in , , ,

TFF YAMALIZA MKUTANO MKUU

MARSH KUAGWA LEO MUHIMBILI

27 WAITWA STARS KUWAVAA MALAWI

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka katika ukumbi wa Morogoro hoteli ya mjini Morogoro ambapo mgeni Rasmi alikua ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe.

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Dr Rutengwe aliushukuru uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Morogoro.

Akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu Dr Rutengwe alisema, TFF ina changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau wa mpira wa miguu nchini kwa ujumla, changamoto hizo ni kukosekana kwa wataalamu wa vyakula, wataalamu wa tiba na wataalamu wa saikolojia.

Dr Rutengwe aliomba TFF kwa kushirikiana na serikali inapaswa kuandaa wataalamu wengi wa masuala hayo ili kuweza kuendana na mahitaji ya kuwaanda wanamichezo bora ambao watakua tayari kwa ushindani na sio ushiriki.

Aidha mkuu wa mkoa huyo aliipongeza Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kuupa mkoa wa Morogoro uenyeji wa mkutano mkuu ambapo pia umefanyika na malengo kufanikiwa kwa asilimia mia moja, na kusema kwa niaba ya serikali ya mkoa wapo tayari kupokea tena mwaliko wa uenyeji wa mikutano mbalimbali ya TFF.

Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, ripoti kutoka kwa Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.

Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.

Kwa mara ya kwanza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepata bendera yake ambayo ilipitishwa na mkutano mkuu na asubuhi ya jumapili Machi 15 mwaka huu, imepandishwa kwa mara ya kwanza Morogoro hoteli.

Aidha wajumbe wa mkutano mkuu pia wamepitisha azimio la kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini (FDF), ambapo kutaundwa kamisheni maalum itakayoshugulikia suala hilo.

Lengo la kamisheni hiyo ni kuisaidia TFF kuandaa na kuratibu mipango ya maendeleo ya soka la watoto, vijana, wanawake nchini na kuviwezesha vyama vya soka vya mikoa (FA), vyama shiriki vya TFF kujiendesha katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya soka la vijana.

Pia mkutano mkuu huo ulitoa azimio la kuitaka serikali itoe msamaha wa kodi kwa vifaa vya michezo hasa vinavyotumika kufundishia watoto michezo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 125 na kati yao wajumbe watano ni wanawake.

Kikao kijacho cha mkutano mkuu kitafanyika kati ya mwezi Novemba na Disemba mwaka huu.

27 WAITWA STARS KUWAVAA MALAWI

rp_taifa-stars-01bc.jpg
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) Mart Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijin Mwanza Machi 29, 2015.

Taifa Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa mwezi huu, itaingia kambini machi 22 machi katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.

Wachezaji walioitwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo ni; Magolikipa, Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).

Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry – Qatar),

Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (Tp Mazembe – Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio (Zesco United – Zambia)

Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.

Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

MARSH KUAGWA LEO MUHIMBILI

Marehemu Sylvester Marsh, wakati wa uhai wake.
Marehemu Sylvester Marsh, wakati wa uhai wake.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Mh. Jamal Malinzi ametuma salamu za ramirambi kwa familia ya Marsh kufuatia kifo cha kocha wa Taifa ya vijana Sylvester Marsh kilichotokea jana jijini Dar es salaam

Katika salam zake kwa familia ya marehemu, Mh. Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini TFF imeshtushwa na msiba huo na kusema Shirikisho na Taifa limempoteza mtu muhimu katika mpira wa miguu nchini.

Mwili wa marehem Marsh utaagwa leo saa 6 kamili mchana, katika kanisa la Hospital ya Taifa Muhimbili na kutasafirishwa kuelekea Igoma jijini Mwanza kwa mazishi majira ya saa 8 kamili mchana kwa bus dogo (coaster) laTFF.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Mtihani wa Arsenal kufikia lengo msimu huu

Mbio za nne bora zapamba moto