in

Nani huyu anataka kuinunua West Ham United?

West Ham

Tajiri mpya ameanza kutikisa hapa London. Ni tajiri anayetaka kuonesha umwamba wake katika mchezo wa soka. Jiji la London linataka kuona mbio za tajiri huyo zitafika wapi, urefu upi,uwezo gani na uendeshaji wa klabu anayotaka utakuwaje baada ya kufanya kile anachokipigania sasa.

Jiji la London ni kama linataka kutawala EPL. Hilo ni jambo la kawaida, lakini habari ya mjini ni huyu tajiri, ametoka wapi? Anataka nini? Malengo yake yakoje? Hayo na maswali mengine utayapata katika makala haya kujua nini kinachojiri  kwa timu maarufu ya Waponda nyundo wa London, West Hammers.

Wapenzi wa mchezo wa soka wanaendelea kushuhudia mabilionea wakimiminika zaidi na kumwaga pesa ambazo awali hazikufikiriwa. Matajiri hawa wanazitaka timu mbalimbali kwa sasa miundo ya timu imewapa nafasi ya kufanya hivyo kwa maendeleo ya mchezo wenyewe.

Wakati familia ya Malcolm Glazer iliponunua hisa na kuimiliki Manchester United ulikuwa kama vile ni suala la matajiri wachache wanaweza kuzinunua timu baada ya kuchungulia fursa za kibiashara zilizopo. Hasa matajiri wa Kimarekani.

Lakini zikaja pesa za waarabu zikanunua Manchester City kutoka Qatar, na sasa Newcastle United imechukuliwa na waarabu kutoka Saudi Arabia. Kule nchini Ufaransa waarabu wakainunua PSG na inaonekana sasa ushindani wa matajiri wa kiarabu kuzinunua timu mbalimbali za Ulaya.

Inaonekana kama vile wazungu wa Ulaya wanakuja kukombolewa na pesa za waarabu ambao wameamua kuwekeza. Lakini hilo la kuwakomboa laweza kuwa utani.

Hata hivyo ukweli waarabu wameamua kuwekeza katika biashara ya mchezo wa soka na kuwapoka umiliki matajiri wenzao. Wakati habari za Newcastle United zikiwa hazipoa sasa zinahusu timu kongwe ya West Ham United.

Kwa wapenzi wa kandanda wa wanajua timu hiyo ni kama Chuo cha soka EPL. West Ham ina historia ya kuibua wachezaji wakali na wenye vipaji vya hali ya juu. West Ham inaweza kuwa kama Southampton  kwa sifa za kuzalisha vipaji vya soka EPL.

Sasa pesa za matajiri zinaelekea kuhamia West Ham, timu kongwe kama ilivyo kwa Newcastle United. Daniel Kretinsky raia wa Czech anaitaka West Ham. Yaani ni sawa na kusema tajiri kutoka nchi ya Ulaya mashariki anaelekea kumwaga pesa Ulaya magharibi na kati.

Wengi wanafahamu familia ya Kifalme ya Saudi Arabia ilivyo na mapenzi katika soka. Lakini ni wachache wanafahamu habari za Daniel Kretinsky katika ulimwengu wa kandanda. Ni kwamba bilionea huyu ndio amekuwa habari ya mjini kutokana na nia yake ya kuinunua West Ham United.

DANIEL KRETINSKY NI NANI?

Huyu ni raia wa Czech kama tulivyoona hapo juu. Ni mfanyabiashara mkubwa nchini humo na Ulaya kwa ujumla. Bilionea huyo anataka kununua asilimia ishirini na saba(27%) ya hisa za timu ya West Ham.

Ripoti toka vyombo vya habari vya michezo zinasema kuwa Daniel Kretinsky anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Euro bilioni 3.4. Malengo ya bilionea huyo ni kununua hisa nyingi kadiri awezavyo na kuimiliki West Ham United.

Ni kwamba anataka kuichukua timu hiyo inayomilikiwa na David Sullivan mwenye asilimia hamsini na moja (51%), huku mmiliki mwenza David Gold akiwa na asilimia thelathini na tano (35%).

Habari zinasema bilionea Kretinsky anataka mpango wa kuinunua West Ham uwe umekamilika mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu wa 2021. Endapo bilionea huyo atainunua Hammers utakuwa mwendelezo wa matajiri kuzinunua timu za EPL.

Daniel Kretinsky ana umri wa miaka 46 na tajiri kutoka Jamhuri ya Czech ambaye amewekeza katika kampuni mbalimbali duniani. Ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EPH ambayo hujihusisha katika sekta ya nishati Ulaya ya kati na anamiliki hisa katika kampuni ya Kijerumani ya Metro AG. Pia anazo hisa katika gazeti maarufu la Le Monde la nchini Ufaransa, pamoja ghala ya Macy’s. Ni mwanahisa katika kampuni ya Royal Mail na supamaketi ya Sainsbury. Ni mwenyekiti wa klabu ya Sparta Prague ya Czech tangu mwaka 2004.

Mikakati ya Daniel Kretinsky kuinunua West Ham United huenda ikakamilika mapema kabla ya kumalizika mwaka huu, ambapo mpango wa kwanza ni kuhakikisha suala hilo linamalizika wiki ya kwanza ya Novemba kama nilivyoeleza hapo juu.

Ripoti zinasema mkakati wake ni kuanza na asilimia ishirini na saba kisha kuichukua West Ham moja kwa moja. Kwa maana hiyo anataka kuwaondoa David Sullivan na David Gold katika umiliki wa West Ham United kwa sababu uhusiano wao na mashabiki wa klabu hiyo umevunjika katika kipindi chao. Ni matajiri ambao hawakubaliki na mashabiki na kila mara wamekuwa wakipaza sauti waondoke klabuni hapo.

Kwahiyo endapo dili la Daniel Kretinsky litakamilika bila shaka mashabiki watapiga vigelegele na shangwe kumkaribisha wakijua kutakuwa na mabadiliko kuliko wamiliki wa sasa ambao wanaonekana hawana mawazo mapya wala mikakati ya kuinua zaidi timu hiyo.

Inafahamika wamiliki wa sasa wa West Ham wamewahi kupinga mpango wa tajiri mwingine kuinunua klabu hiyo, lakini kwa mazingira ya sasa inasemekana wapo tayari kuachana na misimamo yao, na kukaribisha pesa za Kretinsky kuchukua hatamu. Na sasa majibu yanasubiriwa, ni lini atatangazwa kuwa mmiliki mpya wa West Ham. Ni mwendelezo wa matajiri kununua timu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga Vs Simba

Yanga kumaliza ufalme wa Simba?

Kibu Denis

Kama vipi tuwape uraia kina Morrison, Bangala