in

Liverpool watimua mastaa wao

HAKIKA msimu ujao utakuwa na kukata na shoka. Kila timu inasajili nyota wa kuongeza nguvu huku wengine wakitupiwa virago wakiwemo Nyota wa Liverpool. 

Kabla ya Liverpool imethibitisha kuwatimua mastaa ambao hawatakuwa sehemu ya timu msimu wa 2023/2024, huku ukionesha wazi viwango vyao vimeshuka pamoja na hasira za kufanya vibaya kwa klabu hiyo msimu ulioisha ni Sababu zinazowaondoa mastaa hao. 

Liverpool wamemtangaza kuondoka kwa wachezaji 11 katika kikosi chao cha kwanza wakiwa wachezaji huru. Ni Kama vile Liverpool wametimua Nyota hao kwani wangeweza kuwaongezea mikataba ya kuendelea kukipiga katika dimba la Anfield. 

Wachezaji walioondolewa ni pamoja na kiungo mkongwe, mshambuliaji wa Brazil na nyota wa zamani wa Arsenal. Uamuzi wa kuwatupia virago wachezaji hao ni kukabiliana na Sera mpya ya usajili ambayo inalenga kujenga timu mpya Liverpool na ambayo itakuwa na mafanikio makubwa kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita. 

Majina manne makubwa ya Nyota wanaoondoka ni pamoja na mkongwe wa England.

Jurgen Klopp inaonekana amepania kuunda timu mpya baada ha kumaliza msimu wakiwa nafasi ya tano na msimu ujao watakosa kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hasira za kukosa kushiriki UEFA msimu ujao zimeleta matunda baada ha kukamilika dili la usajili wa kiungo mshambuliaji Alexis Mac Allister ambaye anajiunga Liverpool akitokea Brighton kwa ada ya pauni  Milioni 35.

Kundi la wachezaji wanaoondoka ni wale ambao waliaminika mbele ya Klopp na kuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa UEFA mwaka 2019, lakini sasa wanalazimika kuondoka klabuni kupisha mwelekeo mpya.

JAMES MILNER anaondoka klabuni hapo akiwa ni kiungo aliyecheza mechi 857 katika maisha yake ya soka

ROBERTO FIRMINO

Ni nyota mwingine aliyeng’ara Liverpool yangu alipojiunga akitokea klabu ya  Hoffenheim ya Ujerumani mnamo mwaka 2015. Akiwa Liverpool, Firmino ametwaa mataji 7. 

ORODHA KAMILI

Roberto Firmino, Naby Keita, James Milner, Roberto Firmir Naby Keita, Alex Oxlade-Chamberlain.

Tanzania Sports

Nyota wengine kutoka Akademi yao ambao wanaaondoka ni Jack Bearne, Liam Hughes, Charlie Hayes-Green, Oscar Kelly, Fidel O’Rourke, Oludare Olunfunwa, Iwan Roberts.

Reply to allReplyForward

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Arteta anahitaji mabao 40 ya wawili wa Arsenal

Tanzania Sports

KIVULI CHA ARSENE WENGER KINAVYOIONGOZA ARSENAL