in , ,

MASON  GREENWOOD NJIA PANDA MAN UNITED

Ni  bonge la mchezaji. Ni kijana mdogo sana kiumri  ambaye ametumikia adhabu ya kuwa nje ya klabu kwa mwaka moja hivi sasa….

MSIMU mpya umeanza, huku klabu ya Manchester United ikiwa imecheza mchezo mmoja dhidi ya Wolves. Katika mchezo huo Manchester United walishinda 1-0, lakini jambo ambalo linazidi kuvuma miongoni mwa mashabiki wa soka ni hatima ya kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood. Nyota huyo alikuwa anakabiliwa na mashtaka Mahakamani, ambayo yamefutwa na Ofisi ya Mwendesha mashtaka nchini England. 

Tangu kufutiwa mashtaka dhidi yake, bado Mason Greenwood hajapata nafasi ya kutumikia klabu yake. Nyota huyo alikuwa anachunguzwa na waajiri wake ambao  walichukua hatua hiyo bila kujali kilichotokea Mahakamani. Hadi sasa inaonesha kuwa matumaini ya washabiki wa kandanda duniani kumwona Mason Greenwood akitandaza kandanda yanazidi kufifia. Kumekuwa na giza totoro katika kipaji cha kijana huyo na inazidi kuongeza joto kali juu ya hatima yake.

MAN UNITED NJIA PANDA

Kimsingi hili suala la Mason Greenwood  linawapa Manchester United wakati mgumu sana kufanya uamuzi. Sababu ya kushindwa kuamua. ni kutokana na presha ya nje ya timu hiyo hususani  wanaharakati ambao wamekuwa wakilivalia njuga hadi sasa.

Wanaharakati hawajali kuwa Mahakama imefuta shtaka dhidi ya Mason Greenwood, ni kama wanatamani kijana huyo apotee kabisa katika Ulimwengu wa soka au wanataka aondoke Manchester United. Ikiwa Mahakama imefuta shtaka dhidi yake, ni kwanini asichezee Manchester United?  

Vilevile kulingana na uamuzi wa Mahakama, ni kwanini Manchester United wanashindwa kumpa nafasi ya kucheza kandanda?  Greenwood ana kipaji kizuri na anaweza kujiunga na timu kama Arsenal na akafanya vizuri. Ni  bonge la mchezaji. Ni kijana mdogo sana kiumri  ambaye ametumikia adhabu ya kuwa nje ya klabu kwa mwaka moja hivi sasa. 

Greenwood alishachukua hatua kumwomba radhi mpenzi wake ambaye sasa ni mzazi mwenzake. Nayo Mahakama ilishafuta shauri dhidi yake, sijui ni kwanini wanataka kuua kipaji chake wakati kama adhabu kishaitumikia tena bila hatia kuthibitishwa? Hapa wanaharakati katika klabu wanailazimisha Manchester United kumhukumu mtu ambaye amesimamishwa muda mrefu kwa kupisha uchunguzi. Sasa uchunguzi umeisha, wanajua hana kesi ya kujibu, wamebaki njia panda. 

Katika mazingira hayo, lazima Manchester United watakuwa wanabughudhiwa na kujikuta wakishindwa kutolea uamuzi wa mwisho kwa Mason. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanasema inawezekana Mason akirejeshwa, huenda hatojisikia nyumbani tena. Kwahiyo, iwe  atarejeshwa au la, njia pekee kwake ni kwenda kuanza maisha yake ya soka mahali pengine.

Inawezekana kuwa Manchester United  wakimrudisha Mason huenda wanaharakati hawatawaacha salama, ila pia kumuacha mchezaji huyo watu wa haki za Binadamu watapiga kelele pia kwamba klabu hiyo imemwonwa Mason. Huenda hili la mwisho ndilo linalotajwa kuwaweka njia panda Manchester United.

TAARIFA TATA

Uongozi wa Manchester United kwa upande wake umetoa taarifa kuwa haukafanya uamuzi wowote kuhusu mchezaji wao Mason Greenwood, lakini wanatarajia kuchukua uamuzi wakati wowote. Kitendawili hiki ndicho kinazidisha utata juu ya hatima ya Nyota huyo. Kwamba Manchester United watafanya lini uamuzi wao kuhusu Mason Greenwood iwe wa kumwondoa au kumrejesha kundini.

ANAWEZA KUUZWA?

Uwezekano wa hili huenda ukawa mdogo, badala yake Manchester United wanaweza kusubiri hadi mwisho wa mkataba wake kisha wakamwandikia barua maarufu kama zinazofanywa na vilabu vikongwe nchini Yanga na Simba. Wachezaji huagwa kwa namna yake, na huenda ikiwa sio Jambo la kujivunia. Greenwood anaweza kupata nafasi katika vilabu mbalimbali duniani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Jurgen Klopp ataumaliza msimu huu salama?

Tanzania Sports

Wadhamini Ligi Kuu nunueni haki za sura za wachezaji