in

Mkuu wa waamuzi amzungumzia Sterling

Timu ya Taifa ya Italia

“Wajibu wa VAR ni upi? Kutazama kikamilifu kile mwamuzi alichoona. Kwa hiyo, kwa mfano, ikiwa mguu wa kulia haukuwa kwenye mpira bali ulienda moja kwa moja kwenye mguu, basi uamuzi wake ungetenguliwa,” anasema.

Vumbi linatua baada ya kukamilika kwa michuano ya Euro 2020, ambapo Italia walichukua ubingwa kwenye fainali dhidi ya England.

Mengi yametokea humo na wadau wa soka wamechukua wakati wao kwa ajili ya kuchambua mambo – yakiwamo yanayowahusu wachezaji wa Timu ya Taifa ya England – Three Lions, Raheem Sterling.

Mkuu wa Waamuzi wa Euro 2020 anamlinda mwamuzi Danny Makkelie kwa kutoa penati kwa kutoa penati kwa Sterling kwenye mechi ya nusu fainali na pia anatetea uamuzi wa Bjorn Kuipers kutompa kadi nyekundu Jorginho wa Italia kwa kumchezea vibaya Jack Grealish wa England kwenye mechi ya fainali.

Roberto Rosetti anajitetea kwa kuonesha sehemu ya video huku akifafanua kwanini VAR haikutoa marekebisho kwa yoyote kati ya matukio na maamuzi hayo mawili. Penati ya Sterling ilikuja wakati wa muda wa ziada huku England wakiwa sare ya 1-1 na Denmark, baada ya Makkelie kuona kwamba Joakim Mæhle alimwangusha chini mshambuliaji huyo.

Hata hivyo, penati husika iliyopigwa na Harry Kane iliokolewa, lakini mchezaji huyo huyo wa Tottenham Hotspur alikuja kufunga baada ya mpira kurudishwa uwanjani.

Rosetti ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) anasema kwamba hapakuwapo na jaribio hata kidogo la mlinzi huyo kuucheza mpira bali kumkwatua Sterling. Anasema uamuzi ulikuwa safi kabisa na wala sio kashfa.

“Yeye (Makkelie) aliona wazi kwamba mlinzi huyo namba tano hakuucheza mpira. Aliona mguu wa kulia wa mlinzi ukiugusa ule wa kulia wa mchezaji wa England. Hicho ndicho mwamuzi alichoona uwanjani na VAR ikathibitisha uamuzi huo: mchezaji (mwenye jezi nyekundu) hakuugusa mpira. Ni wazi twaweza kujadili mshindilio wa mguso ule lakini wakati wote tunataka mwamuzi awe katikati ya mchakato wa utoaji uamuzi,” anasema mkuu huyo wa waamuzi.

Rosetti hakuishia hapo, bali alichezesha klipu iliyorekodiwa juu ya mahojiano baina ya Makkelie na maofisa wa VAR, huku mwamuzi husika akiambiwa “penati ni sahihi.”

Tanzania Sports
Jamaa akianguka….

Sasa tutazame mkabiliano wa Jorginho kwa Grealish uliokuja wakati wa muda wa ziada baada ya kiungo huyo kuchukua mpira, lakini akaufuata mguu wa mchezaji huyo wa England aliyeingia kuchukua nafasi ya mtu. Rosette anasema kwamba kadi ya njano kwa Kuiper ilifaa, na anatetea hilo kwa kutoa picha.

“Alimwona Jorginho akijaribu kucheza mpira – unaweza kumwona akiweka mguu wake wa kulia kwenye mpira na hii ni wazi kwa asilimia 100, halafu mguu huo wa kulia unateleza kwenye mpira kisha kuna mgusano wa pili kwenye mguu wa mwenye jezi nyeupe namba saba. Mwamuzi aliwaelezea watu wa VAR hasa alichoona uwanjani.

“Wajibu wa VAR ni upi? Kutazama kikamilifu kile mwamuzi alichoona. Kwa hiyo, kwa mfano, ikiwa mguu wa kulia haukuwa kwenye mpira bali ulienda moja kwa moja kwenye mguu, basi uamuzi wake ungetenguliwa,” anasema.

Rosetti anaeleza kwamba mwamuzi anaweza kuuliza ili kuona kitendo kutokea pembe yoyote na kasi za tukio analotaka anapotumia kifuatilia mpira kilicho uwanjani, lakini hatimaye mwamuzi husika huonesha uhalisia wote ulivyokuwa kwa kasi halisi ili kujiridhisha jinsi uchezaji wa klipu kwa taratibu ulivyotia chumvi uhalisia wa kilichotokea.

Rosetti angependa kuona VAR ikitumiwa kwenye mashindano yote ya nyumbani ya Ulaya. Anasema kwamba takwimu kwenye mashindano husika zinaonesha mafanikio kwenye mfumo huo. Kati ya matukio 276 yaliyotazamwa na VAR, masahihisho 28 yalifanywa baada ya mapitio.

Kwenye Euro 2020 iliyochezwa mwaka huu baada ya kuahirishwa mwaka jana kutokana na janga la virusi vya Corona, rafu 1,113 zilifanywa kwenye mechi 51, ikiwa ni wastani wa rafu 21.8 kwa mechi moja.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Jordan Pickford

Makipa Euro, Pickford ni kinara wangu

Yanga Vs Simba

Fainali ya kisasi Kigoma