KINYANG’ANYIRO cha ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania kinaendelea. Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu imetuonesha siri za klabu mbalimbali katika kjupata ushindi. Timu hizo zimesuka vikosi ambavyo vimejaa silaha za kuhakikisha wanaibuka na ushindi, hata pale zinapofungwa ni kwa sababu ya makosa ya mchezaji mmoja mmoja. Simba nimiongoni mwa timu ambazo zinawinda ubingwa wa Ligi Kuu kwa udi na uvumba, huku ikiwa imetinga hatua ya robo fainali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho ambako watamenyana na Al Masry ya nchini Misri. TANZANIASPORTS inakuleta siri tano za Simba katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.

Kombinenga ya viungo

Tangu mwanzoni kocha Fadlu Davids alikuwa anapanga na kupangua safu ya kiungo. Katika safu ya kiungo kuna wachezaji wawili nguzo kwa Simba. Safu ya kiungo ndiyo yenye silaha ya mafanikio ya klabu hii. Fabrice Ngoma na Yusuf Kagoma wametengeneza kombinenga nzuri. Wachezaji hawa wanagawana majukumu wakiwa katikati ya dimba, Fabrice Ngoma huwa anawasaidia viungo washambuliaji kupandisha mashambulizi huku Yusuf Kagoma akiwa anasaidia walinzi wake kwa kucheza katikati yao; kulia akiwa Che Malone, na kushoto kwake akiwa Ibrahim Hamza. 

Katika mfumo huu nguvu na maarifa ya Yusuf Kagoma yanampa nafasi Fabrice Ngoma kuipandisha timu na kuwapa uhuru viungo washambuliaji hasa Jean Ahoua. Kasi ya Jean Ahoua na kushambulia mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao ni kwa sababu nyuma yake kuna ulinzi mkali wa viungo hao. Ni viungo ambao wanaweza kuifanya timu pinzani inageuzwa kuwa nyanya katikati ya dimba. Kitendo cha kuweka mizani sawa ya ulinzi na ushambuliaji kwa viungo hawa inawapa nafasi viungo washambuliaji kuongeza maarifa zaidi kuliandama lango la adui. Pia kocha Fadlu Davids katika kuboresha nafasi hii pale timu inapohitaji ulinzi anao wachezaji wengine pale benchi wa kuimarisha ulinzi, na jina la haraka linalokuja ni Mzamiru Yassin.

Moussa Camara

Lango la samba lina makipa wawili mahiri sana. Aishi Manula na Moussa Camara. Umahiri wa kudaka wa Mousa Camara unachangiwa na kipaji chake alichonacho pamoja na ushindani anaopata kutoka kwa Aishi Manula. Ikumbukwe Aishi Manula alikuwa golikipa namba moja kwa muda mrefu kabla ya kuumia na kukaa nje ya uwanja karibu msimu mzima. Ushindani uliopo kwenye nefasi ya kipa ndiyo inafanya kuwa na ubora. Moussa Camara anatambua kuwa asipokuwa makini na mahiri nafasi yake inakwenda kwa Aishi Manula. Hii ni silaha mojawapo ya Simba katika kusaka ubingwa wa Ligi Kuu na taji la Kombe la Shirikisho barani Afrika. 

Safu ya ushambuliaji

Siku zote naamini kama timu haifungi mabao maana yake inajiweka katika shinikizo la kufungwa ama kuwa na wastani mdogo wa mabao katika ushindani. Wapinzani wa Simba Yanga wanafunga mabao mengi kuliko kawaida, kwa mfano wanaweza kupachika mabao matano katika mechi moja huku Simba ikiwa imefunga moja au mbili katika mchezo fulani. Lakini hadi sasa Simba wanayo silaha ya kutafuta ubingwa kupitia kwa ushindani wa Lionel Atena na Stephen Mukwala. 

Washambuliaji hawa wote wanatambua kocha wao Fadlu Davids anategemea huduma zao, na pia hakuna mwenye uhakika wa namba pamoja na kuchezeshwa kwa zamu. Mbinu ya kuwategemea wote inawaletea mabao na ushindi. Kuwachezesha kwa zamu inawafanya kila mmoja kutumia vyema nafasi anayopewa na kocha wako. Kwahiyo ushindani wao sio kuonesha kiwango bali idadi ya mabao wanayofunga ndiyo sababu ya wao kuendelea kuchezeshwa kikosini. Washambuliaji hawa wanaweza kuchangia mabao 40 katika msimu mmoja ikiwa na maana Lionel Ateba akifunga mabao 230 kisha Mukwala naye akapachika mengine 20 unakutana na idadi ya mabao 40. Kwa Kibu Dennis anakuwa na jukumu la kutengeneza mabao ambayo yanawapa uhai katika mbio za ubingwa. 

Kubadilika kwa Fadlu Davids

Umahiri wa Simba hadi sasa unachangiwa pia na namna kocha wao anavyoweza kubadilika kulingana na aina ya mpinzani anayekutana naye. Fadlu na wasaidizi wake akina Seleman Matola wanaweza kuipanga timu ya kucheza kwa kasi kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo na kuwachosha wapinzani wao. Lakini pia wanaweza kukupangia timu ya kutuliza tempo ya mchezo, na muda wote wanacheza kwa pasi fupi fupi na taratibu mno. 

Mbinu hizi zinachangiwa pia na kubadilisha wachezaji kulingana na mahitaji ya mchezo. Kama wanataka mchezo wa polepole basi watakuwekea wachezaji wa aina hiyo. Lakini kama wanataka kucheza kwa kasi basi watakuweka wachezaji ambao kuanzia dakika ya kwanza itakuwa ni mbio kali kama za Liverpool. Kubadilika na kuchukua uamuzi wa haraka katika mechi mbalimbali inaonesha namna Fadlu Davids anavyoweza kuwasaidia wachezaji kuimarika ndani ya mchezo huo huo.

Kauli moja kwa wote

Kila timu au taasisi lazima iwe na kauli moja inayotolewa na kushikiliwa. Klabu ya Simba  tangu kuanza msimu 2024/2025 wamekuwa wakisistiza kuwa wanajenga timu. Kocha Fadlu Davids amekuwa akisema kila anapofanya mahojiano kuwa anajenga timu. Benchi la ufundi lote pamoja na viongozi wake hawasemi kama wanafukuzia ubingwa. Kauli mbiu hii imedakwa mashabiki ambao wamekubali kuficha karaka zao za ushindi mioyoni kwa kusisitiza kocha wao anajenga timu. Simba wanapambana katika nafasi ya kwanza wakishindana na Yanga, lakini katika mahojiano benchi la ufundi wanasema hawajapata kile wanachokitaka badala yake wanajenga timu. 

Je nini umuhimu wa kauli hii? Kauli mbiu hii inawasaidia wachezaji kutokuwa na presha kubwa ya ubingwa. Inawasaidia mashabiki kuondokana na presha ya matokeo ya klabu yao kwani wanacho cha kujitetea kuwa wanajenga timu. Endapo watakosa ubingwa watakuwa na falsafa yao ya msimu kuwa walikuwa wanajenga timu. Pia viongozi watakuwa na jambo la kuzungumza kuwa wanajenga timu ikiwa wataukosa ubingwa. Hii inawafanya timu nzima wapiganie ubingwa katika mazingira yenye utulivu zaidi. Wachezaji wanaelewa timu yao inajengwa, na saikolojia yao inaelewa msimu huu lazima wapate ubingwa lakini kwa namna tofauti ya kujijenga.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kombe la Shirikisho; Simba washindwe wenyewe

Tanzania Sports

SIMBA VS AZAM