in

Simba ina wachezaji bora na siyo timu bora

Wakati naitazama Simba kwenye mechi dhidi ya Namungo FC, mechi ya ngao ya jamii mechi dhidi ya Ihefu FC mechi yao ya kwanza ya ligi kuu na mechi ya jana dhidi ya Mtibwa Sugar kitu pekee ambacho kilikuwa kinakuja akilini mwangu ni PSG.

Nilikuwa nawaona PSG kwenye timu ya Simba. Kwanini nilikuwa nawaona PSG?  Nilimtazama Aishi Manula golini kwake nikarudi kwenye benchi nikamkuta Beno Kakolanya.

Kila nafasi ndani ya uwanja nilipokuwa naiangalia ndani ya uwanja niliona mchezaji bora.  Na kila niliporudi kwenye benchi pia niliona mchezaji bora akiwa amekalia mbao.

Kikosi cha Simba Sports Club
Kikosi cha Simba Sports Club

Picha hii ipo kwenye timu ya PSG. PSG imejaza wachezaji bora kwenye kila eneo. Wachezaji ambao wanaweza kukupa imani kubwa ya kuondoka na ushindi.

Wakati naendelea kuwatazama Simba kichwani kwangu ilikuja mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu wa mwaka 2019/2020.

Fainali ambayo iliwakutanisha Bayern Munich pamoja na PSG. Kwa lugha nyepesi fainali hii iliwakutanisha timu bora (Bayern Munich ) na timu yenye wachezaji bora (PSG).

Timu ya Bayern Munich ilikuwa na wachezaji ambao walikuwa wameunganika kwa pamoja kuonesha kiwango cha timu kwa pamoja.

PSG ilikuwa na wachezaji bora ambao walikuwa hawajaunganika vyema kama ambavyo Bayern Munich walivyokuwa wameunganika.

Simba iko kwenye eneo la PSG. Ina wachezaji bora sana. Wachezaji ambao hawajaunganika kutengeneza timu bora ya Simba.

Kuna wachezaji wengi wenye uwezo binafsi . Lakini wachezaji hawa hawajatafutiwa mfumo sahihi wa kuwaunganisha ili kupata timu bora ya Simba.

Leo hii kwenye benchi unaweza ukampata Ibrahim Ajib , Francis Kahata , Meddie Kagere , Lary Bwalya , Beno Kakolanya , Chris Magalu.

Uwanjani napo unaweza ukakutana na Luis Miquissone , Bernard Morrison,  John Bocco , Chota Chama , Jonas Mkude,  Mzamiru Yassin.

Lakini wachezaji hawa wanakosa muunganiko mzuri kwenye mechi zao. Pamoja na kushinda mechi kadhaa ila ushindi wao ni ushindi ambao wanahangaika kuupata.

Kwa kikosi cha Simba kupata ushindi kwa kuhangaika dhidi ya timu ambazo ni za kawaida siyo jambo la kawaida. Kuepeushana na haya yote Simba inatakiwa kutengeneza mfumo mzuri ambao utakuwa na faida kubwa kwa wachezaji hawa bora kuunda kikosi bora.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Ni kweli kabisa simba sc sio timu ya kupata matokeo haya kwa timu kama ihefu au mtibwa. Timu imekua haieleweki kabisa.sasa najiuliza kama tunapata matokeo ya kubahatisha kwa timu kama ihefu au mtibwa je itakuaje tukikutana na ma giant wa kandanda afrika. Sijui kinachosababisha haya ila naona haeri ya msimu ulopita tukiendelea katika hari hii timu mapema sana itaondolewa katika mashindano ya kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Liverpool, Leeds United, magoli saba!

Arsenal Chelsea

EPL imerejea