in , , ,

Jude Bellingham amejibu kwanini yupo Real Madrid

WAKATI wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2024, jina la Jude Bellligham liligonga vichwa vya habari na kuzua mjadala mkubwa. Kulikuwa na kila sababu za kuibuliwa mjadala huo kwa jinsi walivyo wenzetu Waingereza wakianza kushmbulia jambo tangu mawio hadi machweo, watalala nalo na kuamka nalo. Jude Bellingham alikosolewa kwa kile kinachoitwa ana maringo mengi kiwanjani kwa sababu alikuwa ni mchezaji wa Real Madrid. 

Wachambuzi na baadhi ya wadau wa soka walikosoa uchezaji wake katika timu ya Taifa na kudai Jude Belligham anajiona yeye ni Lionel Messi wa England. Wakaenda mbali na kusema Jude Belligham alikuwa anahisi wachezaji wenzake kwenye kikosi cha aliyekuwa kocha wa England, Gareth Southgate hawakuwa na kiwango kumzidi yeye. Wakasema kijana wao ana maringo mengi na ameonesha kuwa yeye ndiye mfalme kwa timu ya taifa ya England. Kukosolewa na kuchambuliwa ni sehemu ya mchezo wa soka na maisha. Jude Belligham pia amekosolewa na wakati mwingine kubezwa kwa sababu ya hali yake ya sasa. Je kwanini ilikuwa muhimu kwa Jude Belligham kujibu swali la kwanini yupo Real Madrid.

Anapita njia ya Owen Hargreaves

Bao la tatu alilofunga Jude Belligham dhidi ya Manchester City lilitosha kutoa ujumbe kuwa alikuwa kazini na kuwaonesha jinsi gani anaweza kuwafurahisha na kuwasikitisha kwa wakati mmoja. Jude Bellingham ana sifa moja inayofanana na Owen Hargreaves. Wote wawili hawakuwa na majina makubwa katika Ligi Kuu England. Jude Belligham hajawahi kucheza EPL na hivyo umaarufu wake kwenye ligi hiyo haupo. Pengine washabiki wa soka ambao hawakufahamu umahiri wake kiwanjani, hawakuwa wakielewa kwanini Real Madrid imwendea na kumsajili. Owen Hargreaves hakuwa maarufu katika Ligi Kuu England, ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa mechi mbalimbali kwenye Televisheni. 

Wawili hawa hawakuwa na majina England, badala yake walikuwa wakionekana nyumbani kwao huko wakiitwa timu ya Taifa. Owen Hargreaves alikuwa kiungo na winga matata sana akiwa Bayern Munich. Lilikuwa jambo la furaha kjuona kipaji hicho cha England kikifurukuta nje ya mipaka yao. ndani ya kikosi cha Bayern Munich Owen Hargreaves angeweza kucheza kama kiungo mkabaji, kisha anaweza kumpa kocha wakati mzuri kama atampanga winga wa kulia. Kana kwamba haitoshi Owen Hargreaves anaweza kuichezesha timu vyema sana akiwa kiungo nambari 8. 

Uchezaji wake ulijumuisha kasi na maarifa na ungeweza kushangaa kama ni mzaliwa wa England. Naye kama walivyo wenzake alitamani kuwa maarufu katika Ligi ya nyumbani kwako England, hivyo hakushangaza alipoamua kukubali uhamisho kutoka Bayern Munich kwenda Manchester United ya Alex Ferguson. Hakuna mchezaji ambaye angelikataa wakati ule kucheza chini ya Alex Ferguson, hivyo Owen alikuwa sahihi. Kabla ya kuhamia Manchester United, Owen Hargreaves alikuwa akiitwa timu ya Taifa mara kwa mara na kuonesha uwezo wake. lakini kitu kimoja ambacho kilimkabili ni ‘bond’ yake na mashabiki. Hiki ndicho kinachoendelea kati ya Jude Belligham na mashabiki wa England. 

Kijana huyu ameandika jinja lake na umaarufu wake kwenye Ligi Kuu Ujerumani maarufu kaa BundesLiga. Kwenye Bundesliga, jina la Jude Belligham ni maarufu sana na anao mtaji wa mashabiki., lakini nyumbani kwao England hana umaarufu katika Ligi. Kwenye timu ya Taifa ndicho anakojaribu kujenga bond’ yake na mashabiki. Lakini ili aupate upendo wa mashabiki wa nyumbani kwao ni vyema wakamuona kila siku. Je, ataondokaje kwenye timu kubwa duniani kama Real Madrid? Haiwezekani.

Mbele ya lango na mstari wa kiungo

Kwenye mchezo dhidi ya Manchester City, Jude Bellingham alitumia muda mwingi katika eneo la kiungo. Eneo hilo kulikuwa na wachezaji wenzake wawili Dani Ceballos na Eduardo Camavinga. Watatu hawa walisababisha kiungo cha Man City kiwe kinavunjika vipande kutoka eneo la mabeki hadi viungo na washambuliaji. Sababu ya hilo ni kwamba Jude Belligham alikuwa na kazi ya kuipeleka mbele timu huku akilindwa na Ceballos na Camavinga. Zile mbio zake, chenga, pasi za mwisho na kombinenga aliyonayo na Rodrygo, Vini na sasa Mbappe inamfanya awe na maringo kwa sababu anacheza kwenye timu yenye vipaji vikubwa. 

Bao lake la tatu lililonesha namna avyoweza kutumika kama mshambuliaji w apili (namba kumi) kama ulivyokuwa msimu wake  wa kwanza. Jude Bellingan anakupa mabao, analinda timu yako na anaweza kuwafanya wapinzani  wakose nafasi ya kumdhibiti kwa sababu hatari zake haziji katika mazingira yanayotarajiwa. 

Bao la huzuni na majibu

Bao la tatu alilofunga liliwaachia huzuni mashabiki wa Man City, lakini pia lilionesha umahiri na kutoa ujumbe kwanini anajisikia na mwenye maringo. Kucheza na wachezaji wenye maarifa makubwa, muono mzuri wa mchezo, uwezo wa kupangua safu ya ulinzi na ufundi binafsi ndivyo vitu alivyokosa Jude Belligham katika timu ya Taifa ya England. Pale England hawana Vinicius Junior, Rodrygo wala pasi za Camavinga. Kukosekana wachezaji kama hao lazima Bellingham atajiona yeye ndiye Lionel Messi. 

Bahati aliyonayo katika kikosi cha England ni kucheza na Declan Rice, kiungo mkabaji mwenye macho mazuri na akili nzuri ya kiufundi. Kiungo anayejua kuliona bao linakoweza kupitia. Huyu ndiye mchezaji ambaye anaweza kumpa furaha Jude Bellinghma. Laiti kungekuwa na wachezaji kama huyo wanne wa England bila shaka Jude Bellingham asingewaletea Waingereza mapozi. Kwa bao hilo, na wakirudi nyuma msimu uliopita jinsi alivyotumbukiza penati yake, inabidi wakubali tu Jude Bellingham yuko Real Madrid kwa sababu ana maarifa makubwa kuliko wale waliomzunguka akiwa timu ya taifa ya England. Badala yake ni England wakubali tu, kijana wao anapepeusha vema bendera ya nchi yao na wampe mapenzi yote ya upendo. Na ukipenda muite Jude BellinGoal

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Clement Turpin ni refa wa aina yake

Tanzania Sports

UONGOZI YANGA UACHE PAPARA KAMA MAN UNITED