in

Yanga yanasa mmoja, Morrison bado..

Usajili wa Yanga

Timu ya Yanga imeinasa saini ya mchezaji Yacouba Sogne nyota kutoka Medeama FC  ya nchini Ghana.

Sogne anatarajiwa kutua nchini siku ya jumatatu wiki ijayo ili kuungana na Yanga ambayo imeanza mazoezi kwa ajiri ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi utakao anza Septemba 6 mwaka huu.

Yacouba ni mshambuliaji ambapo takwimu zake za ufungaji wa mabao  hazionekani kwa maana ya ugumu wa takwimu kwa bara la Afrika ila ni raia wa Burkina Faso na ana miaka 28.

Mwinyi Zahera ajiunga na Gwambina FC

Tanzania Sports
zahera

Aliyekuwa kocha wa  Yanga Mwinyi Zahera  ametambulishwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu huu wa 2019/20 na itashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/21.

Zahera aliwahi kuifundisha Yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungaishiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa.

Kocha huyo amesaini dili la miaka mitano na inaelezwa kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga.

Wanaotajwa kuibukia Gwambina ni pamoja na Mrisho Ngasa na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru

Feisal Salum ‘Fei Toto’

Feisal Salum kiungo wa Yanga kwa mujibu wa Injinia Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu hiyo amesema kuwa ameongeza mkataba wa miaka mitatu.

Kwa maana hiyo Feisal atakuwa ni mali ya Yanga mpaka 2024 kwa timu itakayokuwa inasaka saini yake lazima ijipange kuweka mkwanja mezani.

Kwa msimu wa 2019/20, Feisal amekuwa bora ndani ya Ligi Kuu Bara akianza kikosi cha Kwanza kwenye jumla ya mechi 22.

Amefunga bao moja ndani ya ligi msimu huu ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Mwadui FC kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Salum Aboubakar ‘Sure Boy’

Timu ya Azam FC imefunga mjadala na Yanga juu ya usajili wa nyota wao Salum Aboubakar ambapo kwa sasa nyota huyo atabaki klabuni hapo.

‘Sure boy’ alitakiwa na Yanga na yeye kaandi kabarua ya kutaka changamoto mpya lakini mabosi wa Azam walitaka dau kubwa na kubadilishana na na mcheza ambapo Yanga waligoma.

Patrick Aussems

Timu ya Yanga inahusisha na kutaka kumrejesha nchini aliyekuwa kocha wa Simba Patrick Aussems ambapo imearifiwa kuwa mazungunzo yamemalizika.

Kocha huyo muda wowote atatua nchini.

Benard Morrison

Sakata la mkataba wa Benard Morrison bado hajilateguliwa kwani TFF na bodi yake bado hawaja litolea ufafanuzi.

Hivyo bado hawajaweka sawa na kutoa maamuzi sahihi kuwa nyota huyo aende timu gani.

Chama hauzwi

Uongozi  wa Simba umesema kuwa suala la mchezaji wao Clatous Chama kutajwa kujiunga na watani zao wa jadi Yanga hazina ukweli.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa baada ya Yanga kumvuta ndani ya Yaga Senzo Mbatha aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba imeanza hesabu za kumvuta ndani ya kikosi kiungo wao bora, Chama.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwa kuwa ina mkataba naye na ina malengo.

“Chama ana mkataba na Simba hadi Julai 2021, Simba haiwezi kumuuza au kumuachia mchezaji ambae tuna malengo nae.

“Najua viongozi wao wanataka kuwaongopea watu wao ili kutoa droo na issue ya Morrison,” amesema.

Clatous Chama amesema kuwa masuala ya mitandao hayana ukweli yeye bado ana mkataba na timu yake ya Simba.

Papy Tshishimbi kutua Simba

Taarifa zinasema kuwa aliyekuwa kapteni wa Yanga Papy Tshishimbi atajiunga na Simba wakati wowote kuanzia sasa.

Tshishimbi aliachana na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.

Farid Mussa muda wowoteYanga

Yanga iko kwenye mazungumzo mazuri na mchezaji wa zamani wa Azam na CD Tenerife ya Hispania, Farid Mussa ili kukamilisha dili la usajili unaotarajiwa kutangazwa muda wowote baada ya mchezaji huyo kumwaga wino.

Chanzo cha kuaminika ndani ya Yanga kilisema kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri na kilichobaki kwa sasa ni suala la muda tu ili kuona kama wataweza kufi kia makubaliano au la.

“Ni kweli upo mpango wa kumsajili Farid Mussa kama sehemu ya kuimarisha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao na tayari uongozi unaendelea na mazungumzo na mchezaji husika.

“Hivyo kama pande zote zitaafikiana basi ishu ya Farid kuvaa uzi wa Yanga kwa msimu ujao itabaki kuwa suala la muda tu,” kilisema chanzo hicho.

Farid ambaye alikiri kuhitajika na baadhi ya klabu lakini kuhusu wapi atasaini, alisema kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni.

 “Ni mapema sana kusema ni wapi nitaelekea lakini mambo yakiwa sawa basi kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Farid

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Senzo

Siku moja ya Morrison yamuondoa Senzo

Senzo

Yanga Walimnyatia Senzo Kitambo