchezaji wao ghali ambayo alishindwa kufurukuta katika mechi mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa mbele ya Yanga. Udhaifu wa timu hii ni kwamba wanakosa mchezaji kariba ya Yusuf Kagoma.
Kwa maana Mamelodi Sundowns wanabiliwa na kibarua cha kukosa kiungo mkabaji. Yusuf Kagoma anao uwezo mkubwa wa kupenya katika kikosi hicho hasa nafasi ya kiungo mkabaji. Laiti Mokoena angepata kiungo wa ulinzi mzuri na ambaye anaweza kumrahisishia kazi yake basi Yusuf Kagoma ana kila sababu za kutua katika klabu hii. Licha ya Mameodi Sundowns kutazama wachezaji wa mataifa ya mbali na kupuuza wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania, bado ni timu ambayo inaweza kubebwa na staa huyu. Ni kupuuza huko ndiko kulikowagharimu kwa Fiston Mayele ambaye amewakosesha ubingwa Mamelodi wakati walikuwa wanamwona akicheza mechi mbili dhidi ya Marumo Gallants. Yusuf Kagoma ana sifa zote za kufanya kazi chafu katika kiungo cha Mamelodi Sundwons.
Ibrahim Bacca-Mamelodi Sundowns
Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Mamelodi Sundowns hawana kasi. Licha ya kuwa na kimo kizuri lakini wanakosa ile kasi ya mchezo na kuhimili vishindo vya wapinzani, ndiyo maana walipigwa kumbo na Pyramids katika dakika chache sana kwenye mchezo wa fainali.
Comments
Loading…