in , , ,

LIGI YA MABINGWA ULAYA


Chelsea wacheka, Arsenal wakwama
Bado wakabana kwenye makundi yao

 
Wakati Chelsea wamepata ushindi mnono kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal wamepoteza mechi katika dakika za mwisho.

Fernando Torres alifunga bao lake la 100 baada ya kupachika mawili kati ya matatu kwa nunge dhidi ya Schalke usiku wa Jumanne hii.

Ushindi huo umewapandisha Chelsea hadi nafasi ya kwanza kwenye kundi lao wakiwa na pointi sita sawa Schalke wakitofautiana tu kwa uwiano wa mabao.

Katika kundi hilo Steua Bucharest walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Basel ambao kwenye mechi ya kwanza waliwafunga Chelsea.

Basel sasa wana pointi tatu huku Steua wakiwa na pointi yao moja kutokana na sare ya usiku wa Jumanne hii.

Torres ameendelea kuonesha umuhimu wake kikosini Stamford Bridge, na labda ndiyo sababu Roman Abramovich hakubali kumuuza. Bao jingine lilifungwa na Mbelgiji Eden Hazard ambaye anaendelea kuwa fiti katika mfululizo wa mechi nyingi.

Arsenal walionesha soka nzuri, wakitandaza pasi za uhakika na hata kuwazidi wenzao – Borussia Dortmund katika dimba la nyumbani Emirates nyakati fulani lakini waliishia kufungwa 2-1.

Arsenal walitangulia kuwa nyuma kwa bao moja, baada ya kiungo Aaron Ramsey kujaribu kupiga chenga akiwa katika eneo la hatari dakika ya 16, akapokonywa mpira na Henrikh Mkhitaryan hakufanya ajizi bali kukandamiza shuti kali hadi nyavuni.

Arsenal walisawazisha muda mfupi kabla ya mapumziko kupitia kwa Olivier Giroud kwa bao zuri alipowashinda walinzi na kipa na hata kujizuia asianguke na kucheka na nyavu baada ya majalo ya beki wa kulia, Bacary Sagna.

Arsenal walijaribu kutawala mpira kipindi cha pili, wakiwapelekesha wageni wao na hata kukaribia kufunga mabao mawili au matatu, lakini waliumizwa na uharaka wa wapinzani wao kurudisha mpira haraka, ambapo Robert Lewandowski alifunga dakika ya 82 baada ya kutiliwa majalo na Kevin Grosskreutz.

Lewandowski alikuwa na bahati ya kutopewa kadi nyekundu kwa kosa la pili akiwa na kadi ya njano, ambapo alimsukuma kwa kiwiko beki wa kati wa Arsenal, Laurent Koscielny mapema kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo, Arsenal na Dortmund wanafungana kwa pointi huku wakifuatiwa na Napoli ya Italia ambao walifanikiwa kuwafunga  Marseille 2-1, na Wafaransa hao wanashika nafasi ya nne na ya mwisho.

Katika matukio mengine, Celtic ya Uskochi waliwafunga Ajax 2-1, FC Porto wakalala 1-0 kwa Zenit St Petersburg, FK Austria wakakung’utwa 3-0 na Atletico Madrid huku Mila wakitoka sare ya 1-1 na Barcelona.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Machava FC, yaanza kujitetea Ligi Daraja La Tatu, Kilimanjaro

Man U ushindi kidogo, muhimu!