in , , ,

Klabu EPL zajipanga

Klabu EPL zajipanga

Msimu wa soka wa Ligi Kuu ya England (EPL) ulitakiwa uwe unafikia mwisho kwa kawaida ya ratiba yake.

Ni wakati ambao washabiki huwa wanamalizia muda wa starehe hiyo kwa ligi maarufu zaidi duniani, huku wakijiandaa kuingia mfukoni kwa ajili ya msimu unaokuja, ambao kwa kawaida ni Agosti.

Lakini msimu huu umekuwa tofauti kwa sababu ya maambukizi makubwa ya virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, Covid-19 na kulazimisha ligi kusitishwa katika nchi nyingi, ikiwamo hapa England.

Wapo washabiki ambao ni kindakindaki kwa timu zao na hununua tiketi za msimu mzima, hasa kwa mechi za nyumbani za timu zao, na kwa msimu huu wameingia katika sintofahamu kwa sababu jumla ya mechi 92 hadi sasa zimesitishwa na haijulikani zitamalizika vipi, kwani watu bado wamejifungia ndani kwa amri.

Hali ya maambukizi imekuwa ya kutisha hasa kutokana na kasi yake, lakini pia watu kufariki dunia kwa maelfu ndani ya muda mfupi, na kuzua kizaazaa kwa wengi kiasi cha kukubaliana na amri ya Serikali ya kutulia ndani kujikinga.

Baadhi ya washabiki itabidi wasubiri kwa muda zaidi wakati klabu zao za EPL zikijipanga jinsi ya kurekebisha mfumo wa tiketi kwa tarehe za mwisho zitakazowekwa na kufungua dirisha la msimu wa 2020/2021 kwa ajili ya tiketi za msimu.

 Steve Bruce
Steve Bruce

Ligi haitarudia hadi ihakikishwe kwamba ni salama kiafya na Idara ya Huduma za Afya (NHS) ithibitishe hivyo, serikali iridhie na kuondoa marufuku ya mikusanyiko ambayo watu kadhaa maarufu, akiwamo Jose Mourinho na wachezaji wake walipata kuivunja na kukutana na hasira ya wadau.

Je, klabu zinashughulikiaje suala hili la tiketi? Mabingwa ‘wateule’ Liverpool wenye alama 25 zaidi ya wanaowafuata kwenye msimamo wa ligi, wakitakiwa kushinda mechi mbili tu kujihakikishia kombe baada ya miaka 30, waliahirisha uhuishaji wa mfumo wa tiketi kwa msimu ujao.

Klabu tayari imesema kwamba mechi zao za msimu wa 2019/2020 zilizobaki haziwezi kuchezwa mbele ya washabiki, na kwamba fidia kwa wale waliokuwa wameshanunua tiketi kwa ajili ya mechi hizo watafidiwa, ikidhaniwa zitaingizwa kwenye mechi za msimu ujao.

Manchester United nao wamefuta mauzo ya tiketi za msimu, wakijipanga kwa ajili ya kuanza tena baada ya kujulikana lini msimu utarejea. Makataa ya awali ilikuwa Mei msosi mwaka huu lakini sasa imesongezwa mbele kwa muda usiojulikana.

“Hii itaendelea kupitiwa muda hata muda na tarehe ya mwisho itaelezwa bayana baada ya kuwa imethibitika ni lini msimu wa 2020/2021 utaanza,” klabu ikasema katika taarifa yake.

Ikiwa mechi za msimu huu zilizobakia za uwanja wa nyumbani – Old Trafford ziutachezwa bila watazamaji, washabiki waliokuwa wamenunua tiketi za msimu wataingiziwa fedha zao kwenye tiketi za msimu ujao au kutumiwa fedha taslimu kwa thamani husika ya mechi zilizobaki za msimu huu.

Newcastle wao wametupia chagizo kali kutoka kwa washabiki wao, kutokana na kitendo chao cha kusonga mbele na kuwatoza tiketi za msimu ujao wakati kuna viporo vya msimu huu na hata haijulikani mechi zitamalizika vipi.

Baadhi ya washabiki wandaiwa kutozwa hadi pauni 650 Jumatano iliyopita, washabiki wakaja juu na kusema kwamba iliwasumbua. Tottenham Hotspur wamesogeza mbele muda wa kuuza tiketi za msimu ujao. Ilikuwa waanze kuuza mwezi uliopita. Wamewaambia washabiki wao wakae kwa kutulia. Arsenal walishatangaza kwamba washabiki watafidiwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Corona na madhila ya kujifungia ndani Uingereza

Tanzania Sports

Ozil agoma kukatwa mshahara