in , , ,

KUONDOKA MCHEZAJI STEVEN GERRARD WA LIVERPOOL KUMETINGISHA DUNIA YA SOKA

 
Wiki hii habari za kuthibitika zimekiri Steven Gerrard ataihama klabu kongwe ya Liverpool mwisho wa ligi na kuchezea timu ya LA Galaxy Marekani. Utata wa kuhama kwake ulianza mwaka 2003 wakati nguli wa soka, Zinedine Zidane, Mfaransa mwenye asili ya Kiarabu (Algeria) aliyekuwa akiichezea Real Madrid alipopendekeza wamnunue Steve Gerrard. Zidane ni kati ya wanasoka mashuhuri duniani aliyesifia sana ujuzi wake Steven Gerrard.

Akifanyiwa mahojiano na gazeti la daily Telegraph mwaka 2009 Zinedine Zidane alikiri Steve Gerrard ni mchezaji bora kuzidi wote duniani. Alisisitiza kila timu yahitaji injini inayosukuma timu mbele, mtu mwenye mshipa na kujiamini, anayebadili mchezo.

Zidane aliendelea kudai mlinzi na kiungo mashuhuri mstaafu, Claude Makelele alikuwa hivyo kwa Real Madrid na Patrick Vieira kwa Arsenal. Akasitiza kuwa ingawa Gerrard hasikiki kama akina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kazi yake si nyepesi.

Zidane : “Wachezaji kama hawa hawafundishwi. Wanazaliwa hivyo. Anapasi nzuri, hupigania mpira , kulinda timu na kufunga mabao. Huwapa wachezaji wenzake kujiamini na imani.”
Stephen George Gerrard alianzia mpira angali mdogo wa miaka tisa katika klabu ya Liverpool. Mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 18 alichukuliwa na Liverpool. Hadi leo amecheza mechi 695 na kufunga mabao 180 kwa klabu hiyo. Kuanzia mwaka 2001 alisakata kabumbu kwa timu ya taifa ya England. Kipaji chake cha ufungaji mabao kilianza kuonekana alipochangia ushindi wa England dhidi ya Ujerumani uliokuwa 5-1 chini ya kocha Sven- Goran Eriksson.

Aliishiriki katika mechi za kombe la dunia 2006, 2010 na 2014 akiwa nahodha mwaka 2010 (Afrika Kusini) na mwaka jana, Brazil ambapo England bahati mbaya walitolewa michuano ya mwanzo mwanzo. Kitwakimu mwanasoka Gerrard ameichezea nchi yake mara 114 na ni wa tatu katika idadi ya wachezaji waliolitumikia taifa hili kimpira chini ya golikipa Peter Shilton (1970-1990) na David Beckham (1996-2009).

Steven Gerrard
Steven Gerrard

Vile vile Gerrard ameshiriki katika ushindi wa Liverpool, moja ya klabu za zamani na maarufu za mpira duniani. Aliongoza ushindi wa vikombe viwili vya ligi ya FA ya England, vitatu vya Capital One, kimoja michuano ya klabu za Ulaya (UEFA), 2005. Liverpool ni kati ya timu zilizotwaa kombe hilo mara nyingi zaidi. Inayoongoza ni Real Madrid washindi mara kumi, ikifuatiwa na Milan ya Italia (7).Liverpool na Bayern Munich ya Ujerumani mara tano. Liverpool ilishinda miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005. Wababe wa Manchester United wako nyuma ya Liverpool kwa ushindi mara tatu. Kimsingi , Steven Gerrard penda usipende ni mshindi.

Jumamosi iliyopita wanahabari mbalimbali wa michezo waliandika kauli zao kuhusu umuhimu na taaluma yake Gerrard. Mchezaji mstaafu, Jammie Carragher, aliyekuwa naye wakati wa ushindi wa UEFA mwaka 2005 alisikitishwa na Liverpool kutompa Gerrard hadhi ya kutosha na kusababisha kuhama. Alidai iwapo Gerrard angehamia timu nyingine kama Chelsea au Real Madrid, kama alivyofanya Michael Owen angepatwa na matatizo waliyoyakumba ya kutocheza vizuri kutokana na hali tofauti. Alibaki nyumbani, Liverpool, bila tamaa ya fedha, Carragher aliandika. Mwanasafu, Martin Samuel wa Daily Mail alisema Gerrard ni mchezaji ambaye ukiwa naye ni katika timu ni tegemeo kubwa na unajua mambo yote yatakwenda sawa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

JE MAKOCHA NA FEDHA NDIYO TEGEMEO KUU LA USHINDI ?

FA Cup 4th round: