in

‘Uenyeji’ wa mashindano ya CAF ni heshima Tanzania

Benjamin Mkapa Stadium Dar

Shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF limetangaza kuwa timu ya CR Belouizdad ya Algeria itatumia uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam kwa ajili ya mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya kigogo Mamlelodi Sundowns ya Afrika kusini.

Mchezo huo wa hatua ya makundi utachezwa Februari 28 mwaka huu kuanzia saa 12  kamili jioni. CR Belouizdad iliwasilisha ombi hilo kwa Shirikisho la soka TFF ikitaka kucheza mechi yao hapa nchini. Nao TFF walikubali ombi hilo baada ya kushauriana na serikali ili kupitisha maombi hayo.

Kimsingi timu ya nchi fulani kutumia viwanja vya nchi nyingine kama kiwanja cha nyumbani ni jambo la kawaida katika sekta ya michezo. Ni jambo la kufurahia nchi yako kuongeza watalii wa michezo. Hii inanikumbusha mechi kati ya Liverpool na Leipzig ilichezwa katika uwanja wa kigeni.

Inafahamika kuwa serikali ya Algeria imekataza raia kutoka Afrika kusini kuingia nchini humo, kwahiyo chama soka cha Algeria kimefuata masharti ya serikali yao na kuichagua Tanzania kuwa sehemu mwafaka kwao kucheza mechi yao. Tofauti ya Algeria na Tanzania ni kwamba sisi tunaruhusu raia wa nchi zote kuingia na kutoka.

Tanzania Sports
CR Belouizdad

Ujio wa Algeria unatukumbusha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Ahmed Ben Bella, aliyepigania uhuru. Wajukuu wa Algeria Ahmed Ben Bella kuomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wao wa makundi dhidi wageni wao Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini ni hatua ambayo inaipa uenyeji Tanzania na kutangaza pamoja na kujijenga kimichezo kimataifa.

Maombi ya Algeria yamenikumbusha juu ya uamuzi wa shirikisho la Soka Afrika CAF juu ya mechi mbili za raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya klabu ya Namungo na Al Hilal ya Sudan kusini.

CAF ilitangaza uamuzi kuwa mchezo wao uchezwe Tanzania kwa sababu ya chama cha soka cha wenyeji yaani Sudan kusini kushindwa kukamilisha masharti ya CAF. Hivyo Namungo ilicheza mechi mbili za raundi ya kwanza katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam kama uwnaja wa nyumbani na ugenini, huku A Hilal wakiwa wenyeji kwenye mechi ya marudiano.

Hali kadhalika katika mchezo wa raundi ya pili dhidi ya CD De Agosto ya Angola, shirikisho la soka la Afrika liliamua kupanga mechi zote zichezwe Tanzania kutokana na kushindika kufanyika nchini Angola baada ya mzozo na mamoaka ya nchi hiyo.

Timu ya Namungo wakiwa nchini Angola walikumbana na matatizo na mamlaka za nchi hiyo ambayo ilichangia kufutwa mechi yao kutokana na mzozo wa ugonjwa wa corona. CAF iliamua mechi zote mbili zichezwe kabla ya Februari 26 mwaka huu.

Mchezo wa kwanza umefanyika wikiendi iliyopita yaani Februari 21 ambapo timu y aNamungo wakiwa wageni wa De Agosto kwenye dimba la Azam Complex waliibuka na ushindi wa mabao 6-2.

Mchezo wa marudiano Namungo watakuwa wenyeji kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex. Ili iweze kufuzu hatua ya makundi inabidi De Agosto wanatakiwa kuifunga Namungo mabao 5-0 kisha wasiruhusu nyavu zao kutikishwa na washambuliaji hatari kama vile Stephen Sey wa Namungo.

Mechi nne zilizochezwa kati ya Al Hila, Namungo na CD De Agosto inatuletea tafakari kuwa Tanzania inao uwezo wa kuandaa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ambayo ni maarufu kama CHAN.

Aidha, uenyeji huu unajenga imani katikasekta ya michezo baada ya kuwa na kiwanja kizuri kama Benjamin Mkapa na Uhuru  vya Dar es salaam na Amaan uliopo Zanzibar.

Miaka kadhaa iliyopita  Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17. Hatua hiyo ilileta heshima kwa nchi, kwani ni sehemu ya mchakato wa kuendeleza sekta ya michezo. Kwa namna fulani uenyeji huo umekuwa chachu kwani baadhi ya viongozi wa klabu na timu za taifa walitumia kama sehemu ya kujua maendeleo ya sekta ya michezo.

Kwa mantiki hiyo inawezekana kabiasha kutumia uenyeji wa mashindano ya vijana na sasa mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa kama sehemu ya kutangaza uwezo wa kuwa mwenyeji wa michuano kama CHAN.

Hoteli zipo, viwanja vya mazoezi vipo, viwanja vya kutumika kwenye amshindano vipo; Tanzania ina viwanja vya uhakika kuandaa mashindano kama ya CHAN, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Uwanja wa Azam Complex, Uwanja wa Amaan Zanzibar. Viwanja vingine vinahitaji marekebisho tu kama vile CCM Kirumba (Mwanza) au Sheikh Amri Abeid (Arusha).

Ninaamini heshima ya kimichezo tunayopata sasa tunaweza kuitumia kama njia ya kuomba uenyeji wa mashindano mengine kama CHAN hata tukiweza kujilipua kuandaa AFCON. Jambo la muhimu ni utashi wa serikali, viongozi wa TFF na wadau wa michezo. Iwapo tumeandaa mashindano ya chini ya miaka 17, tunaweza kuomba mengine ya chini ya miaka 20 hata michezo kama All Africa Games tunao uwezo wa kuandaa ikiwa utashi wa serikali utadhihirika huko tuendako.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Darren Drysdale

Maajabu ya refa kupigana na mchezaji uwanjani

Kylian Mbappe

Mbappe kuwa nyota au kumezwa na kivuli cha Neymar?