in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE BAADHI YA MECHI ZA EPL WIKI ILIYOPITA

EVERTON vs LIVERPOOL

Liverpool na Everton, moja kati ya mchezo bora wa wiki

Nilitegemea kwa Kiasi kikubwa Pengo là Morgan lingezibwa kwa Kiasi
kikubwa na Barry ambaye kwa kiasi kikubwa uzoefu wake ungekuwa msaada
mkubwa sana kwa Everton.

Tom Davies amekuwa mchezaji mzuri sana katika kikosi cha Everton
ukilinganisha na umri mdogo alionao. Jana kitu pekee ambacho
kilimwangusha ni yeye kukosa uzoefu na mechi yenye kubeba hisia kubwa
za watu wengi kama hiyo ambayo ilikuwa Derby yake ya kwanza.

Kitu hiki kilisababisha Êmre Can kuwa na uwezo mkubwa wa yeye kusukuma
mipira kwa haraka kwenda kwa kina Philippe Countinho, Saido Mane na
Origi ambaye aliingia kipindi cha pili.

Msukumo huu uliipa presha kubwa sana beki ya Everton ambayo ilikuwa
imemkosa mtu muhimu kama Coelman. Kukosekana kwa Coelman kulimpa
nafasi Morgan Holgate ambaye kiuhalisia alikuwa anakosa vitu viwili,
cha kwanza alikuwa anakosa uzoefu wa derby kwani ilikuwa derby yake ya
kwanza, pia ugeni wa mfumo wa 3-4-3 ulikuwa ukimpa shida sana kwake
kitu kilichosababisha yeye ashindwe kuwa na uwiano mzuri wa
kushambulia na kuzuia.

Hali iliyosababisha upande wake wa kulia kutokuwa na mashabulizi mengi
kuelekea lango là Liverpool. Kitu ambacho kilimpa nafasi James Milner
kupanda kusaidiana na Philippe Countinho.

Mzigo ukawa mkubwa Kwake ( Morgan Holgate) ikawa inamwia vigumu kwake
kuwa na uwezo mkubwa wa kukaba ikizingatia pia jana Philippe Countinho
alikuwa katika kiwango kizuri sana.

Liverpool pia wanatakiwa watafute namna sahihi ya kwao kuwa wanazuia
mashambulizi ya kona au krosi, wamekuwa wadhaifu sana upande huo hali
inayosababisha wao kufungwa magoli mengi ya aina hiyo msimu huu .

MANCHESTER UNITED vs WBA

Wachezaji wa Manchester United, ktk moja ya wakati mzuri

Manchester United waliwakosa kwa kiasi kikubwa Herrera, Pogba, Zlatan na Mata.
Hii iliwapa nafasi kubwa Westbrom kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki
mpira na kuwapa presha kubwa Manchester United.

Pia kukoseakana kwa hao watu kulisababisha hali ya ukomavu katika
kikosi cha Manchester United kutokuwepo kwa Kiasi kikubwa.

Kwa sababu Pogba, Zlatan, Herrera na Mata wamekuwa watu ambao ni
mhimili mkubwa sana katika kikosi cha Manchester United msimu huu.

Pamoja na umri wake kuwa mkubwa lakini Zlatan amekuwa mshambuliaji
ambaye amehusika kwenye magoli mengi ya Manchester United.

Hata wachezaji waliocheza jana wamekuwa wachezaji ambao wamekuwa
hawana mwendelezo mzuri wa viwango vyao yani Henrink , Rashford,
Lingard pamoja na Antony Martial.


CHELSEA vs CRYSTAL PALACE

Benteke alikuwa mwiba mkali kwa Chelsea

Crystal Palace hawakuwa wamerudishwa nyuma sana katika nguvu zao za
kupigana baada ya kutanguliwa goli moja tena na timu bora katika kila
idara na iliyo katika nafasi kubwa ya kubeba ubingwa.

Utulivu wao uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kusawazisha na kufunga goli là pili.

Walipigana katika hali ya utulivu walijua matokeo kwao ni muhimu tena
kwenye timu kubwa kama Chelsea.

Na hii inawapa nafasi kubwa kwao kupandisha morali ya kupigana kwa
kiasi kikubwa ili waendelee kubaki katika ligi kuu ya England

Pengo la points saba unafanya kuweka uwazi wa mbio za ubingwa kwa
sababu ushindi wa Spurs jana umejenga matumaini mapya kwao kuwa
wanauwezo wa kupigana mpaka mwisho katika mbio za kusaka ubingwa.

Kitu cha muhimu kwa Spurs ni wao kuhakikisha wanashinda mechi zao bila
kuwaangalia Chelsea ili wasiwe wanacheza katika presha kubwa ndani
yao.

ARSENAL vs MANCHESTER CITY.


Arsène Wenger, akimkumbatia meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, kabla ya mchezo kati ya timu zao

Kuna vitu viwili ambavyo Pep Guardiola anatakiwa avifanye katika
dirisha kubwa la usajili majira ya kiangazi.

Cha kwanza ni kusajili beki wa kati na cha pili ni kusajili kiungo wa
eneo là ukabaji katika timu.

Mabeki wa kati wa Manchester City wamekuwa hawana uelewano mkubwa kati
yao, na kwenye mechi ya jana walikutana na timu ambayo ilikuwa haina
maelewano mazuri uwanjani.

Kuwaanzisha Welbeck, Walcot na Sanchez kwa pamoja kulikuwa na maana
kubwa mbili kwa Arsene Wenger.

Maana ya kwanza ni kwa Arsenal kupata nafasi ya kucheza mashabulizi ya
kushtukiza ( Counter Attacks) na maana ya pili ni kucheza mipira ya
moja kwa moja ( direct football).

Lakini hawakufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu, viungo waliocheza
yani Xhaka na Francis wanatabia kubwa ya kujilinda kuliko kushambulia
ndiyo maana ikawa ngumu kwao kuanzisha mashabulizi hayo.

Pili, Mesut Ozil hakuwa katika mchezo kwa kiwango kikubwa na hii
ilitokana na kukosa Match Sharpness.

Kwa upande wa mabeki wa kati wa Arsenal hawakuwa na uelewano mkubwa
kati yao, kitu kilichopunguza umakini
Ni virahisi sana kuwafunga Arsenal kwa direct football na Counter
attacks kuliko wao kukufunga kwa aina hiyo ya mashabulizi, ndicho kitu
walichokifanya Manchester City katika goli là Kwanza.

Inawezekana hukuona umuhimu mkubwa wa Jesus Navas katika mechi ya jana
lakini mimi niliona katika angle hii, pamoja na kwamba hakuwa na uwezo
mkubwa sana wa kukaba lakini alikuwa na uwezo mkubwa katika maeneo
yafuatayo. Moja alikuwa anapata nafasi ya kuingia eneo là katikati ya
uwanja kuongeza uzito eneo hilo. Pili alikuwa msaada katika kusukuma
mashambulizi.

Sane ameshakuwa mtu mkubwa tayari, maamuzi yake ni ya kiutu uzima na
yuko tayari kupewa nyumba aiongoze

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

EPL bado ngumu

Tanzania Sports

NAFASI NZURI KWA MAKAMPUNI KUNUFAIKA KIBIASHARA NA SERENGETI BOYS