in

Liverpool, Leeds United, magoli saba!

BAADA ya miaka 16 hatimaye Leeds United wameanza kuweka mguu sawa Ligi Kuu England licha ya kunyukwa mabao 4-3 na mabingwa watetezi Liverpool kwenye mchezo wa kwanza wa msimu wa 2020/2021 uliochezwa kwenye dimba la Anfield jijini Liverpool.

Mabingwa hao wa EPL walionesha dalili za kuibuka na ushindi katika dakika 4 ya mchezo huo nyota Mohammed Salah kupachika bao la kuongoza kwa njia ya mkwaju wa penati. Katika dakika 20 beki kisiki wa timu hiyo Van Dijk alipachika bao la pili kwa kichwa, kabla ya dakika 33 Salah akipachikabao la tatu kwa shuti kali. Katika dakika ya 88 Salah alicheka na nyavu kwa mara nyingine  baada mkwaju mwingine wa penati kutinga nyavu za Leeds United.

Tanzania Sports
Pilika pilika

Liverpool walicheza mfumo wa 4-3-3 wakati wa kujilinda lakini walicheza 3-3-4 wakati wa kushambulia lango la Leeds United. Goli la kwanza la Liverpool lilitokana na makosa ya Koch kunawa mpira katika eneo la hatari.

Wageni wa EL, Leeds United walitumia mfumo wa 4-1-4-1 walipachika bao la kusawazisha katika dakika 12 ya mchezo huo kupitia nahodha wake Jack Harrison, kabla ya Patrick Bamford kupachika bao la pili kunako dakika 30 na Mateusz Klich kugongelea bao la tatu katika dakika 66.

Licha ya mchezo mzuri, Leeds United walikuwa dhaifu katika kiugo mkabaji. Leeds United walikuwa wazuri upande wa kushoto ambako Helder Costa alikuwa akicheza kama winga. Makosa madogo madogo na ugeni viliisumbua Leeds United na kushindwa kuibuka na pointi tatu muhimu.

Jambo lingine ni mawasiliano hafifu katika safu ya ulinzi iliyoongozwa na Koch huku beki wa kushoto wa Leeds United, Dallas akiwa na k9ibarua kigumu cha kumdhibiti Salah.

Kasi ya Helder Costa ilikuwa kumrudisha nyuma na kudhibiti mashambuli beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander Arnold ambaye hakuwa na makali kwenye mchezo huo

MABAO SABA

Mchezo huo ulikuwa wa funga ni nikufunge, ambapo ilishuhudiwa mabao 7 yakifungwa katika uwanja wa Anfield. Ni mmoja wa mchezo mkali zaidi mwanzoni mwa msimu huu. Hapakuwa na ulinzi madhubuti. Hapakuwa na hofu dhidi ya mpinzani.

Timu zote zilishambuliana kwa zamu. Hapakuwa na soka la kujihami, bali kila upande ulishambulia zaidi kuanzia dakika ya kwanza hadi filimbi ya mwisho ya mchezo huo. Mchezo hu ulikutanisha timu mbili zenye sifa tofauti.

Leeds United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu na Liverpool mabingwa wa Ligi hiyo. Hata hivyo kikosi cha Leeds United kinachofundishwa na Marcelo Bielsa kilicheza kandanda safi na kuwatuliza mabingwawa EPL, Liverpool hali ambayo ilimlazimu kocha wake Juregn Klopp kuingiza mlinzi Joel Matip wa kulinda ushindi wao baada ya kupata bao la nne.

TAKWIMU

Baada ya miaka 16 Leeds United walifunga mabao mawili ndani ya dakika 30 kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao kapteni Jack Harrison na mshambuliaji Patrick Bamford.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipomalizika Liverpool walipiga pasi 237, wakati Leeds United walipiga pasi 214. Leeds United walipiga pasi nne hadi kupachika bao la pili bila Liverpool kugusa. Bao la tatu la Leeds United lilifungwa na Mateusz Klich baada ya kupigiana pasi 6 bila Livepool kugusa.

Hadi katika dakika ya 68 kindi cha pili, Liverpool walimiliki mpira kwa asilimia 38 wakati Leeds walimiliki kwa asilimia 62. Hadi dakika ya 90 ya mchezo zilipokamilika Liverpool walipigiana pasi 404 wakati Leeds United walipigiana pasi 435.

VIKOSI NA ALAMA

LIVERPOOL (4-3-3): Alisson (5.5); Alexander-Arnold(5), Gomez (5.5), Virjil Van Dijk (6) Robertson (6.5); Nabil Keita (6) Fabinho (6), Henderson (6) Jones (5), Wijnaldum (6); Salah (8), Firmino (5), Mane (6). AKIBA: Adrian, Milner, Origi, Minamino, Fabinho,Jones.

LEEDS UNITED (4-1-4-1): Meslier 6; Ayling 7.5, Koch 5, Struijk 6, Dallas 6; Phillips 7.5; Costa 6.5, Klich 7.5 (Shackleton 81), Hernandez 7 (Roberts 62, 5.5), Harrison 7.5; Bamford 6.5 (Rodrigo 5). AKIBA; Poveda-Ocampo, Alioski, Casilla, Casey

HAT TRICK

Mohamed Salah amekuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kupachika mabao katika mchezo wa kwanza wa EPL msimu huu. Amekuwa mchezaji wa kwanza pia kupachika mabao matatu katika mchezo wa kwanza.

BIELSABALL

Mechi hiyo ilionesha Leeds United hawagopi lolote kutoka kwa Liverpool. Haikuwa Leeds United ile iliyowahi kuitwa inacheza mchezo mbaya zaidi uwanjani miaka ya nyuma, bali ilikuwa Leeds yenye kupiga pasi na udambwidambwi wa kutosha.

Ndiyo, Liverpool ni timu nzuri, lakini ukweli kuruhusu mabao matatu kutinga katika nyavu zao ni ishara kuwa kuna gwiji wa kandanda anaiongoza Leeds United. Leeds walitulia, walipfanya maamuzi sahihi, walipiga pasi zao vizuri licha ya upungufu mdogo mdogo kuhusu kuwafikia walengwa kwa baadhi ya nafasi.

Hii ndiyo Leeds United ambayo imepanda Ligi Kuu ikiwa inacheza kandanda la kuvutia. Mchezo wa pasi nyingi na kuufanya uvutie watazamaji. Ni Leeds ya aina yake. Leeds ya Bielsa kwa jina la utani El Loco, ambaye muda wote akiwa amevalia miwani na pajama lake alikuwa akichuchumaa kwenye ‘touchline’ akiwahamasisha wachezaji wake na kuusoma mchezo. Golikipa wa Leeds Illan Meslier alikuwa kivutio kingine, alicheza kwa kiwango kizuri licha ya ugeni wake katika Ligi hiyo.

MICHAEL OLIVER

Hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi Michael Oliver ilipopulizwa, Liverpool waliibuka na ushindi wa 4 dhidi ya 3 za Leeds United. Na pengine itakuwa mecchi ya kukumbukwa na mshambuliaji mpya wa Leeds United, Rodrigo Moreno ambaye alisababisha penati iliyowapa Liverpool bao la ushindi. Ni mwanzo wa msimu, Leeds United ikiendelea kucheza hivi itakuwa timu yenye kuogopwa zaidi. timu inayotandaza kandanda la aina yake.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Jezi za YANGA zitauza AFRICA

Simba vs Mtibwa

Simba ina wachezaji bora na siyo timu bora