in ,

Natamani kocha wa Simba awe PATRICK AUSSEMS

Patrick Aussems

Simba wameshaachana na aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Sven Vandbroeck. Wameachana kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Baada ya Simba kuachana na Sven Vandbroeck swali kubwa ambalo limebaki ni kocha yupi ambaye anaweza kuja kuchukua nafasi ya Sven Vandbroeck. Ukiniuliza mimi hilo swali jibu pekee ambalo naweza kukupa ni Patrick Aussems.

Kwangu mimi huyu ndiye kocha ambaye anafaa kwa sasa kuchukua mikoba ya Sven Vandbroeck. Kwanini nasema na ninaamini kuwa Patrick Aussems ni mtu sahihi kuchukua mikoba ya Sven Vandbroeck?

Kwa sasa Simba inatazama michuano mitatu mitatu mikubwa iliyo kwenye mikono yao. Simba ina deni la kutetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Simba hiyo hiyo ina deni kubwa la kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika kama ambavyo alifanya msimu wa mwaka 2018/2019 chini ya Patrick Aussems.

Simba ina deni ya kutetea ubingwa kombe la shirikisho. Makombe haya yote tayari yashaanza na yako katikati. Kama mashindano yote yako katikati anahitajika kocha ambaye siyo mgeni kwa Simba.

Patrick Aussems siyo mgeni kwa Simba. Patrick Aussems anawafahamu vyema wachezaji wa Simba kwa sababu asilimia kubwa amefanya nao kazi wakati akiwa kocha wa Simba.

Anafahamu ubora na udhaifu wa mchezaji mmoja mmoja. Ni rahisi kufikia mahitaji ya Simba kwa sababu aina ya wachezaji wa Simba anawafahamu, hii itakuwa tofauti na kocha ambaye ni mgeni sana Simba.

Kocha ambaye ni mgeni ataanza kuanza kwanza kuwasoma wachezaji wa Simba kipindi ambacho mashindano yote anayoshindana Simba yako katikati.

Pamoja na kwamba Patrick Aussems anawafahamu vyema wachezaji wa Simba, Pia wachezaji wa Simba wanamfahamu vyema Patrick Aussems. Wanafahamu vyema mbinu na mifumo ya Patrick Aussems.

Kitu hiki kitakuwa na faida kwa sababu haitokuwa rahisi kwa wachezaji wa Simba kupata falsafa mpya kutoka kwa kocha mpya, Ujio wa Patrick Aussems hautozalisha falsafa mpya ndani ya kikosi cha Simba kwa sababu wachezaji na kocha wanajuana vyema.

Patrick Aussems ashawahi kuwasilisha robo fainali Simba. Kwa hiyo atakuwa anajua mahitaji haswa ya Simba kwa sasa na kuyafanyia kazi. Kwa kipindi hiki cha katikati ya ligi ni vyema Simba wangemleta Patrick Aussems ambaye siyo mpya sana kwa Simba kuliko kuleta kocha ambaye ni mpya.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba

TFF haitaki Simba kufundishwa na kocha MZAWA?

Yanga Vs Simba

Tuanze kumuomba samahani Onyango!