in , ,

Je ni : De Gea, Van Der Sar, au Peter Schmeichel?

Nyakati nyingi huja na majira tofauti, hakuna mwaka ambao huja na majira yanayofanana.

Hii yote inaonesha kila siku huja na kitu kipya chenye utofauti au kushabiana na kitu cha jana.

Kila mawio na machweo huja na kizazi kipya kitakachokuja kurithi kizazi cha zamani.

Hakuna kizazi ambacho huishi milele, kila kizazi huwa na wakati wake wa kuishi, hakuna kizazi chenye pumzi ya milele.

Ndiyo maana kizazi kimoja hufa ili kukipisha kizazi kingine.

Kizazi cha Peter Schmeichel kilikuwepo, kilifanya makubwa sana kwa wakati huo, makubwa ambayo yalileta heshima kwao.

Kipa ambaye anatajwa kama kipa bora wa wakati wote.

Hata mwaka 2000 kulipofanyika kura za wazi alifanikiwa kuchaguliwa kama kipa bora wa wakati wote akifanikiwa kuwashinda Lev Yashin na Gordon Banks.

Hata IFFHS limemweka kama kipa bora wa muda wote.

Huyu ndiye kipa ambaye alifanikiwa kufunga magoli 11 katika kipindi chake cha kucheza .

Kipa ambaye aliitumikia Manchester United na kuacha alama kubwa.

Wakati anakuja alikuwa hana jina kubwa ambalo lingemfanya shabiki yoyote wa Manchester United kujivunia kuwa wamepata kipa bora.

Walihitaji muda kudhibitisha ubora wake, msimu wake wa kwanza Manchester United wakamaliza nafasi ya pili.

Msimu wa pili wa mwaka 1992/1993 , Peter Schmeichel alimaliza akiwa na mechi 22 kati ya mechi 38 bila kufungwa goli, kitu kilichoisaidia Manchesher United kuchukua ubingwa.

Ubora wake ulikolezwa zaidi na mafanikio ya msimu wa mwaka 1998/1999 msimu ambao Manchester United walifanikiwa kuchukua makombe matatu yani kombe la ligi kuu, kombe la chama na kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mafanikio ambayo yanakumbukwa sana na kila shabiki wa Manchester United.

Peter Schmeichel alitoa mchomo wa penalti wa Denis Berkghamp katika nusu fainali ya kombe la chama FA.

Kitu kilichompa heshima sana, na mwisho wa siku alikuwa nahodha wa mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich ambapo Manchester United walikuwa wakikamirisha kombe lao la tatu.

Alama yake aliyoweka Manchester United ilikuwa ngumu kufutika, hata wakati anaondoka alikosekana mtu sahihi wa kuja kuziba pengo lake.

Mwanzoni Manchester United walivutika na Van Der Ser aliyekuwa Ajax.

Van Der Ser alifanikiwa kuwa miongoni mwa kizazi cha dhahabu cha Ajax.

Alidumu kwa miaka 9, muda wote Manchester United walikuwa wanasubiri ujio wake, lakini Juventus walimchelewesha kufika Old Trafford.

Ilipangwa apitie Juventus , aje Fulham ndipo afike Manchester United, nyumbani kwake ambako alifanikiwa kuchukua kombe la ligi kuu akiwa na umri mkubwa wa miaka 40.

Sehemu ambayo alicheza kama nahodha, akiiongoza Manchester United kuchukua vikombe kama kombe la ligi kuu, kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya, kombe la chama cha soka nchini England.

Sehemu ambayo aliweka rekodi ya kucheza dakika 1,311 bila kufungwa goli huku akimaliza msimu akiwa na michezo 21 bila kufungwa goli lolote lile, kitu ambacho kiliisaidia Manchester United kuchukua kombe lao la 11.

Pamoja na kwamba Edwin Van Der Ser alienda Manchester United umri ukiwa umesogea, lakini alibaki kuwa mmoja wa magolikipa bora kuwahi kupita Manchester United.

Swali lilibaki nani ambaye alitakiwa kuja kubeba nafasi yake baada ya kuondoka.

Mtu wa kuja kuziba pengo la Edwin Van Der Ser ndiye aliyekuwa anasubiliwa.

Sir Alex akawaletea mashabiki wa Manchester United, David De Gea.

Mchezaji ambaye alitoka Atletico Madrid, watu wengi hawakuwa na matazamio makubwa juu yake.

Lakini Sir Alex alikuwa na imani kubwa sana juu yake, hata sehemu ambayo aliyokosea alimsihi kuyatumia makosa kama funzo.

Alijifunza mengi, kucheza kwenye timu kubwa dunia, timu yenye kuhitaji ushindi kila mechi.

Kwake yeye presha hii alifanikiwa kuimeza na kutembea nayo mpaka akaizoea.

Leo hii anaonekana ni mchezaji bora na muhimu katika kikosi cha Manchester United.

Amekuwa akiibeba Manchester United katika ugumu wote, na akiwa tayari kaweka rekodi ya ligi kuu ya England ya kutoa michomo 14 katika mechi moja.

Ubora wake umeimarika kwa kiasi kikubwa, ubora ambao unatufanya tubaki na swali kati yake , Peter na Edwin nani ni kipa bora katika timu ya Manchester United? Ingawa wenzake washawahi kuwa manahodha wa timu hii.

mail to: [email protected]

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

REAL MADRID ILIJIBOMOA YENYEWE

Tanzania Sports

ZANZIBAR ANZENI HAPA NDIPO NITAWASIFIA NA MIMI