in , , ,

Tetesi za usajili leo …

*Hull watoa dau kwa Welbeck, Arsenal Cavani
*Liverpool wanawataka Rossi, Sergio Romero

 
WAKATI Ligi Kuu ya England (EPL) ikikaribia kuanza, tetesi za usajili zinazidi, ambapo Hull wapo tayari kuvunja rekodi ya klabu yao wakitaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck.

Bosi wa Hull, Steve Bruce yupo tayari kutoa pauni milioni 14 kumpata mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya England ambaye ameambiwa na kocha Louis van Gaal kwamba uwezekano wa kuanza kwenye mechi ni mdogo, maana watachezeshwa Wayne Rooney na Robin van Persie kwenye ushambuliaji.

Hull wanatafuta mtu wa kuziba pengo la Shane Long aliyeuzwa Southampton kwa pauni milioni 12 katika njia za kuziba mpasuko uliotokea huko baada ya wachezaji sita nyota kuhama kiangazi hiki.

Van Gaal anaweza kukubali kumuuza Welbeck ili atumie fedha hizo kuimarisha kikosi anachokijenga upya taratibu na pia Welbeck anataka kubaki England na kupata muda wa kucheza ili afikiriwe kwenye timu ya taifa itakayoanza karibuni mechi za kufuzu kwa michuano ya Euro 2016.

Arsenal wanamfukuzia mshambuliaji wa Paris St-Germain, Edinson Cavani, licha ya mchezaji huyo kudai kwamba atabaki Ufaransa. Vyanzo vya habari vinavyoaminika vinaeleza uwezekano wa mchezaji huyo kuhama, ikiwa tapata dau zuri na klabu yake kuona ni sawa.

Arsenal pia wanataka kumsajili mchezaji wa kiungo aliyekuwa Queens Park Rangers (QPR),  Stephane Mbia na sasa ni mchezaji huru. Arsenal pia wapo tayari kutoa pauni milioni nane kwa ajili ya kumsajili kiungo mkabaji wa Newcastle, Cheick Tiote, raia wa Ivory.

Kuna habari pia kwamba Sami Khedira anaweza kujiunga na Arsenal au Chelsea, baada ya Real Madrid kumwacha nje ya kikosi chake kilichocheza kwenye Super Cup ya Uefa dhidi ya Sevilla.

Kadhalika zipo taarifa kwamba wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Olympiakos, Kostas Manolas kwa ajili ya kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyeuzwa Barcelona. Haijulikani kama Manolas atakubali kuwa chaguo la pili baada ya akina Per Metersacker na Laurent Koscielny kwenye beki ya kati.

Kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin anadaiwa kukubaliwa kuondoka kujiunga na timu anayoipenda ya Tottenham Hotspur. Kiungo mwingine wa Saints, Jack Cork naye anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kwenda Crystal Palace kwa pauni milioni tatu.

Wakati huo huo, Inter Milan wa Italia wanataka Spurs wawalipe pauni milioni 10 na pia wawape mshambuliaji wao aliyefulia msimu uliopita, Roberto Soldado kisha wao wampeleke White Hart Lane kiungo Fredy Guarin kutoka Italia.

Liverpool wanaendelea na kasi yao ya kutaka kusajili, ambapo wanataka kumpata mchezaji wa Fiorentina aliyepata kucheza Manchester United Giuseppe Rossi. Liverpool wanadaiwa pia kutaka kumsajili kipa wa Sampdoria na Timu ya Taifa ya Argentina, Sergio Romero.

Mlinzi wa Argentina, Marcos Rojo anayetaka kujiunga na Manchester United amechukuliwa hatua za kinidhamu na Sporting Lisbon kwa kutaka kulazimisha kuhama wakati mkataba wake bado unamfunga.

Aston Villa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Serge Gnabry kwa mkopo kwa sababu hatapata muda wa kucheza hapo Emirates. Kuna ushindani kutoka  Southampton, Newcastle, Sunderland na Crystal Palace kwa ajili ya kiungo huyo Mjerumani mwenye umri wa miaka 19.

Atletico Madrid wameanza mazungumzo na Chelsea kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani, Andre Schurrle.
Kipa wa Manchester United, Anders Lindegaard amesema anatafuta timu nyingine ili aweze kucheza mechi nyingi zaidi, hasa awe chaguo la kwanza.
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man U na ‘mechi ya watoto’

Luis Suarez abakishwa kifungoni