in , , ,

Chelsea hawakamatiki

*Man United waanza kung’ara

Wakati Chelsea wanashikilia rekodi ya kutopoteza mchezo, Manchester United wameanza kukaa vizuri kwa kupata ushindi wikiendi hii.

Chelsea waliwafunga Arsenal 2-0 licha ya Arsenal kutawala mchezo kwa asilimia 53 na kocha Jose Mourinho kukiri kwamba The Gunners waliwapa tabu. Walipata bao la kwanza dakika ya 27 kwa penati ya Eden Hazard baada ya Laurent Koscielny kumwangusha.

Diego Costa ambaye Arsene Wenger wa Arsenal alikiri kuwa ni mzuri na sawa na muuaji, aliwaua kwa bao la dakika ya 78 na kukata kiu ya washabiki waliojazana uwanjani. Chelsea walipata pigo kwa kipa wao namba moja, Thibaut Courtois kupelekwa hospitali baada ya kuumia kichwa walipogongana na Alexis Sanchez.

 Kipa namba mbili, Petr Cech itakumbukwa kwamba alipata maumivu makubwa ya kichwa kitambo, na hadi leo hucheza akiwa amevaa ngao.

Makocha Mourinho na Wenger walibwatukiana katika mzozo mkubwa kwenye eneo lao la ufundi, ikabidi mwamuzi wa akiba, Jon Moss kuwatenganisha. Wamekuwa na uhasama mkubwa kwa muda mrefu na Wenger hajapata kumfunga Mourinho katika mechi 12 zilizopita.

Katika mechi ya awali Jumapili hii, Manchester United walifanikiwa kuibuka an ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton kwa mabao ya Angel Di Maria na Radamel Falcao. United wametinga katika nne bora kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwaka.

Steven Naismith alifunga bao na nusura Everton wasawazishe dakika za lala salama kupitia kwa Bryan Oviedo aliyewafunga msimu uliopita, kama si uimara wa kipa David De Gea. Everton hawapo vyema msimu huu, kwani wameshinda mechi moja tu kati ya saba walizocheza.

Mchezaji John Stones wa Everton na Timu ya Taifa ya England aliumia goti na hivyo kuondolewa kwenye kikosi cha taifa, na nafasi yake itachukuliwa na Calum Chambers wa Arsenal. Katika mechi nyingine, Tottenham waliwafunga Southampton 1-0 na West Ham wakawashinda Queen Park Rangers 2-0.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man City safi, Liverpool waamka

Di Matteo kocha mpya Schalke