in

Morrison anabaki kuwa bora mbele ya “Tuisila”

Bernard Morrison

Tuisila Kisinda ni moja ya jina kubwa lililotajwa tarehe 30 mwezi wa nane mwaka huu kwenye kilele cha wiki ya wananchi.

Jina hili liliongelewa sana kwa sababu moja tu ambayo ni uwezo mkubwa wa Tuisila Kisinda aliounesha ndani ya uwanja.

Mashabiki wengi walimtazama kama mtu ambaye anaweza akawa na msaada mkubwa sana ndani ya kikosi cha Yanga. Kikosi ambacho kwa sasa hivi kinajengwa.

Tuisila Kisinda ni aina ya wachezaji ambao wanaendana na utamaduni wa Yanga. Yanga tangu zamani ilikuwa na utamaduni wa kuwatumia wachezaji hatari wanaocheza wakitokea pembeni mwa uwanja.

Tangu enzi za Edibily Lunyamila, Said Maulid “SMG” akaja Simon Msuva. Baada ya Simon Msuva kuondoka Yanga walikosa mshambuliaji anayetokea pembeni mwa uwanja.

Wachezaji wote niliowataja hapo walikuwa na uwezo wa kufunga magoli kwa kutokea pembeni mwa uwanja na kutengeneza nafasi nyingi za magoli wakitokea pembeni mwa uwanja.

Hiki kitu kipo kwenye miguu ya Tuisila Kisinda. Ana uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za magoli akitokea pembeni mwa uwanja.

Tanzania Sports
Wachezaji wa Yanga

Pia Tuisila Kisinda anauwezo wa kufunga magoli akitokea pembeni mwa uwanja. Hiki kitu ndicho ambacho kiliwafanya mashabiki wa Yanga kumuongelea sana.

Walimuongelea sana kwa sababu ni aina ya wachezaji ambao wanaendana na mahitaji sahihi ya Yanga tangu zamani.

Kabla ya ujio wa Tuisila Kisinda alikuwepo Bernard Morrison katika kikosi cha Yanga. Ni aina ya wachezaji ambao wana sifa kama za Tuisila Kisinda.

Mashabiki wa Yanga waliona uwepo wa Tuisila Kisinda ni kitu ambacho kinaweza kuwasahaulisha kwa kiasi kikubwa maumivu ya kuondoka Bernard Morrison.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinawatofautisha kati ya Bernard Morrison na Tuisila Kisinda. Wote ni wachezaji bora sana. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinambeba Bernard Morrison mbele ya Tuisila Kisinda.

Bernard Morrison ni hatari zaidi akiwa karibu na goli kuliko Tuisila Kisinda. Miguu yake inajua vyema goli na anauwezo mkubwa wa kutengeneza magoli kuzidi Tuisila Kisinda. Huu ndiyo mstari unaowatenganisha.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Wachezaji wa Yanga

Mabadiliko ya kiutendaji yaja Yanga..

Simba SC

Yanga, Simba na Azam Ngangari VPL