ILICHUKUA miaka 40 hadi Tanzania kufanikiwa kufuzu Fainali za Koimbe la Mataifa ya Afrika (AFCON) huku ikiwa imepitia mipango na miakkati mbalimbali hadi kuwa miongoni mwa zile nchi zinazoeleka kufuzu mashindano hayo. Wakati AFCON ikianza kuzoeleka kwa mashabiki wa soka, Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars imekuwa miongoni zile zinazofanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika na Dunia, pamoja na vikosi vya vijana wa Serengeti Boys (U17) na Ngorongoro Boys(U20). Sekta ya michezo imechukua sehemu kubwa ya maisha ya raia milioni 60 wa Tanzania huku mchezo wa soka ukizoa mamilioni ya watu wa Taifa hilo kutoka Afrika Mashariki.
Kushindwa kufuzu fainali za AFCON kulisababisha Tanzania ianze safari ya kutafuta suluhisho ili kuwa mojawapo ya nchi zenye mafanikio kisoka barani Afrika. Mara ya mwisho Tanzania kucheza fainali za AFCON ilikuwa mwaka 1980 katika mashindano yaliyofanyika nchini Nigeria na yakihusisha Mataifa manane pekee. Kuanzia wakati huo soka la Tanzania lilipotea katika ramani ya mafanikio na kukaribisha malalamiko kutoka kwa wadau wakihoji mwelekeo wa uongozi na serikali katika kuboresha michezo nchini. Lakini miaka 40 baadaye yaani mwaka 2019 Tanzania ilishiriki mashindano ya AFCON ikiwa ni mara ya pili kwao ambazo zilifanyika nchini Gabon.
Je nini kilifanyika hadi Tanzania kuanza kunufaika kwa kufuzu fainali hizo?
Fainali ya CAF 1992
Ngazi ya klabu ndiyo hutayarisha wachezaji imara na kulelewa katika misingi ya mafanikio. Klabu ya Simba ilifanikiwa kucheza fainali ya kombe la CAF mwaka 1992 ambapo walifungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast. Safari ya klabu ya Simba hadi kufika fainali hiyo ilitafsiriwa kuwa kumbe inawezekana kwa klabu za Tanzania kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote.
Kutokana na mafanikio hayo, falsafa ya ushindani ilisambaa kwenye vilabu vingine ambapo vilishiriki kwenye mashindano ya CAF, mfano Yanga walitinga robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1998 wakiwa na kocha Tito Mwaluvanda. Hiyo ilikuwa ni miaka sita baada ya Simba kufika fainali. Ushindani wa vilabu ulianza kujenga sekta ya michezo hususani soka na kuongeza ari miongoni mwa viongozi kuhakikisha wanasajili wachezaji wenye uwezo na kzualisha wengine wapya kwenye mchezo huo. Fainali ya CAF yua Simba ilitengeneza kiwango cha mafanikio ya vilabu vya Tanzania hivyo ilikuwa lazima vifikie ngazi ya juu zaidi.
Vijana kufuzu AFCON
Kwenye mashindano ya AFCON timu za taifa za vijana chini ya 17 vimefanikiwa kufuzu mashindano hayo mara kadhaa. Katika hatua hiyo Shirikisho la Soka nchini TFF lilikuwa linasimamia mpango ya kuhakikisha wanakuwa na vikosi imara na vyenye vipaji vya kuanzia umri wa miaka 15, 17 na 20. Kwenye mchakato wa kushiriki mashindano ya vijana kikosi chenye umri wa miaka 17 ndicho chenye mafanikio zaidi na kuleta baadhi ya vijana ambao wamelisaidia taifa hadi leo. Katika kikosi cha Yanga wachezaji kama Abdultwalib Msheri, Dickson Job,Kibwana Shomari, Nickson Kibabage ni zao la kikosi cha umri wa chini ya 17 ambacho kilicheza mashindano mbalimbali kwa mafanikio. Wengine ni Himid Mao anayecheza soka la kulipwa nchini Misri, ambaye ni mchezaji wa aina yake aliyepitia ngazi zote za timu ya Taifa kuanzia U17,U20,U23 na Taifa Stars pamoja na mwingine Kiggi Makassy.
Tukirudi nyuma mwaka Tanzania ilifanikiwa kufuzu mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ambapo makosa yaliyotokea yalisababisha kuondolewa mashindanoni. Umri wa mchezaji kiraka Nurdin Bakari ulileta mkanganyiko na hivyo Tanzania kuondolewa kwenye ushiriki wa mashindano hayo. Angalau hatua hiyo ilionesha jinsi Tanzania inavyopambana ili kuwa na timu bora na washiriki wenye mafanikio siku za mbele kwenye mashindano ya CAF.
Msako wa vipaji Kombe la Taifa
Shirikisho la soka TFF lilisisitiza mpango wa kuendeleza vijana kwa kusaka vipaji mikoa mbalimbali na kuwachagua wale waliokuwa nasifa ya kuunda timu za Taifa za ngazi mbalimbali. Chini ya Uongozi wa aliyekuwa rais wa TFF, Leodgar Tenga mashindano ya Kombe la Taifa yalirejeshwa kwa kushirikiana na serikali. Awali mashindano hayo yalikuwa sehemu ya kuibua vipaji na kutumika katika vilabu kabla ya kusitishwa kwa muda. Uongozi wa Rais Tenga uliketi mezani na serikali kisha kurudisha mashindano hayo yaliyochochea ari ya michezo mingine kuwa na mipango thabiti ya kutafuta vipaji na mafanikio.
Mfumo wa mashindano ya Kombe la Taifa ulihusisha Mikoa yote ya Tanzania na kucheza katika kituo kimoja cha Dar Es Salaam. Kupitia mashindano ya Kombe la Taifa baadhi ya wadhamini walijitokeza ili kuunga mkono juhudi za TFF na serikali kupitia Wizara ya Michezo na Utamaduni. Miongoni mwa wadhamini hao ni kampuni ya Cocacola ambayo baada ya miaka kadhaa ilijitumbukiza kwenye mashindano ya Kombe la Taifa.
Mashindano ya Kombe la Taifa yalielekezwa kwenye muundo mpya wa shindano Copa Cocacola ambalo lilikuwa kuvipaji vyua wachezjai wenye umri mdogo. Mabadiliko hayo yalikuwa na maana kupunguza wimbi la wachezaji wa Ligi Kuu kutumika kwenye timu za Mikoa kushiriki Mashindano ya Kombe la Taifa. Copa Cocacola ilifanikiwa kuwaibua wachezaji mbalimbali ambao walikuja kusajiliwa na vilabu vya Ligi Kuu pamoja na kutumikia Timu za Taifa katika ngazi zote.
Aidha, TFF ilikuwa na mpango mwingine wa “Taifa Stars Maboresho” ambao ulilenga kuunda timu imara ya Taifa ya mchezo wa soka. Katika kipindi hicho wachezaji walikusanywa na kupelekwa kwenye mafunzo katika Chuo cha Ualimu cha Msasani, Tukuyu mkoani Mbeya. Wachezaji waliandaliwa,kupata elimu ya michezo,kufundishwa namna bora ya kuendeleza vipaji na kutumikia Taifa. Mpango huo ulikuwa sehemu ya mchakato wa kutafuta ubora katika mchezo wa soka.
Vikosi vya vijana katika klabu
TFF kwa kushirikiana na wadau wa soka walikubaliana kutunga sheria ambazo zinaagiza vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania kuwa na vikosi vya chini ya miaka 20. Vikosi hivyo vilitakiwa kushiriki mashindano ya Ligi Kuu sambamba na timu za wakubwa. Kila klabu ilitakiwa kutekeleza sheria hiyo kama kigezo cha kushiriki Ligi Kuu. Utaratibu huo ni kamaule ambao Ujerumani ulitumia wakati wa kutoa ruzuku kwa vilabu kwa kuanzisha akademi za soka. Hali kadhalika Tanzania ilianzisha mpango huo kwa nia ya kuibua vipaji bkwatika mkondo maalumu badala ya kusubiri majukumu ya Shirikisho pekee.
Kwa kuzingatia ubora huo TFF ilihakikisha hakuna klabu inayoshiriki Ligi Kuu bila kuwa na kikosi cha chini ya miaka 20. Mpango huo umeziwezesha vilaji mbalimbali kuibuka na vijana wenye vipaji na ambao sasa wanatumikia timu za Taifa katika ngazi mbalimbali. Vilevile mpango huo ulipunguza gharama kwa vilabu za kununua wachezaji kila msimu, badala yake wale walioonekana kuwa bora walipandishwa timu za wakubwa na kung’ra Ligi Kuu. Vilabu vyote 16 vinatakiwa kuwa na kikosi cha chini miaka 20 kinachoshiriki michezo ya Ligi Kuu, na hakuna kisingizo chochote kinachotakiwa kuletwa mezani. Kwa kuzingatia hilo TFF yenyewe iliamua kuanzisha akademi yao ambayo inatumika kukuza wachezaji na kuwapandisha timu za vijana pamoja na kuwauza baadhi yao kwenda vilabu vya Ligi Kuu nchini.
Mashindano ya Mitaani
Mashindano ya soka la mtaani yanaendeshwa na taasisi binafsi maarufu kama “Ndondo Cup”. Mashindano hayo hukusanya wachezaji kutoka sehemu mbalimbali na yanafuata taratibu zote za usimamizi wa soka. Iddi Nado, staa wa Azam Fc ni matokeo ya mashindano ya soka la mitaani. Mashindano hayo hushirikisha timu za mitaani ambazo hazipo katika mfumo wa ngazi ya Ligi. Wachezaji kutoka mitaani wanapewa nafasi ya kuchezea timu zao za mtaani.
Mfumo wa mashindano hayo hufanyika katika kituo kimoja na mwisho kunakuwa na mchezo wa fainali na bingwa hukabidhiwa kombe na kitita cha fedha. Ni aina ya mashindano ya kimtaani zaidi (Street Football). Mashindano haya yamekuwa yakiwavutia wadau wa mchezo wa soka ambapo hutembelea viwanja mbalimbali mitaani ili kubaini vipaji vya wachezaji. Katika mashindano haya uhuru wa wachezaji ni mkubwa kuliko ufundi wa kutengenezwa na makocha. Kwenye mashindano ya mitaani wachezaji wanakuwa huru kucheza kwa ufundi wao, kuonesha kile walichonacho na ambacho kinawavutia wadau wa vilabu vya Ligi Kuu hivyo hjufanya uamuzi wa kuwasajili.
Fainali za CHAN
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ni miongoni mwa jukwaa ambalo Tanzania imeshiriki. Chini ya kocha Marcio Maximo na uongozi wa Rais wa TFF, Leodgar Tenga ulichangia kushuhudua Taifa Stars ikifurukuta na kufuzu kwa mashindano ya CHAN. Haya ni mashindano ya kwanza kwa Tanzania iliwezesha kutambulisha vipaji na uwezo wake.
Ingawaje Taifa Stars haikupiga hatua mbele lakini iliwezesha kuwafungua macho wachezaji wengi wa Ligi Kuu Tanzania katika ulingo wa Kimataifa. Wakati wakishiriki CHAN Tanzania haikuwa na mafanikio makubwa kwa vilabu au timu za Taifa. Kwahiyo CHAN zilikuwa fainali za kwanza kushuhudia vipaji vilivyosakwa sehemu mbalimbali nchini vikianza kuonesha cheche zao. Vilevile ilikuwa awamu ya kwanza kuona mipango na mikaikati ya kuimarisha soka ikianza kuleta matunda.
Mabadiliko ya Ligi Kuu
TFF kwa kushirikiana na wadau wa soka ilifanya mabadiliko makubwa kwenye eneo la wachezaji wa kigeni kucheza Ligi Kuu. Tangu idadi ya wachezaji wa kigeni ilivyoongezwa kuanzia 5 hadi 12 imelisaidia soka la Tanzania kupiga hatua. Katika kipindi hicho Ligi Kuu imechangamka kwa kiasi kikubwa na kuvutia wadhamini mbalimbali. Mikakati hiyo inafanywa kwa ushirikiano na Baraza la Michezo, Wizara ya Michezo, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Elimu na Shirikisho la soka ya kuvutia wadhamini binafsi, kutengeneza mazingira mazuri ya utenaji wa kazi wa wachezaji wa kigeni pamoja na kuuza haki za Ligi Kuu.
Mabadiliko ya Ligi Kuu yameleta mafanikio ambapo vilabu vya Simba na Yanga vimekuwa na mafanikio makubwa kwenye mashindano ya CAF. Ligi Kuu Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa ubora na thamani barani Afrika na kuwa miongoni mwa majukwaa bora ambayo makocha,waataalamu wa biashara,utawala na wachezaji wamekuwa wakivutiwa na soka la Tanzania. Hali ya malipo ya wachezaji kuanzia mishahara, usajili na honoraria zingine zimeifanya Ligi Kuu kuwa na mabadiliko chanya.
AFCON mfululizo na mafanikio
Hatua mbalimbali za kutaka mafanikio ya soka zimelisaidia TFF kushuhudia Taifa Stars ikifuzu mashindanoya AFCON mara tatu mfululizo. Kutoka mwaka 1980 hadi 2019 ilipita miaka 40 bila Tanzania kushiriki AFCON. Lakini kuanzia mwaka 2019 Tanzania imefuzu mara mbili mfululizo na kuwa jumla tatu. Mwaka 2023 Tanzania ilifuzu mashindano ya AFCONkwa mara ya pili ambapo fainali zake zilifanyika nchini Ivory Coast. Hali kadhalika Tanzania imefuzu kwa Fainali za AFCON mwaka 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.
Hayo ni mafanikio yaliyokuja baada ya kupitia hatua mbalimbali za makosa,kujaribu,kupanga mipango na kuamini katika mikakati iliyowekwa. wachezaji wengi ni wale wanaotengenezwa kuanzia kwenye vituo vya soka pamoja na vikosi chini ya miaka 20 vya vilabu vya Ligi Kuu ambapo baadhi yao wamekuwa chachu ya mafanikio ya soka la Tanzania.
Comments
Loading…