in

Je, Liverpool wanaweza kutetea taji la EPL?

KIPIGO cha mabao 7-2 walichopata mabingwa watetezi wa EPL,  Liverpool kimeshangaza wapenzi wa kandanda duniani. Mpaka  dakika 38 ya mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Villa Park,  mabingwa watetezi walikuwa wamechapwa mabao 4-1. 

Liverpool walipata kipigo hicho saa chache baada ya mabingwa  wa zamani Man United kuzabwa mabao 6-1. Vipigo hivyo  vimekuja wiki moja baada ya mabingwa wa zamani Leicester City  kuwazaba Man City kwa mabao 5-2 kwenye mfululizo wa Ligi Kuu  England.  

Takwimu zinaonesha kipigo cha Liverpool ni kikubwa kwa bingwa  mtetezi tangu mwaka 1953. Kikosi cha Jurgen Klopp bila shaka  hakikutegemea kukumbana na kipigo kikali cha namna hiyo, hasa  kutoka timu iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita. 

ATHARI ZA CORONA 

Uwanja Bila Mashabiki
Uwanja Bila Mashabiki

Inawezekana ikawa jambo la haraka kushuhudia vipigo hivyo,  lakini EPL imeanza msimu huu ikiwa katika mazingira ambayo  hayakuzoeleka kama ilivyokuwa misimu mingine.  

Timu zilikuwa na wiki za kujiandaa kwaajili ya msimu mpya  kuliko vipindi vya nyuma. Dirisha la usajili limefungwa Oktoba 5  mwaka huu. Soko la mauzo na manunuzi ya wachezaji limeathiri  msimu kwa ujumla wake kutokana na ugonjwa wa Corona. 

Liverpool kama zilivyo timu zingine imeathiriwa kimapato. Lakini  imefanikiwa kwuasajili Diogo Jota na Thiago Alcantara. Usajili wa  nyota hao ulikuja baada ya mchezo wa kwanza wa Ligi dhidi ya 

Leeds United. Kengele ya hatari ilishalia. Klopp alishasikia  kengele hiyo ndiyo maana haraka alimsjaili nyota huyo wa Bayern  Munich kama mbadala wa mbinu zinazoweza kutumia kwenye  mechi mbalimbali na kuibuka na ushindi.  

MIAKA 10 YA UJENZI 

Tanzania Sports
Virgil van Dijk

Baada ya miaka 10 ya kujenga upya klabu ya Liverpool, imevunja  mwiko uliodumu kwa miaka 30 ya kuishi bila kutwaa ubingwa wa  EPL. Makocha mbalimbali wamepita klabu hapo hapo, akina  Kenny Dalglish, Graham Souness, Brendan Rogers, Rafael Benitez  na wengineo. Lakini ni Jurgen Klopp pekee amefanikiwa  kuandika rekodi ya kipekee baada ya kutwaa mataji mawili ya  EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Chini ya umiliki wa John Henry, Liverpool imekuwa ikijaribu  kujitutumua, mara nyingi ilikosa ubingwa katika mazingira ya  kustajabisha. Klopp pekee amebdili masiaha ya mashabiki na  viongozi wa Liverpool na kuwafanya waamini inawezekana. Ndoto  za John Hnery zimekuja kutimia zaidi katika kipindi cha ukocha  wa Jurgen Klopp kwa sababu ndiye alileta soka la aina yake,  maarufu kama Gegen Pressing. Mjerumani huyo ametumia miaka  minne kujenga kikosi imara Liverpool na kuwaibua nyota wakali  wanaotisha katika soka la Ulaya, Mohammed Salah, Sadio Mane,  Roberto Firmino na nyota wengine kama Van Diyk, Fabinho,  Trent Alexander Arnold. Kwahiyo miaka 6 ya kukosa ubingwa  kwa mmiliki John Henry, na kumpa miaka minne Jurgen Klopp  kujenga Liverpool tishio si England pekee bali barani Ulaya ni  matunda ya kazi nzuri na uvumilivu wa hali ya juu. Si jambo  rahisi kwa wamiliki kukaa miaka 10 bila ubingwa au miaka minne  kumvumilia kocha mmoja.  

NDOTO ZA KUWASHIKA MAN UNITED

Tanzania Sports
Sura zilizotabasamu wiki iliyoisha

Kwenye kipindi cha miaka minne ya Jurgen Klopp ametwaa taji  moja la Ulaya na Ligi Kuu moja. Mataji mengine ni kama lile la  dunia pamoja na Super Cup.  

Kihistoria Man United wametwaa mataji 20 ya Ligi Kuu England  ikiwa ni moja mbele zaidi ya Liverpool. Kwa kipindi cha miaka 30  ambayo Liverpool walikuwa wamedorora, Man United walitawala  EPL.  

Nje ya hapo walimenyana na Chelsea na Arsenal kupigania  ubingwa wa EPL. Wakati Liverpool wana ndoto ya kutwaa taji la  20 la EPL, wenzao Man United wanahangaika ili kurudisha  makali yao, huku kocha wao Ole Gunnar Solskjaer akiwa  anaungwa mkono licha ya matokeo mbaya.  

Hapo ndipo ilipo changamoto ya Liverpool kama kweli wataweza  kukimbia mbio ndefu ya Ligi Kuu na kuweza kutwaa taji la 20,  ikiwa watakwepa vipigo kama walichokipata Villa Park.  

Majukumu hayo mawili ya kuwawafikia Man United ambao ndio  wapinzani wao wa jadi, pamoja na kutetea ubingwa ni mambo  ambao yanawapa uzito mkubwa. Wanahitaji utulivu ambao  utakifaya kikosi kifanye kazi yake kwa ufanisi zaidi.  

KILICHOTOKEA VILLA PARK 

EPL
EPL

Mchezo wa wikiendi kati ya Aston Volla na Liverpool umefungua  zaidi tatizo alilioona kocha wa Leeds United, Marcelo Bielsa  maarufu kama El Locco na mpira wake wa Bielsa Ball. Kwenye  mchezo wa ufunguzi Liverpool walisubiri hadi dakika za lala  salama kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Lakini namna timu  yao inavyocheza na mbinu mpya ya Klopp kutaka kucheza na  viungo zaidi bila mabeki wote wa kati ni jambo lingine  linalodhoofisha timu hiyo. 

Kwenye mchezo dhidi ya Astn Villa, Klopp alibanwa eneo la  kiungo. Kwenye mstari wa katikati ya uwanja palikuwa na viungo  watatu wa Astrin Villa ambao kazi yao ilikuw akupokonya mipira  na kucheza mashambulizi ya kushtukiza.  

Kwa vile kiungi wa ulinzialikuwa mmmoja, Fabinho ilikuwa rahisi  kumkwepa Nabil Keita na kumfanya Fabinho arudi nyuma zaidi.  hali ambayo ililazimu beki nambari nne Joe Gomez apande  kumsaidia Fabinho na kutengeneza pengo katio ya ulinzi na  kiungo.  

Villa walisambaratisha eneo la katikati ya Liverpool. Villa  hawakuwa na mpango wa kuwadhibiti mabeki wa Liverpool wa  pembeni ambao ni hatari, badala yake Ross Barkley na Grealish  walikuwa silaha ya kucheza mashambulizi ya kushtukiza.  

Hii ina maana Klopp ni lazima abadili mbinu kwa kuhakikisha  ene la kiungo wa ulinzi linakuwa na viungo wenye jukumu hilo  endapo anamkosa nyota mmoja wapo kati ya Mane,Firmino na  Salah.  

Villa hawakuwa na maajabu zaidi ya Counter Attacks. Hawakuwa  na skills za kuwayumbisha Liverpool isipokuwa ‘game plan’  ilikuwa kuwavuruga Liverpool kwa makosa yao ya kimbinu ndio  maana mabao mengi yamefungwa kutokana na makosa ya mabeki  ambao mara nyingi waligongwa mipira kabla ya kutua kimyani.  Je, bila kubaidli mbinu, Liveerpool wataweza kutetea ubingwa  wao? Hilo ndilo swali.  

Muda utaongea.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba vs Mtibwa

Azam, Yanga Na Simba Zatoa Onyo VPL

Watkins

Samatta,Watkins, majibu mwisho wa msimu..