in ,

Nani Kufunga Goli Uwanja Wa Mkapa ?

Uwanja wa Mkapa

Abdi Kassim ‘Babi’ ndiye mfungaji wa goli la kwanza uwanja wa Taifa Tanzania ambao sasa unaitwa uwnaja wa Mkapa  baada ya kubadilisha jina.

Swali la kila mmoja ni nani atafunga goli la kwanza wakati jina la uwanja limebadilika historia hiyo ataitengeneza nani.

Wakati tunaendelea na historia sasa rasmi uwanja wa taifa Tanzania unaitwa Uwanja wa Mkapa baada ya Rais DKT. John Pombe Magufuli kuidhinisha.

Hii imekuja baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa wananchi(Watanzania) kuwa jina libadilishwe naye akakubali na sasa utaitwa kwa jina hilo.

Juu ya jina kila mmoja atakuwa anajua maana muda mrefu tuliita kwa Mkapa baada ya kipindi fulani kuliita jina la kwa Mchina.

Hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa aliweka wazo la kujenga uwanjamwaka 2000 baada ya kutembea nchi za nje na kuona uwanja bora kabisa.

Alisema kuwa ni aibu kwa taifa kukosa uwanja mzuri hivyo kabla ya kumaliza uongozi wake atajenga uwanja mzuri.

Wazo hilo lilikuwa kweli kwani ilipofika mwaka 2003 ilitangazwa tenda ya kujenga uwanja.

Wakati inatangazwa tenda kiwango cha fedha kilichotengwa kilikuwa ni dola milioni sitini yaani $60,

2004 kampuni ya Ufaransa iliitaka tenda hiyo ila gharama yao ilikuwa juu sana kwa walitaka dola milioni 154 ($154).

Dili hilo lilikataliwa na serikali ya Tanzania kutokana na ukubwa wa fedha hizo.

Aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje wa wakati huo ambaye ndiye rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete alisaini dili  la dola milioni 56 na serikali ya China.

Ndipo serikali ya China imeandika historia kwa kulipokea dili hilo.

Mwezi Juni 2006 kiongozi kutoka China Wen Jiabao alikuja Tanzania kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Uwanja huo ulifunguliwa mwaka 2007, na mchezo wa kwanza kabisa kuchezeka ulikuwa wa kirafiki baina ya Tanzania na Uganda Septemba 2007.

Naendeleea kukumbusha kuwa Abdi Kassim ‘Babi’ ndiye mfungaji wa bao la kwanza katika uwanja huo dakika ya 35 ya mchezo pasi ilitoka kwa Haruna Moshi ‘Boban’.

Tanzania Sports
Rais Benjamin William Mkapa

Abdi Kassim amefunga tena goli la kwanza kwa upande wa klabu katika michuano ya kimataifa wakati huo anaitumikia Azam na goli hilo alifunga dhidi ya Al Nasy, matokeo ya mwisho Azam walishinda magoli 3-1 goli hilo alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche.

Katika michezo ya mashindano uwanja huo ulishuhudiwa ukicheza kwa mara ya kwanza katika kuwania kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ‘AFCON’  kati ya Tanzania dhidi ya Msumbuji.

Kundi lao lilikuwa D, kama haitoshi uwanja huo ulichezewa mchezo wa kirafiki kati ya Gor Mahia ya Kenya na Everton ya nchini England.

Kama bado haitoshi nyota wa zamani wa Manchester United na mfungaji bora wa muda wote wa Mashetani Wekundi Wyne Rooney alifunga goli katika uwanja huo ndani ya mbungi yao dhidi ya Gor Mahia Julai 13,2017.

Jabir Azizi ameweka historia ya kufunga goli katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil iliyokuwa na nyota hodari kama vile Kaka na wengine mwaka 2010.

Fainali ya AFCON kwa wachezaji walio na umri chini ya miaka 17 iliyofanyika hapa Tanzania ilichezwa hapo.

Swali ni kwamba nani atafunga goli la kwanza baada kubadilisha jina la uwanja na kuwa uwanja wa Mkapa.

Uwanja wa Mkapa unaweza kubeba watazamaji walioketi katika viti elfu sitini 60,000.

Ila niliwahi kushuhudia watu wakijaa zaidi ya elfu sitini katika mchezo wa Tanzania dhidi ya Uganda ambao ulihusisha kufuzu michuano ya AFCON ya wakubwa.

Uwanja huu unatumika na vilabu viwili vikubwa Simba na Yanga kama uwanja wao wa nyumbani.

Huku Taifa Stars ambayo ndio timu ya taifa ikiutumia kama uwanja wa nyumbani.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Sergio Ramos

Ramos ‘beki mshambuliaji’ na rekodi La Liga

Eymael

Yanga wamechelewa kumfukuza Eymael?