CHAN
Mafanikio waliyopata Morocco kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN yana sura mbili; kuanzia vipaji walivyo navyo ndani ya kikosi chao, umahiri,kiwango na historia ya soka haijawahi kuwanyima walau kiasi kidogo cha mafanikio pamoja na mafanikio ya vilabu vyake vinne vilivyotikisa kwenye mashindano ya CAF msimu uliopita hivyo kuhamishia mafanikio hayo kutoka ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.
Ushindi waliopata Morocco dhidi ya wenyeji wa Fainali za CHAN, Cameroon ni ushahidi kuwa mchezo wa kandanda haujawahi kuwanyima kila kila kitu mashabiki na wadau wa soka. Morocco wanatembea kifua mbele kwenye fainali hizi baada ya kutinga fainali kibabe kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi wenyeji.
Ushindi huo umewazindua maelfu ya mashabiki barani Afrika wakijiuliza namna gani Morocco inapiga hatua kwenye mashindano ya ndani kinyume cha ilivyotarajiwa. Labda wengi waliamini timu mwenyeji mara nyingi hushinda kila kitu mashindanoni lakini mambo hayakuwa hivyo.
Miongoni mwa hirizi kubwa inayowapa furaha na shangwe mashabiki wa Morocco ni kijana Sofiane Rahimi anayekipiga katika klabu ya Raja Casablanca. Huyu ni toleo jipya la vipaji vya soka ambavyo vimewahi kujitokeza nchini Morocco zama za akina Badou Zaki.
Badou Zaki ni miongoni mwa nyota waliotamba enzi zao kabla ya baadaye kuibuka kuwa kocha aliyetikisa barani Afrika kwenye fainali za AFCON mwaka 2004 kwa kutinga fainali kabla ya kufungwa na wenyeji Tunisia.
Zaki akawa miongoni mwa makocha niliokuwa nawakubali kwa sababu ya hamasa na kuwafanya wachezaji wake kama wadogo ama watoto wake ambao walishangilia na kufurahia naye kila dakika ya mchezo.
Alikuwa kocha ambaye aliwahamasisha Morocco kwa kiasi kikubwa wakiwa na mastaa kama Moustapha Hadji, Yousef Chippo na Zairi. Kipaji cha Jaziri kilikuwa habari nyingine na kilionesha Morcoo wanajua mpira.
Moustapha Hadji alikuwa akichuana na utitiri wa vipaji vya kutisha kutoka Nigeria kwenye tuzo za soka Barani Afrika. Uwezo,ufundi na uhodari vilimfanya Hadji kuibuka mchezaji bora Afrika kwenye baadhi ya tuzo. Kana kwamba haitoshi baada ya Moustapha Hadji akaja mdogo wake Yousef Hadji ambaye kama kaka yake naye alikuwa anakipiga soka la kulipwa Ligue 1 nchini Ufaransa.
Katika historia ya kandanda barani Afrika kumekuwa na mataifa vigogo waliotamba katika nyakati mbalimbali. Morocco ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebahatika kuwakilisha bara la Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia mara kadhaa.
Bahati mbaya katika zama za vipaji bora kabisa Morocco ikatumbukia kwenye utumwa wa kandanda mbele ya mataifa kama vile mataifa kama Nigeria, Cameroon, Ghana na mengineyo. Wakati huo mataifa ya Afrika ya Afrika yalikuwa yamejaza wacheza wenye viwango vya juu katika Ligi Kuu za England,Italia,Ufaransa,Hispania na Ujerumani.
RAHIMI NI NANI?
Soufiane Rahimi mpaka sasa ndiye mchezaji bora wa mashindano ya CHAN ingawaje hayajafika mwisho. Kinda huyo msimu uliopita 2019-2020 alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Morocco. Alicheza mechi 28 na kufunga mabao 10 na kupika mengine 9. Msimu wa mwaka 2020/2021 katika Ligi Kuu Morocco ameshacheza mechi 5 na kufunga mabao matano na kutengeneza matatu.
Kwenye mashindano ya CHAN, amecheza mechi 5 na kufunga mabao matano na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika michezo mitatu. Kipaji cha Rahimi kimewavutia wengi lakini klabu ya Raja Casablanca imekataa ofa ya dola milioni 1.5 kutoka klabu ya Abha ya Saudi Arabia iliyotaka kumsajili Rahimi.
Taarifa ambazo TANZANIASPORTS imezipata ni kwamba Raja Casablanca wanaona dau la kumsajili lililotolewa na klabu ya Abha ni dogo mno, na zaidi wamelenga kumuuza staa huyo kwenye moja ya klabu kubwa barani Ulaya kati ya Ligi za Ufaransa, England,Italia, Ujerumani, Ureno au Hispania.
Ikumbukwe unapotaja jina la Raja Casablanca unalitaja jina la timu kongwe barani Afrika ikiwa daraja moja na Mamelodi Sundowns(Afrika kusini), Esperance (Tunisia), Club Africain (Tunisia), TP Mazembe (DR Congo), AS Vita (DR Congo), Zamalek (Misri), Ismailia (Misri), Al Ahly (Misri), Hearts of Oak (Ghana), Asec Mimosas (Ivory Coast), Wydad Casablanca kwa kutaja chache.
SIRI ZA MOROCCO
Kimsingi siri nyingine ya kung’ara katika mashindano ya CHAN ni kutokana na mafanikio ya vilabu vinne vya soka nchini humo ambavyo vilifika hatua ya nusu fainali kwenye mashindano ya CAF msimu uliopita.
Klabu hizo ni Wydad Casablanca na Raja Casablanca zilifika nusu fainali nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Vilevile klabu ya HUS Agadir yenyewe ilitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ambako bingwa alikuwa RS Berkane.
Kwahiyo mafanikio ya tiu hizo yametengeneza siri za ushindi wa Morocco kwenye mashindano ya CHAN. Kiwango walichonacho kinatokana na timu yao kuundwa na wachezaji wengi waliotoka katika vilabu hivyo vinne.
Ni muhimu kutengeneza Ligi zenye ushindani mkubwa na viwango bora. Mipango ya kuwezesha Ligi kuwa bora iko mikononi mwa mashirikisho ya soka kama TFF. Ili Ligi Kuu Tanzania bara iwe bora lazima mipango ifanyike huku klabu zikipewa taratibu na uwekezaji wenye maana kwenye mchezo wa soka. Mchezo wa soka hauna njia ya mkato kuelekea mafanikio, mipango endelevu
Comments
Loading…