in , , ,

Jurgen Klopp ataumaliza msimu huu salama?

Wakati hekaheka za usajili wa Moses Caicedo zilipozidi kunguruma, kulikuw atimu kadhaa zilizohusishwa kumsjaili staa huyo. Chelsea na Real Madrid ni  iongoni mwao. Hata hivyo Liverpool iliingia katika hekaheka hizo na kupandisha dau la usajili hadi pauni milioni 110. Lakini Moses Ceicedo aligomea mpango w akwenda Liverpool na badala yake akabaki kusimamia msimamo wake wa kujiunga na Chelsea. Kiteno cha Ceicedo kuikatalia Liverepooll licha ya dau kubw ani kitu ambacho kimezua mjadala, na baadhi ya ripoti za vyombo vya habari zinasema jambo hilo limemsikitisha Jurgen Klopp. 

Kwa sasa mjadala mkubw aunakuwa nafasi ya Jurgen Klopp msimu huu kwa sababu Liverpool wameuza nyota kadhaa ili kusajili wapya, lakini bado hali ya mambo haioneshi kuleta mabadiliko. Mshambuliaji Roberto Firmino na nahodha Jordan Henderson, ni miongoni mwa nyota waliondoka Liverpool pamoja na viungo wenzake Fabinho, James Milner, Naby Keita, huku winga Alex Chambaerlain akijiunga na Besiktas. 

Ni dhahiri Jurgen Klopp anahitaji majembe mapya ili kuimarisha kikosi cha Liverpool. Kuondokewa na wachezaji wote hao lazima usajili mwingine wa nguvu ufanyike. Hivi karibuni tumemsikia Virjil van Diyk akilalamikia kuuzwa wachezaji kadhaa muhimu na kusajiliwa nyota wawili pekee. Beki huyo kisiki alisema kuwa anaelewa hali ya mambo kwa wachezaji na timu, lakini kuongeza wachezaji wapya ni jambo muhimu. 

Tanzania Sports

Huu ni ujumbe muhimu kwa viongozi wa Liverpool pamoja na benchi la ufundi. Kuondokewa wachezaji hao pia kunakumbusha namna Fernando Torres alivyochukua uamuzi wa haraka kuondoka Liverpool miaka kadhaa iliyopita kutokana na kuuzwa wachezjai muhimu huku uongozi ukiwa kimya kuleta wachezaji wapya. 

Akiandika katika kitabu chake Torres amefafanua kuwa ulikuwa uamuzi wa haraka na mgumu kwa sababu wachezaji muhimu wanapoondoka laizma timu iangalie inasajili aina gani ya wachezjai ili waweze kuziba pengo lao. Kwa kuwa hakukuw ana usajili wa maana huku msimu mpya ukikaribia, Fernando Torres aliamua kuhamia Chelsea. 

Wengi wanakumbuka sakata hilo, lakini ukweli wa mambo umewekwa kwenye kitabu chake akifafanua masuala mengi ya usajili hasa kuuza wachezaji muhimu na kuiachia timu pengo lisilozibika. Kw amsingi huo,  Jurgen Klopp ameachiwa mapengo ya kuziba lakini baadhi ya wachezaji anaowataka hawataki kwenda Liverpool. Kuingia kwa Liverpool katika sakata la usajili wa Moses Ceicedo ilidhaniwa angebadilisha uamuzi na kwenda Liverpool hivyo Chelsea ingeachwa njia panda kisa dau kubwa kutoka kwa Jurgen Klopp. 

Liverpool imekuwa timu yenye ushindani mkubwa kwa misimu takribani 8 sasa kutokana na ufundi na umahiri wa Jurgen Klopp. Ikiwa Jurgen Klopp hatapewa bajeti ya kutosha kujenga timu hadi Agosti 31 mwaka huu kuna dalili wakaingia kwenye sakata linguine kama la Fernando Torres. 

Kwani wachezaji mastaa kama Virjil van Diyk wameshaonesha hali ya wasiwasi katika kikosi hicho na huenda ikaambukizwa kwa chipukizi wao. Liverpool si timu mbaya, lakini inaweza kukutana na msimu mbaya kama uliopita. Pengine kuwoandoa nyota hao na kuwauza inawezekana ikaemwa walifikia mwisho w aukomo wa uwezo wao, lakini bila kusajili  wapya  watazalisha tatizo linguine. 

Tanzania Sports

Kwa msingi huo atakayeumizwa kichwa zaidi ni Jurgen Klopp kwani ataambiwa rasilimali watu zote zipo kikosini mwake na anatakiwa kuzitumia kusaka ushindi kwa namna yoyote ile. Je unawezaje kutegemea timu ya wachezaji chipukizi kusaka ubingwa wa EPL? Bila shaka hilo haliwezekani, kwa sababu kila timu inahitaji mseto wa wachezaji ili kuibuka na ubingwa. Kuna wachezaji chipukizi lakini hawawezi kumpa Jurgen Klopp uzoefu katika mechi ngumu.  

Wachezaji wenye uzoefu na chipukizi wakiwekwa pamoja wanazalisha kitu kinachompa ahueni kocha, lakini kinyume cha hayo itawawia vigumu Liverpool kutamba mbele ya timu kama Arsenal, Chelsea,Man City au Man United.  Kipindi hiki timu zinahaha kuvijenga vikosi vyao, lakini Liverpool wnaaonekana majribio yao ya kusajili wachezaji wa kuziba mapengo yagonga mwamba. Kufikia hapo ndipo swali linaulizwa, itakuwa wapi nafasi ya Jurgen Klopp? Ataumaliza msimu huu akiwa timu hiyo hiyo bila ongezeko la wachezjai wa kuimarisha kikosi chake? Kw ahakika hili ni jambo la kusubiri na kuona.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ngao ya Hisani imewapa nguvu  Simba

Tanzania Sports

MASON  GREENWOOD NJIA PANDA MAN UNITED