in , , ,

NILCHOKIONA KWENYE BAADHI ZA MECHI ZA EPL ‘WEEKEND’ HII

CHELSEA vs ARSENAL.

Kuna vitu vingi sana viliigharimu Arsenal kwenye mechi hii.

Kuwepo kwa Oxlaide Chamberlain hakukuwa na faida kubwa sana ambayo
ingeweza kunisaidia Arsenal kwa kiasi kikubwa.

Eneo alilocheza la Deep lying Middfielder lilikuwa linamwihitaji awe
na uwezo wa kuditacte tempo ya mchezo.

Na njia moja wapo ya kuditacte tempo ya mchezo ni kusambaza mipira
maeneo mbalimbali ya uwanja ( yani kupiga pasi nyingi).

Lakini Chamberlain alikuwa hana uwezo mkubwa wa kupiga pasi nyingi,
kitu ambacho kilikuwa kinasababisha kina Ozil kufuata mipira
katikati.

Iwobi na Walcot hawakuwa wanapata mipira mingi pembeni hali
iliyowafanya Walcot na Iwobi kuonesha kiwango cha kawaida sana.

Hata Iwobi alipokuja kucheza eneo la katikati hakuwa na madhara
makubwa sana kwa Chelsea kwa sababu Iwobi hana tofauti na Oxlaide
Chamberlain kwa sababu wote ni wazuri kwa kukimbia na mpira na siyo
kupiga pasi nyingi.

Hekaheka uwanjani….

Sanchez hakuwepo kwenye mchezo ule na hakustahili kuwepo mpaka dakika
za mwisho, sema kilichombakisha ni fear factor kwa timu pinzani kitu
ambacho hakikuhitajika kwenye mechi hii, mtu ambaye alikuwa
anahitajika ni kuwabadilisha matokeo kitu ambacho Sanchez hakuwa
nacho.

Kwenye mechi ya Watford moja ya vitu vilivyowaangusha Arsenal kwa
kiasi kikubwa ni pamoja na uimara wao kiakili na kimwili.

Hiki ndicho kilichowaua tena kwenye mechi hii.

Chelsea wamekoma kiakili, akili yao Inawaza jinsi ya kupata point
tatu muda wote ndiyo maana hukuwaona wakipoteana hata kipindi
walipokuwa wanashambuliwa, hiki kitu hakikuwepo kwa Arsenal kwa
sababu hawakuwa na nguvu ya kupigana hata baada ya kufungwa.

Matic na Kante walikutana na viungo dhaifu wa Arsenal. Chelsea
walikuwa wanahasira kila walipokuwa wanashambulia wakati Arsenal
walikuwa wapole kila walipokuwa wanashambulia ( wanapress polepole
sana).

HULL CITY vs LIVERPOOL.

Jürgen Klopp, kaanza kupoteza dira….

Marco Silva kuna kitu amekileta kwenye klabu ya Hull City.

Hull City inaonekana ni moja ya timu ambazo zinapigana sana na kucheza
kwa kushirikiana vizuri.

Kwenye Mechi hii Hull City walikuwa wanakaba vizuri sana kuanzia nyuma
( Backline yao) mpaka katikati ya uwanja.

Hawakuhitaji kumiriki mpira kwa muda mrefu, ila walijitaji kukaba kwa
kushirikiana na kushambulia kwa kushitukiza. Ndicho kitu
walichokifanya na goli la pili lilitokana na shambulizi la kushtukiza.

Liverpool walibanwa kwa kiasi kikubwa kwe nye eneo lake la kiungo cha
kati ambapo ndipo pressing yao huanzia siku zote. Kubanwa kwao
kuliwafanya wapunguze presha kwa Hull City.

Hata wakati walipokuwa wanashambulia Hull City walikuwa watulivu
kupoza mashambulizi ya Liverpool.

Ukiachana na kwamba baadhi ya wachezaji wa Liverpool kushuka viwango,
pia Countinho bado hajarudi vizuri kiasi cha kuibeba timu kama
Mwanzoni, pia safu yao ya ulinzi wa kati ilikuwa mbovu sana. Mabeki
wao wa kati wamekuwa siyo wazuri kwenye mipira ya juu inayotokana na
krosi au kona, ndiyo maana hata goli la kwanza lilitokana na mpira wa
juu uliotokana na kona.

Kuondoka kwa Robert Snodgrass kumeifanya Hull City kucheza kitimu
tofauti na mwanzoni ambapo ilikuwa inacheza kwa kumtegemea yeye ( timu
ilikuwa imeundwa kumzunguka yeye). Kipa wa Hull City alikuwa mhimili
mkubwa wa ushindi, akiendelea hivi atakuwa mhimili mkubwa wa timu
kuibakisha ligi.


MANCHESTER CITY vs SWANSEA CITY.

Sergio Agüero…
Romelu Lukaku, anaongoza kwa kufunga magoli mengi

Inawezekana kitu kikubwa kitakachozungumziwa kwenye mechi hii ni
kiwango cha Gabriel Jesus.

Anaweza akaleta changamoto kubwa sana kwa Aguero. Lakini kitu kikubwa
ambacho Manchester city kimeonekana kuwasaidia sana ni namna ya
kuwaweka pamoja Toure, Fernandinho, Kelvin na Silva.

Kuwepo kwa Toure na Fernandinho kuliwawezesha Kelvin na Silva kuwa na
uwezo wa kusambaza mipira kwa kina Sane, Sterling na Jesus.

Kasi ya hawa watatu ilikuwa na madhara makubwa sana kwa mabeki wa Swansea City.

Kuna kitu kimoja ambacho Paul Clement amekijenga kwa Swansea kwa
kipindi hiki kifupi tangia aichukue timu, nacho ni uimara wa beki.

Tofauti na mwanzoni mwa msimu, Sasa hivi Swansea City wamekuwa imara
sana kwenye eneo lao la kujilinda na wamekuwa na nidhamu na uimara
sana ndiyo maana hawaruhusu mabao mengi ukilinganisha na kipindi
ambacho timu haikuwa kwenye mikono ya Paul Clement.

LEICESTER CITY vs MANCHESTER UNITED

Huan Mata….alitakata

Combination ya Ndindi na Drinking Water ilikuwa na walakini kwenye
eneo moja. Ndindi ni mzuri kwenye kukaba, lakini siyo mzuri kwenye
kuanzisha mashambulizi. Na kama unataka Drinking Water awe hai kwenye
mchezo unatakiwa umchezeshe na kiungo ambaye atakuwa na uwezo wa kuwa
anampa mipira na yeye kusambaza, hicho ndicho kilichokosekana kwa
kiasi kikubwa kati yao wawili.

Kitu kilichozidi kuleta ugumu eneo lao la kiungo ni kuwepo kwa Mata,
Herrera na Pogba ambao walikuwa wametawala eneo hili na kutengeneza
nafasi nyingi kwa kina Henrink, Zlatan na Rashford.

Safu yao ya ulinzi chini ya Huth na Morgan imekuwa mbovu sana.Kuanzia
marking yao mpaka ukabaji wao.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

CAMEROON MABINGWA WAPYA AFRIKA

HILI LA PAMBA NA TIMU ZA MWANZA, WASUKUMA MNACHEZA NGOMA GANI?