in

AUBAMEYANG alivyokataa kuwa VAN PERSIE

Aubameyang

Moja ya kitu ambacho Arsenal kimewagharimu kwa kiasi kikubwa na kwa muda mrefu ni wao kuondokewa na wachezaji wao nyota kwenye kikosi chao.

Kuna nyakati ambazo Arsenal ilimwihitaji Thierry Henry ili kuendeleza walipofikia kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka 2006 lakini ghafla Thierry Henry aliondoka.

Barcelona ndiyo sehemu ambayo Thierry Henry alitumia baada ya kutoka Arsenal. Aliondoka Arsenal kipindi ambacho timu ilikuwa inamwihitaji sana.

Kwanza alikuwa nahodha wa timu ya Arsenal. Busara zake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zilikuwa zinahitajika sana kwa kipindi hiki.

Aliondoka Arsenal akiwa ndiye mshambuliaji pekee mkubwa na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na kuibeba timu nyakati zote ngumu ndani ya Arsenal.

Aliondoka Arsenal akiwa ndiye mchezaji mwenye ushawishi mkubwa. Lakini aliwaacha Arsenal bila cha kufanya , bila kupata mtu sahihi ambaye angeziba pengo lake.

Tanzania Sports
Gabriel Magalhaes

Arsenal walianza upya kutengeneza mshambuliaji mwingine.  Wakati wakiwa katikati ya kutengeneza mtu mwingine mpya ambaye atasimama kama mshambuliaji kuna baadhi ya wachezaji walianza kuondoka.

Taarifa zilianza za Cesc Fabregas. Nahodha wa Arsenal. Akawa nahodha watatu mfululizo kukiacha kikosi cha Arsenal.

Alianza Patrick Viera , akaja Thierry Henry ikawa zamu ya Cesc Fabregas kiungo bora kabisa kuwahi kutokea kwenye kikosi cha Arsenal.

Alex Song naye aliondoka akaenda Barcelona. Safu ya kiungo cha Arsenal ikawa inazidi kubomolewa kwa kuondokewa na wachezaji muhimu ndani ya kikosi chao.

Safu hii ya kiungo ilishuhudia ikibomolewa baada ya Alexander Hleb kiungo ambaye alianza kuwa tegemeo ndani ya Arsenal naye kuondoka na kutimkia Barcelona.

Kiungo wa Ufaransa Samir Nasri aliondoka kwenye kikosi hicho cha London ya Kaskazini na kutimkia katika kikosi cha Manchester City.

Arsenal ilizidi kubomolewa mpaka kwenye safu ya ulinzi ambapo tulishuhudia baadhi ya wachezaji katika safu ya ulinzi wakiondoka katika kikosi hicho cha Arsenal.

Nahodha wa Arsenal kipindi kile Thomas Vermaelen aliondoka katika kikosi cha Arsenal na kwenda Barcelona hivo kufanya kuwa ni nahodha wa nne kuaicha Arsenal.

Mabeki wa pembeni wa Arsenal , Bakery Sagna na Gael Clichy waliondoka na kwenda katika timu ya Manchester City.

Kabla ya kupona vidonda vya kuondokewa na wachezaji nyota ndani ya kikosi cha Arsenal, Arsenal walipata pigo jingine jipya ambalo walipigwa na Sir.Alex Ferguson.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha Manchester United alifanikiwa kumsajili nahodha wa kipindi hicho wa Arsenal Robbin Van Persie.

Arsenal ikabaki mkiwa. Kila ilipokuwa inajaribu kujenga timu ilikuwa inaondokewa na wachezaji nyota wa timu hiyo na kuwafanya kila siku kuanza upya.

Kwa muda mrefu Arsenal imekuwa ikianza upya kila walipokuwa wanaondokewa na wachezaji wao nyota hivo kuwafanya wasiwe timu ya kushindania makombe.

Leo hii Arsenal iko chini ya Mikel Arteta ambaye anajaribu kuijenga Arsenal mpya. Kwenye kikosi hiki anachokijenga yupo Pierre Emick Aubameyang.

Mshambuliaji ambaye ni nyota kwa sasa ndani ya kikosi cha Arsenal. Hofu kubwa ilikuwa ni kumpoteza tena mchezaji huyu ambaye alikuwa anawindwa na Barcelona.

Lakini imekuwa tofauti. Mikel Arteta amefanikiwa kumbakiza Pierre Emerick Aubameyang. Amekataa kuwa kama kina Robbin Van Persie , Patrick Vieira , Thomas Vermaelen , Cesc Fabregas na Thierry Henry.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
TFF

Bodi Ya Ligi Na TFF Lawama Nyingi!

Dar young africans

Huyu ndiye nahodha anayewafaa Yanga..