in , ,

Machava FC, yaanza kujitetea Ligi Daraja La Tatu, Kilimanjaro

 
BINGWA mtetezi wa Ligi daraja la tatu, mkoa wa Kilimanjaro, Machava FC wikendi iliyopita walianza vyema kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa kuifumua Panone 32-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika uwanja wa Magereza ya wilaya ya Moshi, mkoani Hapa.
 
Machava “mnyama mkali” ambao wana kumbukumbu mbaya ya kupoteza nafasi ya kutinga ligi daraja la kwanza hivi karibuni, kupoteza ubingwa wa Mkombozi pamoja na kombe la Jafary, walikuwa wa kwaza kupata goli katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza, likifungwa na Issa Kipese.
 
Wakicheza kwa kujiamini, Machava ambayo hivi karibuni ilikutana na “Majanga” ya kukimbiwa na wachezaji wake wengi mara tu baada ya kukosa nafasi ya kushiriki ligi daraja la kwanza mikononi mwa Stendi United katika michezo ya Klabu bingwa mikoa, iliongeza goli la pili likifungwa na Issa Kipese katika dakika ya 42.
 
Kipindi cha pili Panone ilicharuka katika jitihada za kusawazisha magoli hayo, wakicheza kwa kujihami zaidi wasiweze kuruhusu goli lingine na kuzima ndoto zao za kuondoka na ushindi.
 
Zikiwa zimesalia dakika 4 tu mchezo huo uliochezwa Jumamosi ya Oktoba 19 umalizike, Panone walifanikiwa kupata bao la kufuta machozi, goli lililotiwa wavuni na Mshambuliaji Benny Rafael ambaye katika Msimu uliomalizika alikuwa ni mchezaji wa Machava, kwa shuti kali dakika ya 86.
 
Katika michezo mingine iliopigwa Jumamosi hiyo, Soweto ikicheza katika uwanja wa Mandela ilitoa kipigo cha 1-0 dhidi ya KIA, Polisi Kilimanjaro ikiichabanga Forest ya Siha 2-1 katika uwanja wa Sanya Juu.
 
Ligi hiyo iliendelea tena siku ya Jumapili kwa michezo miwili ambapo katika mchezo wa kwanza Kilototoni ya Moshi Manispaa iliuduwaza Kitayosce katika uwanja wa Magereza kwa kuitandika 3-2 huku Agip Kahe katika uwanja wa David Msuya ikitoa dozi ya 4-0.
 
Ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya vilabu 17 inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi katika viwana mbalimbali wikendi ijayo ikiwa ni hatua ya mtoano kabla ya hatua ya kumi bora.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Rio Ferdinand aitwa Kamisheni ya FA

LIGI YA MABINGWA ULAYA