in

Kama si pesa basi Mbappe atatafuta mataji

Mbappe

MWELEKEO wa sasa wa timu ya PSG ni kuonekana kama vile imekamailika zaidi kuliko zingine. PSG yasasa inavutia wachezaji wakubwa kwa uwezo wao wa kulipa fedha za usajili pamoja na ofa za mishahara minono klabuni hapo.

Kimsingi suala la fedha kwa PSG linaoekana kuwa si tatizo kabisa kwa sababu uongozi wake unadhihirisha kuwa fedja zipo na zinaweza kumsajili mchezaji yeyote.

Wakati PSG ikitunisha misuli sokoni,bado inakabiliwa na kibarua kigmu cha kumshawishi nyota wake Kylian Mbappe ili asalie klabuni hapo kuliko kumpoteza bure msimu ujao.

Ushawishi wa PSG unatumika kwa kuwasajili wachezaji wa viwango vya juu kama vile beki mkongwe Serguo Ramos ambaye ametua kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Real Madrid.

Vilevile kiraka Achraf Hakimi naye amesajiliwa kutoka Inter Milan ya Italia. Hata hivyo ndoto za Hakimi zipo wazi ni kurejea Real Madrid siku moja. Jiji la Madrid ndiko alikozaliwa na kukulia kisha kuichezea timu anayoipenda zaidi ya Real Madrid.

Kwahiyo usajili wake PSG ni sehemu ya kupita ambayo inatumika kumshawishi Mbappe asaini mkataba mpya kwa sababu nyota wanawasili ili kumhakikishia ndoto zake za kutwaa ubingwa wa Ulaya zinakuwa hai.

Wakati Mabppe akiwa njiapand kusaini mkataba mpya ama kuuzwa ama acheze msimu wa mwisho ili ukiisha aondoke bure msimu ujao kuelekea Real Madrid ni jambo lingine linalozua maswali.

Hata hivyo Real Madrid wanaonekana bayana kumtaka nyota huyo lakini wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kiwango kikubwa cha fedha cha kumsajili nyota huyo huko wenyewe wakikabiliwa na uhaba wa fedha. 

Mbappe kwa sasa ahaonekani kuvutiwa na mwelekeo uliokuwepo tangu msimu uliopita kwani timu yake ilikosa wachezaji wa kiwango cha juu hivyo kujikuta ikishindwa vita vya kupigania ubingwa wa Ulaya na Lique 1.

Kwa msingi huo, Mbappe anayo machaguo mawili hadi sasa, akubali kusaini mkataba mpya kubaki PSG na kuhahaka kusaka mataji au aondoke kwenda Real Madrid timu yenye uhakika wa kutwaa mataji ya Ulaya,tuzo za dunia na nyinginezo?

Hadi sasa Mbappe anaonekana yuko nusu kwa nusu abakie klabuni kwako hadi mwisho wa msimu na kuweka matumaini ya ubingwa wa Ulaya au aondoke kwenda Real Madrid kusaka mataji? Hakika hilo ni moja ya changamoto wanazokabiliana nazo kabi ya Mbappe kuamua hatima ya nyota huyo.

Kihistoria Real Madrid wanaweza kumshawishi nyota yeyote kwa sifa zao za kutwaa mataji,tuzo za dunia, wachezaji wa viwango vya juu na ule uhakika wa kugombania ubingwa kila msimu.

Lakini misimu mitatu Real Madrid hawajawa na uwezo wa kugombania ubingwa wa Ulaya. Ni msimu uliopita pekee walitolewa katika hatua ya nusu fainali, wakati msimu mmoja nyuma yake walitolewa katika raundi ya 16.

Sasa wanahitaji supastaa mmoja wa kung’arisha timu hiyo hivyo Mbappe ni chaguo lao baada ya Eden Hzard kuchemsha kubeba timu hiyo kama ilivyotyarajiwa.

Kwa maana hiyo Mbappe anatakiwa kuchagua njia ya kwenda sasa, ikiwa ataamua kuahama huenda kukawa na yimu zenye uwezo mkubwa wa kulipa fedha na mishahara lakini hazina historia iliyotukuka kama ya Real Madrfid.

Zipo Liverpool,Manchester  City au Manchester united zenye uwezo wa kumvutia nyota kwenye masuala ya fedha lakini upande wa Barcelona kuna changamoto za fedha ambazo zinamfanya rais mpya Juan Laporta awe anahangaika kutafuta fedha za kuimarisha timu hiyo.

Hii ina maana chaguo la kwenda Barcelona halipo, kwa sababu hakuna fedha. Machaguo yaliyobaki  yana kigezo cha fedha amabzo Mbappe anaweza kuzipata akiwa PSG, lakini hakuna timu yenye uwezo wa kugombania ubingwa wa ulaya kuizidi Reeal Madrid.

Ndoto ya ubingwa wa Ulaya ina maana kubwa kwa Real Madrid na wanakuwa mstari wa mbele kumnyakua nyota huyo.

Hata hivyo uwezo wao wa kulipa fedha za uhamisho unaonekana kushuka sababu kubwa ikitajwa ni uwekezaji katika marobesho ya uwanja wao wa Santiago Bernanebu, pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa corona ambao unatajwa kudhoofisha timu nyingi kiuchumi.

Halisi halisi inaonesha kuwa Mbappe anatamani kwenda Real Madrid lakini bado anatamani fedha za PSG. Fedha zitambakisha PSG lakini mataji ya ulaya na kimataigfa hayaonekani kutua PSG.

Wakati Mbappe akiwa njiapanda, upande wa Neymar Junior ulishafanya uamuzi wa kubaki PSG hadi mwaka 2025.

Mkataba wa Neymar una maana kubwa kwa Mbappe, kwamba anatakiwa kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake kubaki kikosini PSG au kuondoka.

Neymar amemaliza minong’ono kuhusu hatima yake ya baadaye ambapo naye alidaiwa kuwa angelihama timu hiyo baada ya kushindwa kuipatia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kulikuwa na habari nyingi zilizomhusisha Neymar kurejea Barcelona lakini sasa imedhihirika kuwa hatoondoka PSG.

Uamuzi wa Neymar kubaki PSG huenda ukatoa mchango mkubwa katika mkataba wa Mbappe kumshawishi kuendelea kukipiga klabuni hapo kwa lengo la kufanya jaribio lingine la kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa upande mmoja.

Upande wa pili mkataba wa Neymar una maana kuwa Mbappe ataendelea kuwa chini ya kivuli cha Mbarazil huyo hadi mwaka 2025  utakapokwisha na kuamua kuondoka.

Ama Mbappe aondoke kwenda kugombania namba kwenye kikosi cha makinda cha Real Madrid na kujihakikisha kufuata nyayo za mastaa kama Zinedine Zidane,Luis Figo,Ronaldo de Lima, Cristiano Ronaldo,Ricardo Kaka, Karima Benzema na wengine waliotamba kwa kunyakua tuzo mbalimbali.

Kubaki PSG ni kudidimiza ndoto za tuzo za uchezaji bora ulaya na dunia, lakini vile vile kukosa mataji ya Ulaya hata kama kocha wake Mauricio Pochettino ameongeza mkataba. Kwahiyo kama pesa zipo PSG, inabidi Mbappe atafute yaliyoko mataji ya Ulaya nje ya jiji la Paris.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Ligi Kuu Tanzania

TFF wamekosea uzani wa ‘Play-off’ ya kupanda na kushuka Ligi

Dar young africans

Nani kuibuka kinara wa mabao Yanga?