Timu ya Yanga imetangaza majina 14 ya wachezaji walioachwa huku ikishuhudia ikimbakisha winga msumbufu Benard Morrison.
Wachezaji ambao wameachwa huru na mikataba yao kuisha ni pamoja na David Molinga, Mrisho Ngassa, Papy Tshishimbi, Jaffar Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vicent, na Issa Banka.
Wachezaji ambao mikataba yao bado iko na atimu inazungunza nayo ni pamoja na Ali Mtoni, Muharami Issa, Ali Ali, Yikpe Gislain, Patrick Sibomana, Eric Kabamba na Rafael Daud.
Wachezaji ambao wanabaki na kuendelea na kuitumikia timu ya Wananchi ni pamoja na Farouk Shikalo, Ramdhani Kabwili, Metacha Mnata, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyun Saleh, Said Makapu, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Abdullaziz Makame, Benard Morrison na Paul Godfrey.
Yanga inaendelea na mazungunzo na baadhi ya wachezaji ili wabaki ndani ya timu hiyo ni pamoja na Juma Abdul, Kelvin Yondani ambao mikataba yao imeisha na timu inataka kuendelea nayo.
Timu hiyo imesha sajili wachezji wanne ikiwemo beki Bakari Nondo, Yassin Mustapha, Wazir Junior na Zawadi Mauya.
Wachezaji wanaotazamiwa kuingia wakati wowote ni pamoja na Tunombe, Tuisilaa Kisinda na Jesse Were.
Comments
Loading…