in

EPL vita kubwa

Aston Villa

*Liver, Man City wameshafuzu kwa UCL

*Mchuano Chelsea, Leicester na Man U

*Norwich kwaheri, Villa mguu ndani, nje

Ligi Kuu ya England (EPL) inakaribia ukingoni, huku vita ikiwa kubwa kufuzu kwa mashindano ya Ulaya pamoja na kukwepa kushuka daraja.

Ligi hii maarufu zaidi duniani imerejea huku washabiki wakiwa hawaruhusiwi, na kuna timu zilizojihakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) – mabingwa wapya Liverpool wenye alama 93 na Manchester City waliovuliwa ubingwa, wakiwa na alama 75. Kocha Pep Guardiola alieleza furaha yake kwa kuondoshwa kwa marufuku dhidi yao ya kucheza UCL kwa misimu miwili.

Mechi hazinogi tena kivile, kwani washabiki wanatazama kwenye televisheni kama kinga dhidi ya virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, maarufu kama Covid-19 vilivyosababisha mechi kusitishwa Machi mwaka huu.

Liverpool walikuwa kwa kiasi kikubwa wamejiweka pazuri kutwaa ubingwa, kwani waliwaacha wapinzani wao wakubwa mbali, wakichanga karata zao vyema mapema, wakienda bila kupoteza mechi hadi walipokuja kuadhiriwa na Watford, Manchester City na Arsenal.

Vijana hao wa Jurgen Klopp wamefanikiwa kufanya vyema kwa ujumla nyumbani, japokuwa walivuliwa ubingwa wa Ulaya walioupata mwaka jana kwa kuwafunga Tottenham Hotspur kwenye fainali iliyofanyika jijini Madrid, Hispania.

Chelsea, Leicester na Manchester United zinapigania kuhakikisha zinakuwa kati ya zile nne bora zitakazocheza kwenye UCL msimu ujao. Alama zao ni 63, 62 na 62 mtawalia. Wamepigana na zikiwa zimebaki mechi mbili, inaelekea wanne bora watakuwa miongoni mwa hao, japokuwa miujiza ikitokea labda Wolverhampton wakapita.

Ama kwa vita ya kucheza Ligi ya Europa, ukiondoa Liverpool, hao wengine wanaingizwa humo pamoja na Spurs, Sheffield United, Arsenal na Burnley japokuwa hawa wa mwisho uwezekano wa kupenya ni mdogo. Alama zao ni 55, 54,53 na 51 mtawalia.

Matokeo ya Alhamisi ya jana na siku moja kabla yake yaliweka picha tofauti kidogo, ambapo Everton walikwenda sare ya 1-1 na Aston Villa, Leicester wakiwapiga Sheffield 2-0, Crystal Palace wakapoteza 0-2 kwa Manchester United wakati Southampton walikwenda sare ya 1-1 na Brighton.

Katika mechi za Jumatano Arsenal waliwafyatua Liverpool 2-1, Spurs wakawakandika Newcastle 3-1, Man City wakawashinda Bournemouth kwa mabao 2-1 huku Burnley na Wolves wakienda sare ya 1-1.

Hali ikiwa hivyo huko juu, kule chini tayari Norwich tayari wameaga EPL na msimu ujao watakuwa wakicheza kwenye Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championships, baada ya kuboronga kwa kupoteza mechi nyingi, hadi hivi karibuni wameendelea kuachia mabao tu.

Aston Villa ambao Mtanzania wa kwanza kucheza EPL – Mbwana Samatta yumo wapo mguu mmoja nje na mwingine ndani, uwezekano mkubwa zaidi ukiwa ni kushuka daraja. Wakati Norwich wala alama 21 tu, Villa wanazo 31 sawa na Bournemouth na huenda watatu hao wakaaga.

Hata hivyo, bado kuna uwezekano wa Watford na West Ham wakashuka ikiwa hao wawili wa chini watafanikiwa ‘kupindua meza’, kwani hawa wana alama 34 kila mmoja. Brighton nao wanachungulia shimo na alama zao 37 lakini kimantiki uwezekan mkubwa zaidi ni wa kubaki EPL.

Kila kocha anaangalia kikosi chake kinaweza kujiokotea alama ngapo kwenye mechi mbili zilizobaki kabla ya pazia la msimu kushushwa rasmi kupisha mapumziko, usajili na maandalizi ya msimu mpya. Haitarajiwi kwamba kutakuwapo na usajili wa fedha nyingi, kwani klabu zipo kwenye wakati mgumu kiuchumi kutokana na

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mtibwa

Mtibwa Sugar yaifanya ngazi Azam FC

Zinedine Zidane

Real Madrid Mabingwa