in , ,

Yanga wanadanganya kuhusu Kagoma

Baada ya Yanga jana kupitia mwanasheria wao Simon Patrick kutoa tamko la klabu ya Yanga kuhusiana na sakata lao dhidi ya mchezaji Yusuph Kagoma. Leo hii Tanzania Sports imemtafuta mkuu wa idara ya habari ya Singida Fountain Issah Liponda  kutoa msimamo wao kama klabu

Issah Liponda amedai kuwa klabu ya Yanga ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuonesha nia ya kumsajili Yusuph Kagoma ambaye kimsingi alikuwa na mkataba na Singida Fountain Gate.

Vongozi wa pande zote mbili yani Singida Fountain Gate na Yanga walifikia makubaliano ya kuuziana Yusuph Magoma kwa ada ya uhamisho wa milioni 30.

Kwenye ada hii ya uhamisho ilitakiwa kulipwa kwa awamu mbili kila awamu ni milioni 15 ambapo awamu ya kwanza ilitakiwa kulipwa tarehe 27 mwezi wa tatu na awamu ya mwisho ilitakiwa kulipwa tarehe 30 mwezi wa 4 2024

Mpaka kufika mwezi wa saba Yanga walikuwa hawajakamilisha malipo ya usajili wa Yusuph Kagoma ambapo walikuwa wamelipa awamu moja tu ambayo ni milioni 15.

Kimsingi Yanga na Singida Fountain Gate walitakiwa kufanya biashara ya wachezaji watatu msimu huu ambao ni Nickson Kibabage, Yusuph Kagoma na Aziz Andambwile.

Yanga walianza kuingiza fedha  za mchezaji Nickson Kibabage kama fedha za uhamisho kwa wakati, lakini fedha za uhamisho wa Yusuph Kagoma zilichewa kuingia kwa wakati.

Ikumbukwe makubaliano yalikuwa Yanga kuingiza fedha zote za uhamisho mwishoni mwa mwezi wa nne. Baada ya kuchelewa kuingiza fedha, klabu ya Singida Fountain Gate iliwakumbusha Yanga kuhusu kukiuka makubaliano ya kimkataba.

Ambapo Singida Fountain Gate waliwatumia Yanga barua ya kuwakumbusha tarehe 7 mwezi 6.Bada ya Yanga kukumbushwa waliingiza fedha tarehe 8 mwezi 6. Fedha hizo ziliingizwa muda ambao ulikuwa kinyume na makubaliano ya kimkataba.

Kwa mantiki hiyo Yanga walivunja mkataba wao wenyewe kwa kutotimiza masharti ya kimkataba kwa kutolipa fedha ya usajili kwa wakati. Hivo Singida Fountain Gate iliamua kufanya biashara na Simba baada ya Yanga kuvunja mkataba.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yusuph Kagoma ni mali halali ya Yanga

Tanzania Sports

Tunatamani Yanga iwe “Man City”