Klabu ya Aston Villa ya nchini England imefanya makubwa msimu huu kwani imefuzu kushiriki mashindano ya klabu bingwa ya soka barani Ulaya. Mafanikio hayo ymefanya baadhi ya mashabiki wa soka wakiwa mdomo wazi kwani wakati msimu unaanza hawakutarajiwa kuwa na mafanikio hayo. Wengi walidhani klabu hiyo itashika nafasi za kawaida tu. Wengi walidhani nafasi ya kufuzu klabu bingwa ingeenda kwenye vilabu vilivyozoeleka kama vile Chelsea FC Tottenham Hotspur, Manchester united na vinginevyo. Kwa nchini Tanzania klabu hiyo ilianza kupata wafuatiliaji katika mitandao ya kijamii pale ilipomsajili mshambuliaji wa kimataifa ambaye ndiye mshambuliaji tegemeo bwana Mbwana Samatta. Kurasa zake za kijamii zilikuwa zinajaa mashabiki wa soka wa Tanzania ambao walikuwa wanajaza maoni yao kwenye kurasa hizo kwa wingi sana na tena wakiwa wanatumia lugha ya Kiswahili.
Nchi ya Hispania ni mojawapo ya mataifa ambayo yanasifika sana kwenye mchezo wa soka. Vilabu vya Barcelona na Real Madrid ni vilabu maarufu sana ulimwenguni. Katika miaka ya hivi karibuni taifa hilo limeanza kutanua wigo wake wa umaarufu katika mchezo wa soka kupitia kwa makocha. Kocha maarufu Zaidi kutoka taia la uhispania kwa sasa ni kocha wa klabu ya Manchester City ya England bwana Pep Guardiola. Ameshinda mataji yote ambayo yanashindaniwa nchini England kwa ngazi ya klabu na hadi klabu bingwa ulaya. Lakini kama waswahili wanavyosema katika msafara wa mamba lazima mijusi nao wawepo basi katika taia hilo kuna kocha mwingine anayevuma kwa mafanikio ambaye naye ni Unai Emery ambaye kwa sasa ndiye kocha mkuu wa klabu ya Aston Villa.
Kocha huyu alizaliwa mnamo novemba mwaka 1971. Alizaliwa huko nyumbani kwao nchini Uhispania. nyota ya kocha huyu ilianza kuonekana nchini hispani pale alipokuwa anafundisha klabu ya daraja ya kwanza ya nchi huyo na kuisaidia kuingia ligi kuu. klabu hiyo ilikuwa ni Almeria. baada ya hapo alienda klabu ya Sevilla ambapo aliisaidia kocha huyu ana rekodi kubwa sana katika soka la barani ulaya katika ngazi ya vilabu. ana rekodi ya kubeba kombe la UEFA mara tatu mfululizo na hakuna kocha mwingine barani ulaya ambaye amewahi kufanya hivyo. alifanya hivyo wakati anafundisha klabu ya Sevilla ya uhispania ambapo alipata mafanikio hayo katika miaka ya 2014, 2015 na 2016. mafanikio hayo yalimfanya apachikwe jina la utani na mashabiki wa soka ulaya ambalo lilinasabishwa na mafanikio hayo ambalo ni UEL(Unai Emery League). Baada ya hapo alienda klabu ya matajiri wa Ufaransa klabu ya PSG ambapo alifanikiwa kombe la ligi kuu ya soka ya nchini humo na pia kushinda kombe la Coupe de france.
Katika klabu ya PSG hakukaa sana kwani aliondoka katika klabu hiyo na akaenda zake katika klabu ya wababe wa jiji la London yaani klabu ya Arsenal. katika klabu ya Arsenal alisaidia klabu hiyo kufika fainali ya kombe la Europa na hivyo kumfanya aonekane kama ni mbabe wa kombe hilo licha ya kwamba hakushinda fainali hiyo. mwaka uliofuata aliondoka klabu ya Arsenal na kwenda zake nchini Uhispania ambapo alijiunga na klabu ya Villareal ambapo katika klabu hiyo aliisaidia kubeba taji la ligi ya Europa. msimu uliofuata alijiunga na klabu ya England ya Aston Villa ambapo amefanikiwa kuifanya klabu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la UEFA conference league. katika soka la Aston Villa atakumbukwa zaidi kwani amesaidia klabu hiyo kufuzu kushiriki klabu bingwa ulaya.
nimemtolea mfano huyu kama aina ya kocha ambaye tunahitajika kuona katika ligi yetu kwani ni kocha ambaye amekuwa anavichukua vilabu vya kawaida na kuvisaidia kubeba mataji makubwa. pili katika safari hiyo ya kubeba mataji makubwa amekuwa hatumii sana bajeti kubwa katika kutafuta hayo mafanikio.
Comments
Loading…