in

Azam, Yanga Na Simba Zatoa Onyo VPL

Wiki ya vipigo ligi kuu Tanzania Bara imeendelea katika raundi ya tano kwa mara ya kwanza Yanga, Simba na Azam wakizalisha magoli 11.

Yanga

Wananchi wamecheza Jumamosi na kwa mara ya kwanza wamemchapa Coastal Union magoli 3-0, Metacha Mnata akiibuka na ‘Clean Sheets’ yake ya nne.

Baada ya hapo wamefanya sherehe ya kumfukuza kocha wao Zlatko Krmpotić hili walilijua kati ya viongozi na kocha mwenyewe.

Magoli matatu yana maana kubwa kwa timu hiyo ya Jangwani kwa kuongeza kujiamini.

Hadi sasa timu hiyo imefunga magoli 7 na kuruhusu goli moja na ndio timu pekee iliyopoteza magoli machache zaidi kuliko Azam na Simba.

Yanga wamejikusanyia alama 13 kwa michezo mitano kwani walitoa sare mchezo mmoja.

Azam FC

‘Wanarambaramba’ Azam FC wamejiongezea mataji na msimu huu patachimbika kweli katika kinyang’anyiro cha ubingwa ligi kuu Bara kwani tayari wamefanikiwa kukusanya alama 15 wamebutua mechi zote 5.

Azam FC wamefunga magoli 9 na wameruhusu  magoli 2 baada ya jana kuruhusu kuchanyatwa goli mbili katika ushindi wa magoli 4 dhidi ya Kagera Sugar.

David  Kisu ameruhusu magoli 2 sasa anabakia na zile ‘Clean Sheets’  nne kama Metacha Mnata.

Simba SC

Mnyama Simba anaendelea kupika biriani uwanjani kwani idadi ya magoli inaashiria kuwa ina safu nzuri ya ushambuliaji.

Hadi sasa timu hiyo imefunga magoli 14 na kufungwa magoli mawili.

Wafungaji bora wa wa timu hizi tatu ni Prince Dube ana magoli 5 akifuatiwa na Medie Kagere aliye na magoli 4 huku beki wa Yanga Lamine Moro akiwa na magoli mawili.

Jumla timu hizi zimefunga magoli 30 na zimefunga magoli 5, hivyo katika magoli 73 yaliyofungwa kwa raundi tano ikiwa bado mechi moja, wao peke yao wamechangia thelathini.

RAUNDI YA TANO

Katika raundi hii ya tano imeshavuka rekodi za raundi zote nne za nyuma. Kwani tayari zimedumbukiza magoli 19 ikisalia mechi moja.

Kama tulivyosema hapo awali magoli 73 yametiwa kambani kwa timu zote 18.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
cedric kaze

Kaze Kumrithi Zlatko

AV

Je, Liverpool wanaweza kutetea taji la EPL?