in

Kiu Ya Kiduka Ni Mwakinyo

ngumi

Bondia namba mbili kwa ubora Tanzania Twaha Kiduku amesisitiza kuhitaji pambano na Hassan Mwakinyo ili afahamike nani bingwa wa nchi.

Kauli hii aliitoa wiki mbili zilizopita ameirudia tena siku ya jumatano alipokuwa anafanya mahojiano na moja ya kituo cha Radio hapa nchini.

Kiduku ametoka kumchapa kwa pointi  Abadallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ katika pambano la raundi kumi.

Baada ya ushindi huo amepaa hadi nafasi ya pili na anahitaji kutawazwa kuwa namba moja endapo atacheza na Mwakinyo na akishinda.

Kiduku ambaye ameweka wazi kuwa hana uongozi unaomsimamia  anawakaribisha watu wanaopenda kumsapoti katika kazi zake.

“Sina meneja wa wakala kwa sasa hvyo kama mtu akihitaji kunipa sapoti namkaribisha,” alisema.

Bondia huyo kutoka Morogoro aliye na miaka 28 moja ya hazina mahususi katika ngumi za Tanzania.

Ni bondia ambaye anathamini utu pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika kazi yake.

Huenda imani yake ya kumuogopa Mungu ndio inayompa hofu ya kuto mdharau mtu yoyote.

Huenda kila mmoja anamtazamo wake kwa  Kiduku kwa jicho lake na vile anavyoona ila kwa anayetaka kuwekeza hiki ndicho kipindi sahihi kwake.

Makampuni mbalimbali pamoja na bidhaa za vinywaji hasa zile za ‘Energy’ hamuoni kitu kwa Kiduku.

Ni bondia ambaye anamuonekano wa kimatangazo kama watu wakiamua  kumpa mashavu hayo.

Pia wakala hii ndio sehemu ambayo mnaweza kupiga pesa kipindi ambacho yuko na uwezo wa  hali ya juu.

Mtafutie mapambano makubwa atengeneze hela ndefu na nyie mnakuwa na kiasi chenu.

Uwezo aliouonesha na heshima aliyoiweka kama kweli mtu anahitaji kuwekeza Kiduku ni sehemu sahihi kwa upande wa ngumi za kulipwa.

Kugoma kwa Mwakinyo kucheza naye ni lengo la kibiashara  baina yao wawili na wanatakiwa watengeneze hela kweli.

Nimeshangaa kusikia kuwa hela nyingi mtu anaweza kupokea kwa pambano lenye hadhi kama la Mbabe na Kiduku shilingi milioni sita.

Maneno hayo aliyatoa Mwakinyo alipokuwa anamjibu Kiduku juu ya kupigana naye.

Na Kiduku katika mahojiano alisema kuwa kuna pambano moja dhidi ya Mada Maugo alipata hela kuliko hili la Dulla Mbabe aliloshinda hii ina maana alipata chini ya milioni nne.

Kwakuwa yeye ndio kalitaka pambano wakala wanatumia mwanya huo kuwanyonya mabondia.

Hii ni sehemu nyingine ambayo inatakiwa iangaliwe kwa mapana yake, ngumi za Tanzania zina mambo mengi sana ni vizuri kuangalia namna ya kuwasaidia ndugu zetu ili wafike mbali.

Ushabiki upo tangu zamani mfano mimi niliwahi kuwa shabiki wa Mike Tyson mwingine alimshabikia Lenox Lewis lakini haibadilishi kuwa unapotaka kuusogeza mbele mchezo umbane mmoja mwingine apande.

Hivyo ukiniamsha usingizini ukiniuliza mabondia saba bora Tanzania kwa sasa basi sitosita kuwataja , Twaha Kiduku, Hassan Mwakinyo, Dulla Mbabe, Mfaume Mfaume, Tony Rashid, Ibrahim Classic  na Cosmas Cheka.

Sasa hawa watu tuwafanye bidhaa zitakazo leta heshima ya ndondi Tanzania.

Tuwainue kwa pamoja na kila aliyebora kwa kiwango chake basi anyanyuliwe kwa kiwango chake.

Kwa upande wangu naamini kabisa Twaha Kiduku, Dulla Mbabe na Hassan Mwakinyo wakipata watu sahihi watafika mbali sana.

Nakumbuka katika pambano la utangulizi baina ya Twaha kiduku na Msauzi Afrika France Ramabolu alimtandika kwa ‘TKO’ uwezo wake aliounesha pale ndio ikawa mwanzo wa kumtaka Dulla Mbabe.

Lakini uwezo wake haujifichi kabisa hivyo ni wakati wa kumbeba na kuhakikishia mtu ambaye unataka kuwekeza kwake ni kijana msikivu  aliye na nidhamu ya hali ya juu sana.

Naamini kabisa mtu akijtokeza kumdhamini au kuwa kama Wakala wake, Twaha atalipaisha taifa mbele.

Rekodi zake katika mitandao zina utata lakini mtua anaweza kunirekebishaa amepigana mapambano 21 ameshinda 15 amepigwa 5 na sare moja jina lake kamili alilopewa na wazazi wake ni  Twaha Kassimu Rubaha, amezaliwa mkoani Morogoro ila baba yake Mzaramo.

Amezaliwa 05.01. 1992, Kiduku mmoja ya mabondia wachache Tanzania walio na miili yenye muonekano wa kibondia.

Uwezo wake wakuongea kwa busara pamoja na  kuishi vizuri na watu wanaomzunguka ndio sababu ya kupendwa na kila rika.

Anatamani naye siku moja awe bondia mkubwa na atakaye tambulika duniani naamini atafika huko kwa uwezo wa Mungu aliyeumba mbingu na ardhi.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

73 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
VPL mechi za ufunguzi

VPL: Rekodi ya Sabiyanka haijavunjwa

simba yanga

Yanga itatoa ushindani kwa Simba