in

Mtibwa Sugar yaifanya ngazi Azam FC

Mtibwa

Timu ya Mtibwa Sugar inaendelea kujinasua kushuka daraja  baada ya jana kuitandika Azam FC goli 1-0 mchezo uliofanyika Gairo mkoani Morogoro.

Goli la ushindi la Mtibwa Sugar limefungwa na Issa Rashid ambaye alipiga kona iliyoingia moja kwa moja nyavuni dakika ya 38 ya mchezo huo.

Kwa ushindi huo sasa unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe  alama 41 ikipanda hadi nafasi ya 13 iliyokuwa inashikiliwa na Lipuli yenye alama 40.

Mtibwa inalingana alama na Alliance ambayo imetoa sare ya  goli 1-1 dhidi ya JKT Tanzania ikiwa na utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa.

Matokeo mengine ya michezo ya jana ni pamoja na Namungo kuichakaza Mbeya City goli 1-0, Kagera Sugar 1 Coastal Union 0 na Ndanda FC 2 Tanzania Prisons 1.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Morrison

Ipo nafasi ya Morrison Simba?

Aston Villa

EPL vita kubwa