in , , ,

Je, Real Madrid kuhama La Liga?

WIKI hii habari kubwa iliyoripotiwa ni taarifa ya klabu ya Real Madrid kutaka kujiondoa katika Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga ili kujiunga na ligi ya nchi nyingine, huku ikielezwa zipo nchi tatu ambazo klabu hiyo inaweza kujiunga nazo. Taarifa zinaeleza kuwa Real Madrid inafikiria kuchukua uamuzi huo kutokana na kushuhudia wimbi la maamuzi mabovu ya marefa kwenye mechi zao ikiwemo tukio la kulimwa kadi nyekundu kiungo wake Jude Bellingham wikiendi iliyopita wakati wa mchezo wao dhidi ya Osasuna. 

Jude Bellingham alitlimwa kadi nyekundu na refa Jose Luis Munuera Montero kwa madai kwamba kiungo huyo alitumia lugha ya kudhalilisha hivyo akaadhibiwa kadi nyekundu. Mwamuzi huyo wa Hispania anatuhumiwa kumtoa nje Jude Bellingham kwa madai ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi baada ya kughafilika kwa usimamizi wa refa huyo katika mchezo huo. 

Sababu za kutolewa Bellingham

Hata hivyo tuhuma za mwamuzi huyo zinakanushwa na Bellingham mwenyewe pamoja na kocha wake, kwamba hakutumia maneno ya lugha chafu dhidi ya mwamuzi bali alijisemea mwenyewe. Mwamuzi wa mchezo huo anadai kwamba Bellingham alitamka neno “f*ck You”, wakati mchezaji mwenyewe anasema hakutamka neno hilo badala yake alisema “f*ck off”. Tofauti ya maneno na maana zake ndizo zinazodaiwa kuingiza mjadala huo ambao Real Madrid imeendeleza lawama zake kwa shirikisho la soka la nchi hiyo. Carlo Ancelotti amebainisha kulikuwa na maelewano mabaya kati ya mwamuzi na mchezaji wake na hivyo mwamuzi alichukua hatua ambayo haihusiani na kile anachodai. 

Bellingham amedai kuwa kwa lugha za kwao England, neno “f*ck off” sio tusi wala sio kashfa kw ayeyote. Tafsiri ya neno hilo kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na “kwenda zako” au “nenda zako wewe”.

Kwa mujibu wa ripoti za vombo vya habari nchini Hispania zimeeleza kuwa Real Madrid wanafikiria mpango wao wa kuachana na La Liga na kwenda kujiunga nan chi nyingine inayoshiriki mashindano ya Ulaya. Sababu za kutamani kuondoka La Liga ni maamuzi mabaya yanayotolewa viwanjani dhidi ya timu hiyo.

Wazo la kuhamia Ligi nyingine

Tanzania Sports

Ripoti zinasema Real Madrid imweka kipaumbele kwa Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Seria A, huku nafasi ya pili inafikiriwa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 pamoja na Ligi Kuu ya Ujerumani inayofahamika kama Bundesliga ili kutatua matatizo wanayokabiliana nayo kwenye ligi ya Hispania. Endapo Real Madrid itahamia katika Ligi hizo maana yake itaendelea kushiriki mashindano ya Ulaya na kubaki kuwa mwanachama wa shirikisho hilo.

Je uamuzi huo una athari gani?

Hata hivyo mabadiliko yoyote ya kuhama Ligi kwa Real Madrid yatatakiwa kuidhinishwa na shirikisho la soka la Dunia, FIFA pamoja na Ligi mwenyeji ambako timu hiyo itahamia. Vilevile Real Madrid watahitaji idhini ya shirikisho la soka la Ulaya, UEFA ili kuhama Ligi ya Hispania na kujiunga kwingineko. Ripoti za vyombo vya habari zinasema ikiwa Real Madrid itasimama kidete katika uamuzi huo kwa hadhi yao litakuwa jambo ambalo litaimarisha Ligi watakayohamia kwa sababu wao ni taasisi kubwa duniani na yenye rekodi za kipekee katika mchezo wa soka. Madrid wamekuwa wakilalamikia maamuzi ya marefa wa La Liga katika mechi zao mbalimbali, huku tukio la Bellingham likiwa limeongezeka kwenye orodha ya matukio yenye utata yanayofanywa na waamuzi hao.

Mapema mwanzoni mwa mwezi Februari, baada ya Bellingham kutolewa nje klabu ya Real Madrid iliwasilisha malalamiko yao kwa shirikisho la soka nchini Hispania, huku ikibainishwa kuwa tabia za waamuzi zimekuwa mbaya na kinyume cha sheria za soka.

Kikosi cha kocha Carlo Ancelotti kilipoteza mchezo dhidi ya Epsanyol kwa bao 1-0, ambapo kulitokea tukio la faulo baada ya beki Carlos Romero kufunga bao hilo katika dkaika 85 kwa wenyeji. Kabla ya goli hilo mwamuzi alishindwa kusimamia sheria pale mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappe alipochezewa faulo mbaya. Real Madrid ilisema kuwa Romero alitakiwa kutolewa nje ya uwanja na hakupaswa kuendelea na mchezo huo kwani alifanya faulo za makusudi lakini mwamuzi hakuchukua hatua zozote.

Masharti ya Real Madrid

Mara baada ya Real Madrid kuwasilisha malalamiko yao ambayo yalisema, “Matukio yaliyotokea kwenye mchezo huo yamezidi kipimo cha makosa ya binadamu au refa kushindwa kutafsiri sheria. Kilichotokea kwenye uwanja wa RCDE ni uthibitisho wa kufeli kwa mfumo mzima wa wamuzi, ambapo uamuzi unatolewa dhidi ya Real Madrid umefikia kiwango kisichovumilika, ambacho marefa wanafanya hadaa za wazi na kuonesha chuki pamoja na kupunguza ldha ya ushindani wa mpira kiasi kwamba wanazidi kupuuzwa na kuufanya mchezo wa soka upoteze heshima na kuonekana hauna maana. Kutokana na vitendo visivyozingatia sheria. Mosi, Real Madrid inataka kwamba shirikisho la soka Hispania haraka litoe hadharani Audio ya mazungumzo ya waamuzi wa VAR na yule wa kati kuhusiana na tukio la Romero dhidi ya Kylian Mbappe. Pili, Audio ya mawasiliano kati ya waamuzi wa VAR na yule wa uwanjani kwenye mchezo ambao goli la Vinicius Junior lilikataliwa. Tatu, majadiliano kati ya waamuzi wa VAR na wale wa uwanjani,”

Mara baada ya taarifa ya Real Madrid kutolewa, Rais wa La Liga, Javier Tebas alijibu mapigo kwa kuelza kwamba katika mkutano waliofanya kabla klabu hiyo ilishindwa kuwasilisha mbinu mbadala za kukabiliana na matatizo yanayotokea uwanjani. Kwa mujibuwa wa gazeti la Marca, Javier Tebas alisema, “Sikushangazwa na barua ya Real Madrid kwa sababu haisemi chochote cha kipekee kwani vyote vinaonekana katika televisheni na vitendo hivyo vimetokea mara  kadhaa. Wengi wetu tunaunga mkono mabadiliko ya kimfumo, ili tuweze kukaribia mtindo wa Ligi ya England au Ujerumani, tukiwa na kitu chetu cha tofauti kama taasisi na zaidi kwa uwazi wa maamuzi yanayochukuliwa na waamuzi kwa mfumo wa Hispania.”

Je Bellingham ataadhibiwa?

Wakati huo huo, baada ya kutolewa nje jumamosi iliyopita, Belllingham akabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi 12 kutokana na tuhuma za matamshi ya kudhalilisha dhidi ya mwamuzi. Sheria za La Liga zinasema, “kumdhalilisha refa, kutukana au kuashiria lugha zamatusi dhidi ya refa, wasaidizi wake, refa wa akiba, wakurugenzi, na mamlaka za michezo na mengine yenye nia ovu, adhabu yake ni kusimamishwa mengi 12,”

Endapo adhabu hiyo itatekelezwa, Bellingham atakosa mechi za Girona, Real Betis na Rayo Vallecano, pamoja na mechi ya nusu fainali ya kwanza ya Cope Del Rey dhidi ya Real Sociedad. Pia anaweza kukosa mechi zilizobaki katika msimu huu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Fahamu mambo muhimu Yanga na Singida Black Stars

Tanzania Sports

Masharti mapya Ligi Kuu Tanzania