in , , ,

Pazia EPL linafunguliwa

PAZIA la Ligi Kuu ya England (EPL) linafunguliwa Ijumaa hii, ambapo
hadi sasa bado kuna makocha wanajaribu kukamilisha dili za kusajili
wachezaji wapya lakini pia kuachia wengine waondoke.

Chelsea ni timu inayoonekana kwamba inahitaji wachezaji zaidi ili
kujiimarisha hasa kwenye ushambuliaji, huku Tottenham Hotspur ambao
hadi Jumatano hii hawakuwa wamesajili mchezaji wakipenda kupata damu
mpya.

Miongoni mwa klabu sita za juu kwenye EPL, Manchester United wamekuwa
wakipigania kuimarisha kikosi chao huku kiungo Mfaransa, Paul Pogba
akidaiwa kwamba amekuwa akishinikiza ili aende Barcelona.

Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wanaonekana kukamilika kila
idara na inadhaniwa kwamba Riyad Mahrez ndiye alikuwa ingizo lao la
mwisho kwa msimu huu wa kiangazi.

Liverpool nao walishajiimarisha vya kutosha, kwani hata kikosi
walichokuwa nacho msimu jana kilikuwa kizuri tu.

Chelsea na Arsenal wanaingia viwanjani wakiwa na matumaini chini ya
makocha wapya, Maurizio Sarri na Unai Emery mtawalia.

Spurs wanajulikana kwamba hawakufanya usajili kwa sababu, pamoja na
nyingine, kubwa ni kuwa katika ujenzi wa uwanja mpya pale pale White
Hart Lane, jambo waliloambiwa litawapatia tabu kwa kitambo na kocha wa
zamani wa Arsenal, Arsene Wenger.

Chelsea walikuwa katika harakati za kupata kipa mpya, tena kwa bei
kubwa kutokana na Thibaut Courtois kutaka kwenda Real Madrid, lakini
pia kwenye ushambuliaji wanahitaji mtu, kwani Alvaro Morata si mzuri
kivile huku Olivier Giroud akiwa si mtu wa kukimbia hapa na pale kiasi
cha kufiti kwenye mfumo wa kocha huyo Mtaliano.

Tutasubiri kuona iwapo Eden Hazard na Willian watakuwa kwenye kikosi
cha Sarri ifikapo Agosti 31, tarehe ya mwisho kwa wachezaji wa England
kununuliwa na klabu za nje wakati Alhamisi hii ndio mwisho wa klabu
hizo kusajili.

Inaelezwa kwamba Chelsea wametenga pauni milioni 72 kwa ajili ya kumchukua kipa
Kepa Arrizabalaga wa Athletic Bilbao. Kiungo wa Madrid, Mateo Kovacic
anadaiwa nanaweza kuingia Stamford Bridge kwa mkopo.

Jose Mourinho bado ana malalamiko, na anasema kwa kikosi walicho nacho
sasa, hawawezi kufanya vyema kwenye ligi. Alikuwa anawafikiria Toby
Alderweird wa Spurs au Harry Maguire wa Leicester ili aimarishe safu
ya ulinzi. Inasemwa kwamba walikuwa pia kwenye mazungumzo kwa ajili ya
kumsajili Jerome Boateng kutoka Bayern Munich lakini kwamba alikataa
kwa upole.

Anthiny Martial anataka kuondoka lakini Mourinho ndiye wa kuamua na
kwamba anaweza kumwondosha kumuuza akipata mbadala wake kama Ousmane
Dembele anayedaiwa kuwaniwa pia na Arsenal.

Yapo matumaini Arsenal chini ya Mhispania Emery aliyetarajiwa kuongeza
mchezaji baada ya kipa Bernd Leno na walinzi wazoefu, Stephan
Lichtsteiner na Sokratis Papastathopoulos. Lucas Torreira anaongeza
uzoefu unaotakiwa kwenye kiungo na alikuwa mtamu sana kwenye fainali
za Kombe la Dunia na Uruguay.

Kwenye wingi kwa sasa bado wanao akina
Henrikh Mkhitaryan na Mesut Ozil ambao hupenda kucheza ndani zaidi
wakati Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang huwa si wazuri
sana wakicheza huko kwenye wingi.

Lakini Arsenal wanaingia kwenye msimu mpya huku mmiliki wa hisa nyingi
zaidi, Mmarekani Stan Kroenke ambaye hapendwi sana na washabiki akitoa
ofa kwa Alisher Usmanovu ili ainunue klabu kwa ujumla. Ameweka mezani
pauni milioni 550 ili anunue asilimia 30 ya Usmanov aongezee kwenye
zake zinazokaribia 70.

Dembele ni rafiki mkubwa wa akina Aubameyang na Mkhitaryan, lakini
akisajiliwa atakuwa gharama kubwa kifedha kwa Arsenal.
Emery alikuwa akimwangalia Ricardo Rodriguez wa AC Milan kwa ajili ya
kumarisha beki ya kushoto.

Liverpool wana silaha za kutosha katikati,
Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane kwenye ushambuliaji,
lakini pia asisahaulike Daniel Sturridge.

Kiungo sasa kmekuwa kizuri zaidi baada ya kuongezwa Naby Keita na
Fabinho lakini golini ni yule wa Timu ya taifa ya Brazil, Alisson.
Liver hawajapata kuwa na kipa mahiri sana tangu enzi za Pepe Reina kwa
hiyo Klopp anataka huyu awasaidie kupata alama badala ya kuzipotea
kama walivyomanyia Loris Karius na Simon Mignolet karibuni.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TUNATAKA KUMZAMISHA SALAMBA KWA KOSA MOJA

Tanzania Sports

JORGINHO, SIGARA YA ZIADA YA SARRI