in , , ,

Siku ya burudani na malalamiko imewadia

MACHI 8 imewadia, inaadhimishwa kuwa siku ya wanawake duniani. Lakini kwenye mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania, Machi 8 ni siku muhimu kwa vilabu viwili nchini Simba na Yanga. Ligi Kuu Tanania bara itashuhudia mchezo maridadi kati ya miamba miwili ya soka nchini Tanzania, Simba na Yanga. Timu hizi ni watani wa jadi, ambapo zimekuwa zikishindana kutwaa mataji, kusajili wachezaji wazuri, kunyang’anyana wachezaji, kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kadhalika. Mchezo wa Machi 8 unakuja huku mashabiki wa kila timu wakiwa wamejiandaa kwa malalamiko na burudani. Kw akuzingatia mchezo huu, je ni mambo gani muhimu ya kutupiwa macho kuelekea na wakati wa mchezo wenyewe baina ya miamba hii. TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi yakinifu wa mpambano huo wa kukata shoka.

Kutoka Mijini hadi Vijijini

Dabi ya Karikaoo inawahusisha Yanga na Simba. Dabi ya Mzizima inawahusika Yanga na Azam au Simba na Azam. Lakini michezo hiyo ni muhimu inafuatiliwa sana kuanzia Mijini hadi vijijini. Kupanuka kwa matangazo ya Televisheni na usambazaji wa huduma za umeme nchini umewezesha maelfu ya amshabiki kushuhudia mtanange huo laivu kwenye televisheni. 

Maeneo ya Mijini watu wengi hujikusanya kwenye sehemu za starehe na burudani ama wengine kwenye Vibandaumiza mitaani kushuhudia mpambano wa miamba hiyo. Azam TV na serikali wamefanikiwa kuipeleka Dabi ya Kariakoo hadi vijijini. 

Maeneo kadhaa ya vijijini kwa sasa yanashuhudia mechi za Ligi Kuu moja kwa moja. Haya ni mafanikio ambayo TFF inatakiwa kujivunia kwani inajenga ngome ya watanzania kupenda ligi yao na kuunga mkono wachezaji wao. Katika Dabi hii si watu wa mjini pekee ndiyo wanaofaidi, bali hata watu wa Vijijini wanashikwa vyema na wanafurahia. 

Filimbi ya Ahmed Aragija

Sio siri mwamuzi Ahmed Aragija ni tishio kwa kiwango. Ni kati ya marefa ambao wanasifika kwa ustadi na umakini wa kutafsiri sheria za soka nchini. Huyu ndiye mwamuzi ambaye amekabidhiwa jukumu la kusimama katikati ya dimba kuziamua Yanga na Simba. Ni refa tishio kwa sababu hana ubabaishaji, hababaishwi na presha ya mchezo, haogopi kutoa maamuzi sahihi dhidi ya timu yoyote iwe Yanga au Simba hasa pale sheria inapoelekeza. 

Kama kadi nyekundu anatoa, penati anatoa na zaidi mara nyingi anakuwa karibu na matukio ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa yenye utata. Refa huyu ana beji ya FIFA. Ni kati ya marefa wenye sifa nyingi wawapo dimbani. Ni refa ambaye filimbi yake inapopulizwa inaonesha bayana anajiamini, anajua kuongoza mchezo kwa mujibu wa sheria. 

Tanzania Sports

Filimbi ya Aragija wakati mwingine inatuachia burudani ya soka, anaruhusu mpira uchezwe na kila timu ishinde kwa juhudi na maarifa yake. Huyu ni refa wa kuaminika na hana mashaka yoyote kila anapotafsiri sheria 17 za soka. Machi 8 filimbi ya Ahmed Aragija itaamua kama Yanga au Simba wataburudika au watalalamika. Ni filimbi ambayo ikipulizwa pande zote zinakuwa na imani kuwa mchezo upo katika mikono salama ya uamuzi.

Mtetezi wa kombe na mjenga timu

Moja ya falsafa muhimu inayotumika klabu ya Simba ni kujenga timu. Wenzao Yanga ni bingwa mtetezi ambaye anataka kudhihirisha sababu za kulishikilia kombe hilo. Ili utetee ubingwa wako lazima umfunge mtani. Na ili ujenge timu yako lazima umfunge mtani. Katika mchezo huu Fadlu Daviids ana kibarua cha kuthibitisha kwamba lilipofika suala la mechi dhidi ya Yanga anao uwezo wa kushinda. 

Ni kweli kwamba Fadlu Davids amejijenge aimani miongoni mwa mashabiki, lakini sehemu ambayo auasubiriwa ni hili la kuifunga Yanga. Atajenga timu kwa kila namna lakini lazima awape burudani mashabiki kwa kuwashinda Yanga. Lakini Yanga wanafahamu kuwa ili kuthibitisha wao ni miamba ya soka nchini lazima wamgomee Fadlu Davids. Kwa maana hiyo Yanga nao wanacho cha kuthibitisha kuwa hawawezi kufungwa na Simba kirahisi. Kufika hapo unakuta mchezo huu unaibua ushindani katika idara nyingi na kuufanya kuwa muhimu kuanzia Mijini hadi Vijijini.

Kulia na kushoto kwa Simba

Kocha wa Simba anatakiwa kuwa mwangalifu kwa upande wa mabeki wake wa kulia na kushoto. Mohammed Hussein ni beki mzuri sana mwenye uzoefu wa ndani ya nje., mechi kama hizi ana uizoefu nazo, lakini msimu huu upande wake kunatumika kama njia kuanzia dakika 75 ambapo wapinzani wamekuwa wakituimia upande huo mara nyingi kwa sababu wanagundua beki na nahodha wa Simba anakuwa amechoka. 

Kwahiyo ni jukumu la kocha Fadlu Davids kuangalia namna bora ya kuimarisha kadiri mcherzo utakavyokuwa unakwenda. Upande wa kulia wa Simba kwa Shomari Kapombe ni silaha nzuri ya kutengeneza mabao, lakini pia umetumika kama njia ya kuwaadhibu wana msimbazi. Kwamba Shomari Kapombe huwa anatamani kusonga mbele zaidi na anapendelea kushambulia mno, hivyo uwiano wake wa kujilind ana kushambulia haufanani. Kama timu inachza mashambulizi ya kushtukiza eneo la kulia mwa Simba linaweza kutumika kama nyenzo ya kuwaadhibu. Kwa ujumla Shomari Kapombe ndiye beki pekee wa kulia mwenye ubora na uzoefu nchini, hivyo bado ni nafasi yake. Maboresho madogo ya kimbinu kulingana na mchezo ni kawaida. 

Safu za ushambuliaji Simba, Yanga

Yanga wanategemea zaidi kasi ya Clement Mzize, Prince Dube, Pacome Zouzoua na Aziz Ki. Wakati Simba wanategemea Jean Ahoua, Lionel Ateba, Stephen Mukwala, na Kibu Dennis. Sifa ya wachezaji wa vilabu hivi wanaweza kuendana na kasi aina ya yoyote. 

Safu ya ushambuliaji ndiyo itakayoamua nani ataibuka kidedea na nani ataishia kulalamika. Safu hizo zote zina uwezo wa kufunga mabao si chini ya matano ndani ya mchezo mmoja kwahiyo ni sehemu ya kivutio cha mchezo huu. Kuna mabao ya Mzize na Ateba, kisha kuna kasi ya Dube na Kibu Dennis. Kwa ujumla safu hii itakuwa na jukumu la kuboresha maarifa yao kusaka ushindi wa timu.

Walinzi wenye utimamu

Makosa binafsi ya mchezaji wa safu ya ulinzi yanaigharimu timu. Baadhi ya makosa hayo ni utoaji mbaya wa pasi, kupoteza umakini katika nyakati kadhaa, kukosa maarifa ya kuwasaidia viungo ni miongoni mwa mambo yanayosababisha timu kuelemewa na mashambulizi. Kama mabeki wanaweza kuipandishatimu maana yake wanaongoza nguvu kwa viungo wao ambao wanakuwa na nafasi nyingi za kutengeneza kwa ajili ya washambuliaji wao. Hii ni mechi ambayo kila upande inautaka. Kuna burudani tutashuhudia na kuna malalamiko tutaona. Kila la heri.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Changamoto ya kufundisha timu ya Taifa Morocco

Tanzania Sports

Man United kwenye mstari wa kushuka daraja