in

VPL: Takwimu Za Yanga, Simba Na Azam Noma!

Yanga Simba

Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea yakishuhudiwa mengi makubwa na takwimu mbalimbali zikiendelea kuzungunzwa tayari mechi nane zimepigwa  katika mzunguko wa pili.

Katika zile timu tatu kubwa Tanzania Simba imeambulia alama moja baadaya kutoa sareya kufungana goli 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Yanga ambayo bado haina muunganiko mzuri kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja,  ameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mbeya City huku  Azam FC  nayo ikitoka kifua mbele kwa kuitandika Coastal Union  magoli 2-0.

Takwimu zao hawa miamba watatu , Simba ina magoli matatu mchezo wa kwanza imeshinda magoli 2-1 dhidi ya Ihefu FC  magoli yote yamefungwa kipindi cha kwanza na John Bocco pamoja na Mzamiru Yassin.

Mechi ya mzunguko wa pili imepata goli moja lililofungwa na Mzamiru Yassini kipindi cha kwanza.

Ichukue hii Simba imepata magoli 3 katika raundi ya kwanza naya pili kipindi cha kwanza.

Hadi sasa Mzamiru Yassin anaongoza kwa ufungaji wa magoli Simba akiweka magoli 2.

Kwa upande wa Wananchi  katika raundi mbili wamepata magoli mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na cha pili.

Wafungaji wa Yanga ni Michael Sarpong dakika ya 19 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons na mchezo wa raundi ya pili goli la kichwa la Lamine Moro akiipa ushindi wa kwanza timu hiyo kwa kufunga dakika ya 86 dhidi ya Mbeya City.

Azam FC imefunga magoli 3 katika raundi mbili, ile ya kwanza imepata goli moja lililofungwa na Obrey Chirwa dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo wa pili imepata magoli mawili yaliyofungwa na Princes Dube dhidi ya Coastal Union.

Wakati hayo ya majemedari watatu wakiendelea kufanya makubwa katika hatua raundi mbili za ligi hizi zifuatazo za wote.

Katika raundi ya kwanza magoli 14 yalifungwa kwa mechi zote za ligi mzunguko wa kwanza.

RAUNDI YA PILI

Katika hatua ya pili ya ligi kwa maana ya mzunguko wa pili hadi muda huu mechi nane zimepigwa na magoli 12 yamefungwa ikisalia mchezo mmoja ambao unachezwa leo.

Katika hatua hii kipindi cha kwanza yamefungwa magoli 8 kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili yakifungwa 4, ukijumlisha vizuri unapata 12 ikiwa umesalia mchezo mmoja kukamilisha raundi ya pili.

Prince Dube yeye amefunga  magoli 2 katika mechi moja hakuna mwingine aliyefanya hivyo kwa mzunguko wa kwanza hadi kufikia mechi nane kabla ya mechi moja iliyobaki.

Nyota wa Ihefu FC,  Enock Jiah anashikilia rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi akimpiku Lambert Sabiyanka kwa aliyefunga goli dakika 8 dhidi ya Yanga, Jiah yeye metumbukiza katika nyavu dhidi ya Ruvu Shooting dakika ya 7 ya mchezo huo na ndio goli la ushindi.

Rekodi hii inaangaliwa kabla ya mchezo wa mwisho Namungo dhidi ya Polisi Tanzania.

Swali ni kwamba kweli watafikisha magoli 14 au kuzidi katika mchezo mmoja uliosalia ili ipite rekodi ya raundi ya kwanza.

Baada ya kuona yote hayo katika raundi ya kwanza na ile ya pili ambayo bado mchezo mmoja yamefungwa magoli 22.

Chukua hii kipindi cha kwanza raundi ya kwanza yamefungwa kipindi cha kwanza yamefungwa magoli 9 na cha pili yalifungwa 5, huku raundi ya pili kipindi cha kwanza yamefungwa 4 na cha pili yamefungwa 8.

Jumla kipindi cha kwanza yamefungwa magoli 13 huku kipindi cha pili yamefungwa magoli .

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga Na Simba Hazichezi Ugenini

TFF

Bodi Ya Ligi Na TFF Lawama Nyingi!