in , , ,

Kila nabii na zama zake

IMEBAKI miezi miwili Ligi Kuu England ifike tamati, huku Liverpool ikionesha dalili zote za kunyakua taji hili. Hali kadhalika bingwa mtetezi Man City ameonesha kutokuwa tayari kutetea taji lake. Wakati Man City akifikiria namna ya kumaliza Ligi kwenye nafasi nne za juu anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa Aston Villa na Manchester United. Aston Villa ametinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wakitwaa taji watashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya bila kujali watamaliza nafasi ya ngapi. Hali kadhalika Man United wakitwaa taji la Europa League watakuwa na nafasi ya kuchagua kucheza Ligi ya Mabingwa au la.

Hivyo basi msimu huu unaelekea ukingoni huku vilabu vikiwa havina uhakika juu ya nafasi ambayo watamaliza msimu huu. Timu yenye uhakika ni ile inayoshikilia nafasi ya kwanza ambapo inaweza kuhakikisha inabaki hapo au haishuki chini ya nafasi ya pili.

Wakati hayo yakiendelea tuigeukie Manchester City, klabu ambayo iliwatetemesha wengi kwa kipindi cha miaka minne mfululizo imenyakua taji la EPL na kulimiliki kana kwamba ni lao. Msimu huu hali imekuwa tofauti. Wachezaji wameporomoka, kocha amechoka kifikra kutokana na msongamano wa mambo ya kifamilia. 

Tanzania Sports

Miongoni mwa wachezaji ambao wameonekana kushuka makali yake ni nahodha wa sasa wa Man City, Kevin De Bruyne ak maarufu kwa jina la KDB. Nyota huyo alienzia soka la EPL katika klabu ya Chelsea, alilazimika kuondoka kutokana na kukosa nafasi. KDB aliondoka EPL si kwa kupenda bali alitaka dakika nyingi za kuonesha kipaji chake uwanjani, hivyo kuihama Chelsea iliyokuwa chini ya Jose Mourinho lilikuwa jambo sahihi kwake. Maisha ya soka katika klabu ya Wolfsburg yalimwendea vizuri na alicheza Bundesliga kwa kiwnago kizuri kilichowavutia wamiliki wa klabu mbalimbali. Akiwa kijana mdogo mwenye ndoto nyingi kutoka kwao Ubelgiji hadi England, lakini ghafla akaelekea Ujerumani ilidhihirisha jinsi anavyoweza kuchukua uamuzi mgumu. Uamuzi wa akuhamia Wolsfurg uliwezesha kupandisha chati yake na hapo ndipo Manchester City walibisha hodi na kuhitaji huduma ya kiungo huyo.

Kwa muda ambao amechezea klabu ya Man City hadi kuwa nahodha wao, KDB amefanya mambo makubwa ndani ya uwanja. Uchezaji wake, ufundi, kasi na uwezo wa kupiga mashuti umemwezesha kupata sifa nyingi kwenye mchezo wa soka. Akiwa kwenye uzi wa Man City ametwaa mataji mbalimbali. Sifa kubwa liyokuwa nayo ni kucheza kwa matokeo. Mara nyingi ali likitajwa jina lake alikuwa amefanya tukio la kiufundi ama amepachika bao au kuchangia upatikanaji wa mabao. Alikuwa nyota ambaye kila anapopangwa kikosi cha kwanza unaelewa kabisa kuna kaiz nzito anakuja kuifanya. KDB alikuwa mmoja ya silaha muhimu ya Man City na iliyompa kiburi Pep Guardiola. Popote ambapo Man City ingcheza basi moja kwa moja ilikuwa inakwenda kuogopesha wapinzani wao, na hasa aliyekuwa akiwatisha ni KDB.

Hata hivyo kila Nabii na zama zake. Kuna wakati ukimwona KDB akiwa ameinuliwa pale benchi ili aingie uwanjani basi kitu cha kwanza wanachofanya makocha wa timu pinzani ni kutoa maelekezo mapya kwa wachezaji wao iwe kubadilisha mfumo au kumpa kazi maalumu kudhibiti maarifa ya KDB kutamba. Ilikuwa ukimtazama nyota huyo akivaa jezi kutokea benchi au akiwa ameanza mechi unajua kabisa hali ya mchezo inakwenda kuwa ya maumivu makali kwa timu pinzani. Haijalishi Pep Guardiola atumie mfumo gani lakini kila mmoja angeweza kujua hatari ya KDB. 

Hofu ya wapinzani wa Man City ilianza kuondoka taratibu na hasa baada ya KDB kuporomoka kiwango kwa kiasi kikubwa. Hali mbaya ya Man City haitokani na kufeli vibaya kama timu bali uti wa mgongo wao wa timu ulianguka kwanza kisha timu nzima ikashuka na kugeuzwa kichwa cha mwendawazimu kwa msemo wa Rais Ali Hassan Mwinyi. 

Ilikuwa s rahisi kuifunga Man City hata goli moja, lakini walichapwa mabao 4-1 na Sporting Lisbon ikiwa chini ya Ruben Amorim huku KDB akionekana kama nyanya kikosini mwao. Katika kikosi cha Man City kwa sasa KDB anakuwa mchezaji ambaye hana uhakika kama atakuwepo timu hiyo msimu ujao. Ni mchezaji ambaye kuna kila dalili ataondoka kwa sababu nafasi yake inaweza kuzibwa kirahisi. Kw amfano mwezi Januari Man City wamemsajili Omar Mamoursh ambaye anaweza kucheza winga wa kulia, kushoto, mshambuliaji wa kati na mshambuliaji namba mbili yaani namba kumi. Hali kadhalika namba 10 au 8 anaweza kucheza Phil Foden na kuondoa uwezekano wa KDB kuendelea kubaki kikosini hapo. Wakati wawili hao wakiwa na uhakika wa kuchukua namba ya KDB, wapo Savinho na Bernado Silva wenye uwezo wa kuchezeshwa kama viungo washambuliaji. 

Kwa maana hiyo nafasi ya KDB inazidi kushuka na uwezekano wa kurudisha kiwnago unakuwa mdogo, huku mshahara anaopokea ni mkubwa zaidi. Bila shaka zama zake zimefika tamati na hataweza kufikia kiwango cha Luka Modric ambaye licha ya kuwa na umri wa miaka 38 bado anakipiga vyema La Liga huku akihusishwa pia kuhamia kwenye vilabu kadhaa vya EPL. Ama hakika kila nabii na zama zake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Wakaguzi wa viwanja vya Ligi Kuu wazomewe kwa uzembe

Tanzania Sports

EPL, Liverpool, kuhusu kipaji cha Federico Chiesa