in ,

Kuna aliyedhani VAR ingemaliza manung’uniko?

cost Arsenal two points

TUANZE na jambo chanya kuhusiana na VAR. alama za juu ziende kwa Howard Webb kwa kukiri kwamba VAR ilifanya makosa kwa Arsenal na kwenye dimba la Selhurst Park ambako Brighton nao walikuwa waathirika wa makosa ya VAR. 

Si rahisi kukubali maamuzi wakati timu yako imefanyiwa makosa. Hata hivyo, inakuwa ngumu zaidi pale maofisa wanapounda fenge na kukataa kukubali makosa yao.

Hii ndiyo dunia tunamoishi chini ya Mike Riley.  Alikuwa mwamuzi dhaifu asiye na uwezo kabla ya kuteuliwa kuwa mwakilishi mkuu katika PGMOL. Kama mwanafunzi aliyepata kukandamizwa shuleni kabla ya kusonga na kuja kuwa na mamlaka, Riley akaja kutumia nafasi yake kulipa kisasi akiwa PGMOL. 

Ilikuwa njia yake, au njia yake kuu – akitaka kuwa na usemi wa mwisho katika kila kitu. Hata pale Sheffield United walipofunga bao zuri na la kamilifu pale Villa – tuliloona sote kwamba lilizama ndani – Riley alikuja na Riley alikuja na upuuzi akidai eti VAR haingeweza kuingilia kati na kutoa bao kwa wafungaji.

Bournemouth walishushwa daraja  kama matokeo yake – na sio Villa, waliotakiwa washushwe. Imazidi sasa kwa makosa ya VAR yenye ‘athari kubwa’ tofauti na tulivyoahidiwa.

Lee Mason alikuwa kwenye VAR akitazama mechi ya Arsenal v Brentford. Alikosea. Bao la kusawazisha la Toney halikuwa halali na halikutakiwa kubakishwa – ikiwa unaamini katika kutafuta njia za kuzuia bao.

Tanzania Sports
Terrible day for the refs and the VAR.

Sifanyi. Sijui kwa nini tunaangalia kwa karibu sana hata zile offside za pembezoni kabisa. Kwa chochote kilichotokea kiasi cha kumpa mshambuliaji faida ya shaka wakati ilikuwa ‘tight’ vile?

Hata hivyo – ikiwa unaamini kufanya mambo yawe magumu zaidi kwa yaliyo magumu kabisa uwanjani – funga – basi bapo halitakiwi kuzuiwa.

Mwenzangu Keith Hackett, alipata kuwa mkuu wa waamuzi, ametaka Mason afukuzwe, katika makala yake aliyoandika kwenye gazeti la The Telegraph. Sikubaliani. Kwa hakika nahisi huruma kwa jamaa hawa wa VAR. nimekuwa na huruma hiyo siku zote.

Nimesema haya mara nyingi – kutazama soka kwenye TV ni aina ya sanaa. Inachukua miaka kuelewa kipi unaangalia au kutafuta na kwa nini. Ni upuuzi kuamini kwamba unaweza kuwa mwamuzi siku moja na kukaa kwenye ‘handaki’ pale na kutazama TV hapo kando. Ni tofauti. Tofauti sana. Najua Mason ni VAR kamili sasa. Ndivyo ilivyo kwa Mike Dean na huo ni mwelekeo sahihi. Waendesha VAR wnatakiwa kuwa wa muda wote. Na nilisema haya tangu awali, lakini bado inachukua muda mrefu kuzoea ipasavyo namna ya kutazama soka kwenye tv.

Ikiwa Mason angefukuzwa, kipi kingefuata? Hakuna hata mmoja angejihisi vizuri kuwa hapo kwenye tv kwa ajili ya VAR. wote wangekuwa pembezoni, wakiogopa kuhusishwa na dude hilo. Kuna hoja kwamba haingekuwa kitu kibaya, lakini hatungeweza kuendesha mambo namna hiyo.

Sipendi VAR. sijawahi kuwa nayo na sitakaa niwe nayo. Imeharibu mchezo wetu, lakini haiondoki. Kwa hiyo tunatakiwa kufanya kazi vyema kabisa kuitumia na Howard Webb anahitaji muda ili kufanya hivyo. Amekiri makosa kwa wikiendi hii na namwamini ataifanya kuwa vizuri.

Hii tu ndiyo ina uhakika – wale walioahidi kwamba VAR itamaliza mijadala juu ya mambo yanayoendelea uwanjani walikuwa ama wajinga au wasio waaminifu, au vyote. 

Hivi kuna yeyote aliyesikia yowe la upinzani kutoka Arsenal pale Saka alipoonekana kwamba huenda angekuwa ameotea wakati akitengeneza mpira uliosababisha bao la kwanza la Martinelli dhidi ya Liverpool? Hapana. Wala mimi.  Kumbuka – VAR ilituambia haikuonyeshwa hivyokwa bendera na kamera hazikuwa zimewekwa sawa sawa, hivyo uamuzi wa mwamuzi wa uwanjani wa kuruhusu bao lile ulisimama vile vile kwa sababu hawangeweza kuthibitisha kwamba Saka alikuwa kaotea. Ningeweza. Naam, ningeweza kuona. Ah, Riley alikuwa mfawishi wakati huo.

Ipo mifano mingi ya jinsi VAR ilivyokosea kuthibitisha. 

Nani alimshauri Guardiola kutoka nje akiwa katika hali ya kubembea bembea baada ya mkutano na wanahabari wiki jana? Alifanya makosa juu ya safu ya ulinzi ya City. Huku kukiwa na mashitaka 115 kutoka PL kuhusiana na mwenendo wa City – kitu cha kwanza alichosema alikosea – City hawakukutwa kwamba ‘hawakuwa na hatia’ walipokata rufaa dhidi ya mashitaka ya UEFA kwenye Mahakama ya Usuluhisi wa Michezo.

Ndio – marufuku ya miaka miwili CN iliondolewa, lakini ni kwa sababu muda wa sheria husika ya ukomo wa miaka miwili ilishapita na UEFA wakazuiwa haki ya kuanzisha mashitaka kwa mara nyingine. 

Lakini bado City walipigwa faini. Hupigwi faini ikiwa huna hatia. PL hawana vizuizi vya jinsi hiyo wala kuwa na wasiwasi. Mashitaka yao yatatakiwa kujibiwa – kikamilifu. Kwa hiyo Guardiola alikosea juu ya hilo kabla ya kuelekeza lawama kwa timu tisa za PL na kumtaja Daniel Levy kuhusika na kufuatilia mashitaka hayo. Kama ingekuwa Levy ningemtaka Guardiola kuthibitisha hilo mahakamani

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Fei Toto

MAHAKAMANI KUSIKILIZA KESI YA FEI TOTO WA YANGA

Tanzania Sports

Madhila ya Chelsea, Spurs yafute ukocha wa muda