in

Hakuna Yanga Na Simba Safi Kwa Mkupuo !!!

Katika historia ya mpira wa miguu Tanzania hakujawahi kuwa na Yanga imara wakati huo Simba ikawa bora au Simba imara huku Yanga nayo ikawa bora.

Japo kwa wale wazee wa zamani watakwambia mwaka 1993 timu zote zilikuwa bora ila ukiangalia kwa msimu huo timu ipi imechukua ubingwa na kumfunga mwenzake utapata jibu.

Historia huwa haidanganyi tuanzie mwaka 2006 hadi 2017 kisha tunarudi nyuma tutaelewana tu.

2006-2017

Kuaniza mwaka 2006 hadi 2016 Yanga ilitawala sana miaka hiyo kwa watani wao wa jadi Simba unaweza ukahesabu pia mafanikio ambayo Yanga waliyapata kwa kipindi hiko.

Baada ya timu kuichukua  Yusuph Manji mwaka 2006 Yanga haijatetereka wala kuyumba.

Katika miaka 10 yanga ilichukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara 7 ikiwa Simba imechukua mara mbili mwaka 2009 ile bila ya kufungwa na ile ya 2012 huku 2013 akichukua Azam FC.

Sio rahisi kulielezea hili ila ile unga unga mwana kwa timu ya Simba ilionekana ilfika wakati ikawainua wachezaji wa kikosi ‘B’ kusaini mikataba ya timu kubwa.

Hawakuwa na hela timu ilichakaa sana ndicho kipindi ambacho Yanga inatawala na majina ya hovyo hovyo yalitoka kwa Simba.

Aliyekuwa Afisa Habari wa Yanga  wakati huo Jerry Muro aliwaita ‘Wamchangani’, ‘Watopeni wakati huo wakijiita wao wakimataifa kwakuwa wanacheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Nachokumbuka wakati Mohamed Dewj anarudi ilia pate nafasi aliwasaidia kumnunua mshambuliaji Laudit Mavugo pamoja na nyota wengine nakumbuka alitoa milioni mia moja pia katika usajili.

Hapo ndipo ikaanzaa taratibu kurudi hadi ilipofika katika mabadiliko.

Cha kusikitisha katika kipindi hiko ambacho Simba alikuwa mbovu ndicho Yanga walichokula goli 5-0, ndicho kipindi amabcho ya Yanga walirudishiwa sare ya magoli 3-3.

Tanzania Sports
Simba

Tofauti na Yanga mbovu ya mwaka 1977 ilifungwa magoli 6-0 na ‘Hat-trick’ ya kwanza kupatikana na Abdallah Kibadeni hadi leo haijafungwa tena.

1976-1977

Historia ya Yanga hii mwaka 1976 iliwafukuza wachezaji wake wengi nyota baada ya utovu wa nidhamu.

Baada ya kusuka kikosi kipya ndipo wakakutana na Simba bora mwaka huo na ikachapwa nyingi.

MSIMU WA 1989

Simba ilihitaji alama moja ili isalie katika ligi ilikuwa na michezo miwili, mmoja ikapoteza na mchezo wa mwisho ulikuwa dhihi ya Yanga ambapo timu ya Wananchi ilidanja kwa kukubali kichapo cha maagoli 2-1.

Watu wa Yanga wanasema aliyekuwa golikipa wa timu hiyo kipindi hiko Sahau Kambi aliibeba Simba kwa kuacha wafungwe goli la pili.

MSIMU WA 1989

Kuna msimamo wa ligi unaendelea katika mitandao ya kijamii au hata uki-‘Google’ msimamo wa ligi kuu Bara mwaka 1989 utapata kuona kuwa mchezo wa mwisho Yanga alitakiwa acheze na Simba.

Wakati huo huo Simba inatakiwa ishinde ili ijinusuru kushuka daraja.

TUUCHAMBUE KWA UNDANI MSIMU HUU WA 1989

Mwaka 1989 ulikuwa mgumu kwa timu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na hata kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) na hata ile ya Tanzania Bara, ambayo ilishiriki kwenye michuano ya Kombe la Chalenji.

Matokeo ya ajabu zaidi yalikuwa klabu ya Simba, ambayo ilijikuta ikinusurika kuteremka daraja mwaka huo, lakini kikubwa zaidi ni kule kushangazwa na ubora wa timu ya wajenzi ya Mecco kutoka Mbeya, ambayo mwaka huo ilikuwa imepanda daraja la kwanza.

Mecco ambayo ilikuwa inaundwa na wachezaji kama Epharaim Kayeta, Nassib Abbas, Betwell Africa, Abeid Kasabalala, Rashid Mandanje, Danford Ngesi, Charles Makwaza na wengineo, ilifanikiwa kuwabana mbavu Simba chini ya kocha Mohammed Hussein Hassan ‘Msomali’ ikiwa na wachezaji Moses Mkamdawire, Juma Shamte (alitokea Tukuyu), Omari Hussein ‘Kakakuona’ (alitokea Maji Maji), Dan Muhoja, Michael Kidilu, John Mkelele, Edward Chumila, Raphael Paul, Ramadhani Lenny, Adam Selemani (alitokea Reli), Malota Soma, Adolf Kondo, Sunday Juma, Aston Pardon, Twaha Hamidu, Iddi Selemani (alitokea Sifa United ya Manzese), Abubakar Kombo, Augustine Haule, Rashid Salum ‘Killer’ (alitokea Ndovu SC), Niva Mtawa, Suleiman Mathew Luwongo (alitokea kwa watani wao Yanga), Clement Kazamala, Daniel Manembe, Juma Limonga (alitokea Reli) na Ally Machella (kutoa Temeke Rangers).

Mechi ya kwanza baina ya Simba na MECCO ilifanyika jijini Dar es Salaam Februari 25, 1989 ambapo Simba ilibanwa mbavu na kuambulia suluhu mbele ya vijana hao waliokuwa wakitandaza boli kwa kiwango kikubwa.

Walau Simba ilikuwa imefuta aibu ya vigogo kuumbuliwa na timu hiyo, kwani tayari MECCO, katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo iliyoanza Desemba 31, 1988, ilikuwa imeichapa Yanga bao 1-0 ambalo lilipachikwa wavuni na Ephraem Kayeta kwenye Uwanja wa Sokoine.

Hata hivyo, Simba haikujua kwamba vijana hao walikuwa imara, na walipokutana katika mechi ya marudiano Juni 24, 1989, wakachezea kichapo cha mabao 3-2! Haya yalikuwa maajabu ya mwaka na ndiyo matokeo yaliyozidi kulididimiza jahazi la Simba mpaka ikanusurika kuteremka daraja. Zilizoshuka mwaka huo ni RTC Kigoma na Kurugenzi Dodoma.

Wenzao Yanga walifanikiwa kulipa kisasi kwa Mecco baada ya kushinda mabao 2-1 katika mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Taifa Julai 26, 1989.

2017-2020

Simba imetawala ligi kwa kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo kama ilivyofanya Yanga msimu wa 2014 hadi 2017.

Lakini Simba imeimarika zaidi na kuitesa Yanga tangu mwaka 2015 katika ligi Yanga imepata ushindi mara moja huku vikombe vyote Simba wakivimiliki.

Mara Pap! 2019-2020 GSM HAO

Hapa sasa ndipo palipokuwa na utamu hadi sasa kila timu inaonekana kujitutumua na kuchagua wachezaj walio na viwango vya juu nani atakubali kuanguka ili ile dhana ya hakuna Yanga bora na Simba bora kwa msimu mmoja ?

 Wewe unaonaje nani kati ya timu hizi mbili atakaye anguka au watafanya vizuri wote na kuondoa mazoea ?

Mara zote inapokuwa timu moja iko vizuri kiuongozi na wachezaji timu nyingine inakuwa dhaifu kila idara.

Matukio makubwa ya timu hizi ni yale yaliyokuwa yanagawa makundi mawili.

Yanga walikuwa na kundi linaitwa Yanga Asili na Yanga kampuni unaikumbuka hii hadi bakora zinasafirishwa katika ‘pickup’ .

Simba nao walikuwa na jambo lao kwa upande wao walikuwa na Simba ya viongozi fulani na Simba ukawa.

Kwa miaka yote hiyo kulipokuwa kuna msuguano basi mafanikio hukimbia mbali sana.

UTOFAUTI WA YANGA NA SIMBA

Wakati Yanga inapokuwa na migogoro ikiingia uwanjani wanafanya kazi kweli , ile migogoro haiwasumbui sana tofuati na Simba kukitokea mpasuko basi unaathiri hadi wachezaji.

Hayo sio maneno yangu aliwahi kukiri Afisa habari wa Simba Haji Manara juu ya tatizo linapotokea katika timu.

Swali linarudi pale pale kuwa msimu huu timu ipi itaamua kunyoosha mikono juu bundi la migogoro likiendelea kuitafuna au zote zitasimama na kutonesha soka safi lenye mvuto.

Toa maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii utueleze juu ya maoni yako.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

69 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba vs Yanga

Yanga ‘Unbeaten’, Simba ‘Pira’ biriani

Edersson

Je, ni wakati wa makipa kutoka Brazil kutamba Ulaya?