in , , ,

JE MAKOCHA NA FEDHA NDIYO TEGEMEO KUU LA USHINDI ?

 
Karibuni runinga (TV) ya African Channel imeeleza wastani wa umri wa maisha ya wanadamu nchi zilizoendelea umeongezeka kwa miaka mitano (wanaume) na sita (wanawake) kati ya 1990 hadi 2013. TV hii ilinukuu takwimu zilizotolewa na bloga la Sayansi ya kimataifa na kusisitiza kwamba umri wa maisha ya Waafrika unashuka chini kutokana na hali ya duni ya maisha inayosababishwa na umaskini na maradhi .

Michezo nayo inaathirika sana. Tukiangalia kiwango cha maendeleo ya timu za mpira nchi tajiri hupiga hatua kutokana na fedha na makocha. Miaka 15 iliyopita Chelsea haikuwa ikisikika sana, ila kutokana na kipato inaongoza ligi ya England.

Juzi hapa Yanga na Simba zimebadili tena makocha. Hans Van de Pluijm aliingia mjini kwa kishindo. Uchaguzi wa kocha ni muhimu si tu kwa Yanga na klabu nyingine, vile vile kwa timu ya taifa.

Bila shaka, wapenzi wa michezo na wataalamu, wanaafiki kocha ndiye huwa kiungo cha mchezaji. Kipindi ambacho bondia maarufu Mike Tyson alipotamba alikumbwa na furaha na majonzi. Tyson alizaliwa na kukulia katika shida ambazo zilizomfanya awe kibaka na kuishia jela ya watoto.
20140106-180158.jpg

Baba yake mwenye asili ya Kijamaika alimkimbia mama na hatimaye mama akafariki Tyson akiwa na miaka 16. Kutokana na kutaniwa na watoto wenzake mitaani alipigana pigana ovyo.
Bahati nzuri maisha yake yaliokolewa alivyoanza kujifunza ngumi. Hatimaye alimpata kocha maarufu, Cus D’Amato aliyegeuka mlezi na mzazi. Amato alikuwa kocha mwenye mtindo na utaalamu wa kipekee.

Akiwa na miaka 18 mwaka 1985 Tyson alianza kushinda kila pambano. Bahati mbaya kipigo kikali kilimfika baada ya kocha wake mzee Cus D’Amato alipofariki. Kuanzia hapo Mike Tsyon alisakamwa na matatizo ya mahusiano na wanawake, mizozo, madeni na polisi au dawa za kulevya. Tathmini iliyopo ni kama kocha Amato asingefariki mapema , leo Mike Tsyon angekuwa vingine.

Kocha wa Chelsea , Jose Mario Dos Santos Mourinho, alizaliwa katika familia ya mpira maana baba yake, aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ureno. Akiwa kijana Jose alichezea timu mbalimbali za mpira ikiwemo, Os Belenenses na Rio Ave. Lakini kutokana na kutokuwa na mbio na nguvu za kutosha alijifunza ukocha. Mafunzo yalimchukua miaka mitano na akawa msaidizi wa makocha wakubwa wakubwa kama Louis Van Gaal ( Manchester United) na marehem Bob Robson aliyekuwa kocha wa Barcelona, New Castle na Uingereza. Kutoka marehem Robson Mourinho alijifunza lililoandikwa katika gazeti la Times , 2008:

“Ukishinda usijigambe wewe bora kuzidi wengine, na ukipoteza mechi usidhani wewe mpumbavu au hujui kucheza.”

Mourinho amejenga umaarufu Chelsea ambayo zamani haikuwa timu kubwa. Chelsea ilianza kufundishwa na kocha wa Kiholanzi, Ruud Gullit aliyekuwa mshambuliaji maarufu wa Uholanzi miaka ya 1980. Akiwa meneja wa Chelsea mwaka 1997 kwa mara ya kwanza katika miaka 26 Chelsea ilishinda kombe la FA Cup na kupanda nafasi ya sita katika ligi ya England.

Kuingia kwa Mourinho, mwaka 2004 hadi leo, timu ya Chelsea ambayo zamani ilikuwa na sifa ya ubaguzi wa na kutokuwa na wachezaji wa kigeni au weusi mambo yamebadilika. Ama kweli ushindi au kuanguka kwa wachezaji hutegemea makocha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Vinara wa ligi wapunguzwa nguvu

KUONDOKA MCHEZAJI STEVEN GERRARD WA LIVERPOOL KUMETINGISHA DUNIA YA SOKA