in , , ,

Arteta anahitaji mabao 40 ya wawili wa Arsenal

Nyota huyu kutoka Chelsea ana umri wa miaka 24 tu, pamoja na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya…

Ukiangalia orodha ya wafungaji bora wa EPL msimu ulioisha inaonekana wazi safu ya ushambuliaji ya Arsenal imeachwa mbali sana. Vita yake ya ubingwa dhidi ya Manchester City ingekwama katika idadi ya mabao ya kufunga. Man City walikuwa wamefunga mabao mengi na haikuwa ajabu kuwaona wanafunga 5 kwa mechi moja. 

Safu ya ushambuliaji ya Man City ilikuwa Ina wazimu wa kupachika mabao mengi. Hakika ilikuwa Vita tamu na ya kupendeza katika ushindani wa kandanda EPL. 

Mikel Arteta bila shaka aliumizwa na tofauti ya mabao ya kufunga. Hili linaonesha namna anavyoandaa timu yake kwa msimj ujao. Hadi hapo inadhihrika kuwa Arteta licha ya kuirudisha Arsenal katika Ligi ya Mabingwa ameona mahitaji makubwa ya kuboresha idara ya ushambuliaji. 

MABAO 40

Kwanza Arsenal imerudi Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa juhudi ya washambuliaji waliopo kikosini. Lakini ili aweze kudumisha na kuibuka bingwa wa EPL lazima awe na uhakika wa kupachika mabao 40. Katika safu yake, Gabriel Jesus anatakiwa kupachika mabao 20 msimu ujao kama njia ya kuweka hai matumaini ya Arsenal kufanya mambo makubwa zaidi na yenye ushindani. Msimu ulioisha Arteta alitegemea huduma ya Gabriel Jesus, Eddie Nketiah, Martin Odegaard na Nelson. Hata hivyo safu hiyo imepata ingizo jipya; Kai Havertz. Nyota huyu kutoka Chelsea ana umri wa miaka 24 tu, pamoja na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Mabao 40 ya Arsenal ni kwa ajili ya EPL ili kujihakikishia nafasi za juu msimu ujao. 

VIBARUA VIWILI

Mshambuliaji mpya wa Arsenal Kai Havertz atakuwa na vibarua viwili kwa wakati mmoja. Kwanza kuhakikisha anampa mabao 20 Mikel Arteta katika EPL. Kisha kibarua Cha pili kitakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako uzoefu wake unahitajika ili kuimarisha ubora wa kikosi cha Arsenal.

SUPER SUB 

Mikel Arteta anatakiwa kuandaa wachezaji wa akiba wenye ubora na ambao wataipa nguvu timu yake. Hivyo basi katika kikosi Cha Arsenal kwa sasa ingizo la Kai Havertz linakuwa na manufaa zaidi lakini nalo linahitaji kupewa nguvu za ziada. Ikiwa washambuliaji wote watakwama kimbinu au kuwa na siku mbaya kazini maana yake atahitaji mwingine wa kuua mechi mbalimbali. Huyu atakuwa ‘super sub’, kwahiyo bado Arsenal inapaswa kupngeza nguvu kikosini mwake ili iweze kushindana zaidi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

73 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kwanini Ilkay Gündogan amechagua Barcelona?

Tanzania Sports

Liverpool watimua mastaa wao