Fungate la kocha maarufu duniani, Jose Mourinho na Chelsea limefufuka, baada ya Mreno huyo mwenye umri wa miaka 50 kurejeshwa Stamford Bridge.

Hii ni mara ya pili kwa ‘The Only One’ kuajiriwa Darajani, akichukua nafasi ya Mhispania, Rafa Benitez aliyekuwa kocha wa muda baada ya kufukuzwa kwa Roberto Di Matteo mwaka jana.

Mourinho amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza kibarua chake Real Madrid ya Hispania, ambapo atakumbukwa kwa jinsi alivyotwaa ubingwa wa England mara mbili mfululizo na Chelsea kabla hajaondoka 2007.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chelsea, Ron Gourlay alinukuliwa akisema kwamba Mourinho ndiye mtu maarufu zaidi katika klabu hiyo ya London na kwamba wanafurahi kurejea kufanya naye kazi.

Mourinho anatarajiwa kutambulishwa rasmi Jumatatu ya Juni 10 na anaingia na wasaidizi wake watatu, ambao ni Rui Faria, Silvino Louro na Jose Morais.

Mourinho anaelezwa kuwa kocha maarufu mwenye ufuasi mkubwa, ambapo pia vyombo vya habari vinampenda, na hivyo wakati mwingine hufanya kazi yake kuwa rahisi.

Aliwasili Darajani kwa mara ya kwanza msimu wa kiangazi wa 2004, wiki chache tu baada ya kuiongoza Porto kutwaa ubingwa wa Ureno. Alitwaa pia makombe ya FA na Ligi akiwa na Chelsea, lakini hakuweza kutwaa kombe la Ulaya na klabu hiyo.

Aliondoka Chelsea baada ya mahusiano yake na mmiliki wa klabu, bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich kuwa mabaya, na nafasi yake ikachukuliwa na Mwisraeli Avram Grant.

Gourlay alisema kwamba lengo lao ni kuwa na Mourinho kwa muda mrefu, lakini takwimu zinaonesha kwamba kocha huyo hajapata kuwa na klabu yoyote kwa zaidi ya miaka mitatu.

Mourinho amekuwa akiendea changamoto kila baada ya kupata mafanikio, ambapo alipata ubingwa wa pili wa Ulaya akiwa na Inter Milan ya Italia 2010, lakini akaondoka na kujiungana Real Madrid, akichukua nafasi ya Manuel Pellegrini, anayeterajiwa kuwa mpinzani wake msimu ujao, kwani huenda akajiunga na Manchester City.

Akiwa nchini Hispania, alimaliza La Liga akiwa nafasi ya pili msimu wake wa kwanza, lakini alitwaa kombe msimu uliofuata, lakini msimu huu wa mwisho hakuwa na mafanikio makubwa, japo alimaliza akiwa nafasi ya pili.

Chelsea imekuwa na makocha wengi tangu Abramovich anunue klabu hiyo, wa mwanzo akiwa Claudio Ranieri tangu 2000 hadi 2004, akifuatiwa na Mourinho Juni 2004 hadi Septemba 2007 alipomwachia Grant.

Luiz Felipe Scolari aliajiriwa tangu Julai 2008 hadi Februari mwaka uliofuatia, akapewa nafasi hiyo Guus Hiddink hadi Mei 2009. Hapo alichukua Carlo Ancelotti hadi 2011 alipoitwa Mreno mwingine, Andre Villas-Boas aliyefutwa kazi Machi mwaka jana na kuajiriwa

Di Matteo na Benitez akampokea Novemba mwaka jana.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TAIFA STARS, SUDAN ZATOKA SULUHU

FA yalilia wazawa Ligi Kuu England